HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Thursday 11 August 2016

VideoMPYA: Hutotaka hii video mpya ya Dully Sykes na Harmonize ikupite, inaitwa ‘Inde’


Legend wa bongofleva Dully Sykes kamualika mdogo wake kwenye game ambaye niHarmonize na wakakaa juu ya huu mdundo mpya unaitwa ‘Inde‘ alafu wakamuitaDirector Hascana awapigie kichupa, ukishaitazama video yenyewe hapa chini 

Wednesday 10 August 2016

Diamond atoa Tsh 20M kwa ‘GSM’ kusaidia jitihada za upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Diamond atoa Tsh 20M kwa ‘GSM’ kusaidia jitihada za upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi

Msanii wa muziki Diamond Platnumz ametoa msaada wa tsh 20 Milioni kwa ‘GSM Foundation’ kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo ya kutoa huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Diamond na Rais wa GSM

Diamond akikadhi hundi kwa uongozi wa GSM
Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na GSM Foundation imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote.
Raisi huyo wa label ya ‘WCB’ ameonyesha kuguswa na jitihada za taasisi hiyo na kuamua kuchangili kiasi hicho.
“Moyo wangu unaniambia nisingeshikwa mkono ama kusaidiwa na watu basi nami nisingeweza leo hii kufikia hatua hii ndogo niliofikia na ndio maana kidogo nikipatacho huwa napenda kusaidia wenzangu,” aliandika Diamond Istagram. “Leo Mapema nilitembelea ofisi za GSM foundation kuwasilisha kidogo tulichobarikiwa kwa niaba ya WCB. kwajili ya kusaidia watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa (Bobble Head Syndrome) na Mgongo wazi,”
Kwa upande wa GSM Foundation, ameandika:Leo tumepokea hundi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kutoka kwa @diamondplatnumz kama mchango wake kwa #GSMFoundation. Tunamshukuru kwa kuja kututembelea ofisini kwetu na kwa msaada aliotupatia. Mwenyezi Mungu amuongezee pale alipopunguza.

Diamond na Rais wa GSM

Video: Majumba ya kifahari zaidi ya rappers wa Marekani 2016

Top 10 ya nyumba kali za mastaa wa Hip Hop Marekani pamoja na thamani za nyumba hizo kwa mwaka 2016 hii imetolewa na mtandao wa Hot List. Rappers hao ni pamoja na Jay Z, Kanye West, Will Smith, Eminem, Birdman,50 Cent na wengine. Angalia orodha hiyo hapa.

Hii video mpya ya B.o.B ‘$tack of Dreams’ Enjoy



Hii video mpya ya rapa B.o.B  “$tack of Dreams.” kutoka kwneye mixtape yake ya mwezi wa nne ya E.A.R.T.H: Educational Avatar Reality Training Habitat.

Video mpya ya Usher Ft Young Thug ‘No Limit’ itazame hapa.


Hii video mpya ya Usher Raymond ‘No Limit’ aliomshirikisha Young Thug, Dabing imechezwa sana kwenye video hii