HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday 29 April 2016

Picha: Mvua zasababisha taharuki Dar

Siku ya jana ilionekana kuwa ngumu sana kwa wafanyabiashara na wasafiri kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kusababisha kusimama kwa shughuli mbalimbali.
Mvua 3

Mvua iliyonyesha jana jijini Dar es Salaam imeonekana kuwa ni moja ya mvua iliyonyesha kwa muda mrefu tangu mwaka 2016 umeanza na kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa jiji hili.
Mvua 2

April 26, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ilitoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa mvua kubwa ambayo itaambatana na upepo mkali. Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo iliyataja maeneo ambayo yataathirika ni pamoja na Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Visiwa vya Uguja na Pemba.

13102336_1572487909716665_257963960_n
Hata hivyo ripoti hiyo inasema kuwa mvua zitaendelea kuwepo mpaka kufikia Mei 9. Kutokana na utabiri huo wananchi wote tunaoishi kwenye mazingira hatarishi tunatakiwa kuchukua hatua zaidi kabla hatujapata madhara zaidi.

Mvua 1


Mvua hiyo iliyonyesha jana kwa takribani masaa kadhaa iliathiri miundo mbinu mbalimbali na kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wananchi, lakini pia mvua hizo zimesababisha nyumba kibao kujaa maji

Naibu Spika azua sintofahamu bungeni baada ya kumwita mbunge ‘bwege

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, Alhamisi hii amezua sintofahamu bungeni baada ya kumwita bwege Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara (CUF)

mh2

Dk. Tulia alimwita bwege mbunge huyo wakati wa kuchangia mjadala wa hotuba za bajeti za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Utawala Bora.
Kilichomponza mbunge huyo ni hatua yake ya kusimama na kuhoji Bunge kutorushwa moja kwa moja kwenye runinga wakati Naibu Spika akitoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu mjadala uliokuwa ukiendelea.
“Bwege acha ubwege wako hapa… Bwege acha ubwege,” alisema Dk. Tulia huku akionya hatua ya kuzomea ndani ya Bunge.
Baada ya Dk. Tulia kutoa kauli hiyo, mbunge huyo alimjibu kwa kusema si ajabu kumwita bwege kwa sababu hilo pia ni jina lake.
“Bwege ndiyo jina langu, kwani kuna ajabu gani, kwani wewe mwanamume? Ukiitwa mwanamume utajisikiaje?” alisema mbunge huyo ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Bwege’.
Hivi karibuni, mkazi wa Mtaa wa Olasit jijini Arusha, Isaac Habakuk Emily, alifunguliwa mashtaka na Jamhuri akidaiwa kuweka kwenye ukurasa wake wa Facebook ujumbe ulioonyesha kumdhihaki Rais John Magufuli kwa kumwita bwege, huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Ujumbe huo ulisomeka: “Hizi siasa za maigizo, halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana”

Wednesday 27 April 2016

VIDEO: Tatizo la vijana kukosa ajira halijaachwa kimya bungeni leo




Vikao vya Bunge vimeendelea tena leo April 27 2016, katika kipindi cha maswali na majibu
 moja ya Wizara zilizopata nafasi ya kujibu maswali ya wajumbe ni pamoja na Wizara 
ya Kazi, Vijana na Ajira, ambapo swali kutoka kwa Esther Michael Mbunge wa viti
 maalumu aliuliza>>
Serikali kupitia Taasisi za umma zimeweza kufanya tafiti nzuri kujua uhalisia wa
 suala la ajira kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu‘ –Esther Michael
Je, ni kwa namna gani Serikali inaweza kutumia majibu ya tafiti hizo kutatua 
changamoto za ajira katika nchi yetu?’-Esther Michael
Majibu yakatolewa na Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde 
 ‘Serikali kupitia Wizara imekuwa ikifanya au kutumia tafiti mbalimbali 
 kushughulikia changamoto za ajira, upangaji wa mipango na utatuzi wa changamoto
 za ajira kwa vijana wa vyuo vikuu na wengineo‘ 
Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwezeshaji kwa vijana na wahitimu wa
 vyuo vikuu ili kutatua changamoto za ajira katika nchi yetu‘ –Antony Mavunde




UMEWAHI KUMSIKIA PROF JAY AKIONGEA BUNGENI? HUYU HAPA SASA?

 

New >> Huawei MateBook

Huawei MateBook


KEY FEATURES

  • 12-inch IPS quad-HD display
  • Windows 10
  • USB-C
  • Fingerprint sensor
  • 33.4W battery
  • Intel Core M processor
  • 4/8GB RAM
  • Keyboard folio
  • Manufacturer: Huawei
  • Review Price: to be confirmed

Monday 25 April 2016

Raymond asimulia jinsi alivyomshawishi Diamond hadi kumchukua WCB (Video)


Raymond amesimulia jinsi ambavyo alimshawishi Diamond hadi kuamua kumchukua kwenye
 label yake, WCB

12960178_1004660659627506_1027037883_n


Alisema kuwa alipigiwa simu na mshkaji wake, Maromboso aende studio kuungana
naye katika kusikiliza wimbo wa Diamond aliokuwa anataka mawazo ya watu wengi.
“Brother Diamond akifanya ngoma anapenda management yake, kuanzia madancer,
mameneja wote waweze kusikiliza wimbo wake. Katika hiyo crew ya watu waliokuwepo
 Maromboso akapendekeza na mimi niwepo,” amesema

Anasema baada ya kumshauri vitu kadhaa Diamond aligundua ana kitu cha ziada na kumuuliza kisa cha kutotoka hadi muda huo. Amedai kuwa Diamond alimuomba nyimbo zake azisikie na akawa anamshauri vitu vya kurekebisha. Aliendelea kurekodi nyimbo kwenye studio mbalimbali na kuwa anamtumia hadi alipofungua studio ya WCB.
Anasema kuwa kwenye studio hiyo alirekodi nyimbo nyingi kali zilimchanganya Diamond na uongozi wake hadi wakashindwa watoi upi.
Ray ameongeza kuwa Bado ilitoka kwa mbinde kwakuwa kulikuwa na nyimbo zingine kali sana. Mtazame hapo juu kumsikia akielezea.

Sunday 24 April 2016

New Video: Mafikizolo f/ Diamond& Dj Maphorisa – Colors of Africa

Hatimaye unaweza kuangalia video ya wimbo wa Mafikizolo waliomshirikisha Diamond na Dj Maphorisa ‘Colors of Africa

New Video: Lady Jaydee – Ndindindi

Ona video ya wimbo wa Lady Jaydee ‘Ndindindi’ iliyoongozwa na Justin Campos