HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 29 April 2016

Naibu Spika azua sintofahamu bungeni baada ya kumwita mbunge ‘bwege

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, Alhamisi hii amezua sintofahamu bungeni baada ya kumwita bwege Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara (CUF)

mh2

Dk. Tulia alimwita bwege mbunge huyo wakati wa kuchangia mjadala wa hotuba za bajeti za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Utawala Bora.
Kilichomponza mbunge huyo ni hatua yake ya kusimama na kuhoji Bunge kutorushwa moja kwa moja kwenye runinga wakati Naibu Spika akitoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu mjadala uliokuwa ukiendelea.
“Bwege acha ubwege wako hapa… Bwege acha ubwege,” alisema Dk. Tulia huku akionya hatua ya kuzomea ndani ya Bunge.
Baada ya Dk. Tulia kutoa kauli hiyo, mbunge huyo alimjibu kwa kusema si ajabu kumwita bwege kwa sababu hilo pia ni jina lake.
“Bwege ndiyo jina langu, kwani kuna ajabu gani, kwani wewe mwanamume? Ukiitwa mwanamume utajisikiaje?” alisema mbunge huyo ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Bwege’.
Hivi karibuni, mkazi wa Mtaa wa Olasit jijini Arusha, Isaac Habakuk Emily, alifunguliwa mashtaka na Jamhuri akidaiwa kuweka kwenye ukurasa wake wa Facebook ujumbe ulioonyesha kumdhihaki Rais John Magufuli kwa kumwita bwege, huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Ujumbe huo ulisomeka: “Hizi siasa za maigizo, halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana”

No comments:

Post a Comment