Siku ya jana ilionekana kuwa ngumu sana kwa wafanyabiashara na wasafiri
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kusababisha kusimama kwa
shughuli mbalimbali.
Mvua iliyonyesha jana jijini Dar es Salaam imeonekana kuwa ni moja ya
mvua iliyonyesha kwa muda mrefu tangu mwaka 2016 umeanza na kusababisha
adha kubwa kwa wananchi wa jiji hili.
April 26, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ilitoa taarifa kwa umma juu
ya uwepo wa mvua kubwa ambayo itaambatana na upepo mkali. Taarifa
iliyotolewa na mamlaka hiyo iliyataja maeneo ambayo yataathirika ni
pamoja na Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Visiwa
vya Uguja na Pemba.
Hata hivyo ripoti hiyo inasema kuwa mvua zitaendelea kuwepo mpaka
kufikia Mei 9. Kutokana na utabiri huo wananchi wote tunaoishi kwenye
mazingira hatarishi tunatakiwa kuchukua hatua zaidi kabla hatujapata
madhara zaidi.
Mvua hiyo iliyonyesha jana kwa takribani masaa kadhaa iliathiri miundo
mbinu mbalimbali na kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wananchi,
lakini pia mvua hizo zimesababisha nyumba kibao kujaa maji
No comments:
Post a Comment