HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday 10 June 2016

JINSI YA KUMFANYA MSICHANA APENDEZWE NA KUVUTIWA NAWE KABLA YA KUMTONGOZA.


"Umekutana na huyo msichana mzuri kama ua, mcheshi, mrembo na ametulia kwa kila jambo na kwa vyovyote vile nafsi inakusunta inataka umsogelee, moyo haushi kudunda hujui hata pa kuanzia...!"

 Tulikutana na  wakufunzi wetu wa waulize wanaume wa sekta ya mapenzi na kujadili njia zinazofanya kazi na ambazo hazifanyi kazi katika kumfanya msichana apendezwe nawe kwa mara ya kwanza, hizi hapa ni njia za kumfanya msichana apendezwe nawe kwa siku ya kwanza...
  •  Punguza spidi ukiwa unatembea...
Ukiwa unaenda uelekeo wake au ukiwa pembeni yake tayari umeshamsogelea, hakikisha tembe yako iwe taratibu ili uonekane umetulia na unayejiongoza, hii itamfanya akuone unajiamini na kujiamini ni moja ya vitu msichana wanavyovutika navyo, fanya haya huku ukimwangalia machoni bila kukwepesha huku ukitabasamu, hapo ni rahisi kumfanya awe makini na wewe, ila hakikisha umesimama wima na mabega yako yawe katika hali ya usawa.
  • Ongea kwa hali nzuri ukiwa umejipanga...
Kama unaweza kuongea lugha nyingine ongea, au kama unafani yeyote ni muda mzuri umwonyeshe, fani au kipaji huwa vina mvuto mkubwa kwa msichana na kukufanya uonekane wa aina flani ya kupendeza, unatakiwa uingize mambo haya kwa ujuzi kwenye maongezi ili mradi ugusie vitu hivi ili usije onekana wa ajabu au unajikuza, kwenye maongezi kuwa na subira na ingiza mambo hayo katika muda unaohisi unafaa.
  • Ongea kwa sauti na kwa kujiamini...
Sio uongee kwa nguvu, inatakiwa unaongea kwa sauti ambayo inasikika, na iwe sauti yako asilia na isiwe inatetemeka, sauti iwe ni ya kujiamini na isiwe ya kuwa makini sana, iwe nyepesi yenye utulivu isio ya kuhoji, hakikisha umevuta pumzi mara kadhaa ili kujinga kujiamini kwenye sauti yako
  • Hakikisha akili yako yote ipo kwake...
Ukiwa nae hakikisha ajione kama yupo mwenyewe pekee kwenye dunia yako, hata kama kuna sahani zimepasuka au msichana mzuri zaidi yake anapita karibu yenu, hakikisha macho yake yote yawe kwake, msikilize anacho ongea na onyesha hamasa kwa anayoyaongea, kumwangalia machoni utamfanya akuzoee haraka.
  • Mchezee kwa maneno...
Hisia zako, unaweza sema uende nae taratibu ili upate kumjua, ila huu ndo wakati wako hivyo usipoutumia vilivyo, huyu ndege anaweza kupaa!, hakikisha unaanzisha ubishi na tumia maneno ya uchangamfu, unaweza anzisha ubishi hata kwa wasanii wa nyimbo anazopenda kuzisikiliza, hii itakufanya akuzoee mapema zaidi na anaweza kujikuta mkajisahau kabisa kama ndo mmekutana na kwa kutumia ubishi utamfanya afurahie na kucheka pamoja na kujisikia vizuri na kuhisi yupo katika mazingira aliyoyazoea, na kujikuta akipendezwa sana nawe.
  • Mchukua na mpeleke kwenye mgahawa mzuri wa karibu...
Kama unataka mapigo yake ya moyo yaongezeke na usiishe kwa kumshangaza, mtoko wa karibu kwenye chakula au nyama choma na kapire ni jambo zuri unaloweza kufanya, kama anapendelea pili pili, ni vizuri mkaitumia, pili pili huongeza hamu ya kula na muwasho wa kusababisha maongezi yanoge zaidi hivyo kusababisha furaha na vicheko kutokukatika, ikiwezekana agiza chakula mnacho weza kula kwa pamoja.
  • Jidhalilishe kwa stori za vichekesho...
Wanawake wanapenda kucheka na stori za hapa na pale, mwadisie kipindi ambacho ulikutwa na majanga ambayo yanavichekesho ndani yake, stori kama ulikua pembeni ya bara bara, gari likapita kwa kasi na kukanyaga maji machafu na kukuta umelowa mwili mzima, mwonyeshe kwake huogopi kitu, na ukiwa naye unaridhika na unaweza ongea kitu chochote
 
 

ISHARA KUBWA TATU ZA MWANAMKE ALIYEKUZIMIA KISAWASAWA.

Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupeda kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na haraka kumtolea uvivu huyo mwanamke.


* Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, atahangaika juu ya usalama wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke huyo anaupendo na wewe.
* Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,Wivu ni ishara kuwa anakupenda wewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa.Japo wivu ukizidi sana pia inaweza kuleta tatizo


* Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia ww macho/uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia ww kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.
* Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine,mara nyingi atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa “NJOO NIKO KWAAJILI YAKO.”
Hivyo kama ulikuwa unahisi unamhitaji basi ni wakati mwafaka wa kumfuata na kumweleza ukweli na kirahisi nakuhakikishia unabeba mzigo kwani ni mtu tayari aliyekuwa anahisia kali za mahaba juu yako
 

No comments:

Post a Comment