HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 30 September 2016

PICHA: Majiji yanayoongoza kwa kutembelewa zaidi duniani


Leo September 26, 2016 nafahamu utakua unayajua majiji mengi kutoka kwenye nchi tofauti tofauti na huenda umeshatembelea huko au kwa kuyaona kwenye picha, Sasa leo nakusogezea hapa list ya Majiji yaliyotajwa na taasisi ya The Mastercard’s Global Destination Cities Index ikiyaweka kwenye majiji yanayotembelewa zaidi duniani.
List hii imetoka baada ya kukusanya taarifa za majiji hayo za miaka Saba kuanzia mwaka 2009 mpaka 2016. Bara la Asia limechukua headlines kwa kuingiza Majiji 11, wakati hakuna jiji lolote lililoingia kutoka Bara la Afrika.
Hii ndio List kamili ya majiji 20 yaliyotajwa kutembelewa zaidi duniani.
20. Prague, Jamhuri ya Czech
Jiji hili limetajwa katika nafasi ya 20 likiwa idadi ya watu Milioni 5.81 wanaolitembelea kika siku.

19. Shanghai, China
Hutembelewa na watu Milioni 6.12 kwa siku.

18. Vienna, Austria
Hutembelewa na watu Milioni 6.69 kila siku.

17. Osaka, Japan 
Hutembelewa na watu Milioni 7.02 kila siku.

16. Roma, Italy

15. Taipei, Taiwan
Hutembelewa na watu Milioni 7.35 kila siku.

14. Milan, Italy
Hutembelewa na watu Milioni 7.65 kila siku.

13. Amsterdam, Uholanzi
Hutembelewa na watu Milioni 8 kila siku.
Amsterdam Nederland Amsterdam Netherlands city night sunset home church cathedral buildings roofs roads cars street lights exposure
12. Barcelona, Hispania
Hutembelewa na watu Milioni 8.2 kila siku.

11. Hong Kong, China
Hutembelewa na watu Milioni 8.37 kila siku.

10. Seoul, Korea Kusini
Hutembelewa na watu Milioni 10.2 kila siku.

9. Tokyo, Japan
Hutembelewa na watu Milioni 11. 7 kwa siku.

8. Istanbul, Uturuki
Hutembelewa na watu Milioni 11.95 kila siku.

7. Kualar Lumpur, Malaysia
Hutembelewa na watu Milioni 12.02 kila siku.

6. Singapore
Hutembelewa na watu Milioni 12.11 kila siku.
Singapore city night
5. New York, Marekani
Hutembelewa na watu Milioni 12.75 kila siku.

4. Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu
Hutembelewa na watu Milioni 15. 27 kila siku.

3. Paris, Ufaransa
Hutembelewa na watu Milioni 18.03 kila siku.

2. London, Uingereza
Hutembelewa na watu Milioni 19.88 kila siku.

1. Bangkok, Thailand
Hutembelewa na watu Milioni 21.47 kila siku.


RIPOTI ya Benki ya Dunia kuhusu Uchumi wa Tanzania na Rwanda iko hapa..


Taarifa hii kutoka Benki ya Dunia ambayo imetoa ripoti ya ustawi wa uchumi wa Afrika ambapo nchi za Afrika Mashariki za Tanzania na Rwanda zinaonekana kuwa na uchumi wenye kustawi kwa wastani.
Ripoti mpya ya Benki ya dunia itolewayo mara mbili kwa mwaka, Africa’s Pulse, inaonesha kuwa mwelekeo wa ukuaji uchumi barani Afrika unatarajiwa kudorora zaidi na kuwa asilimia moja nukta sita mwaka huu ikilinganishwa na asilimia tatu mwaka jana.
Hata hivyo imebainisha kuwa, mwelekeo wa ukuaji unatofautiana ambapo baadhi ya nchi ustawi umedorora huku nyingine uchumi unakua. Kwa mfano Rwanda, Tanzania na Ethiopia zimetajwa kuwa nchi zenye ustawi wa wastani ambao ni zaidi ya asilimia sita kwa mwaka, huku Cote d’Ivoire na Senegal zikiongoza kwa kasi ya ustawi barani Afrika.
Mchumi Mkuu wa Benki ya dunia kuhusu Afrika Albert Zeufack amesema chanzo cha kukwama ustawi wa uchumi ni kudorora kwa bei za bidhaa ikiwemo mafuta, hali ngumu ya kifedha na sera za uchumi zisizo makini.
Benki ya Dunia inasema mwelekeo ni kupanua wigo wa bidhaa zinazouzwa pamoja na kuboresha sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo ili kuinua vipato vyao na kupunguza umaskini.

Video: Patoranking ft. Phyno – Money


Patoranking takes it a notch higher by pleasuring us with the official video to one of the hit tracks off the album, Money.
The song which features the Fada Fada crooner, Phyno has for its video an amazing interpretation of the song

Thursday, 29 September 2016

Video: Marota – Bila Wewe

Msanii mchanga wa muziki, Marota ameachia video yake mpya ya wimbo ‘Bila Wewe’. Video imeandaliwa na director Jackson Joachim.

Video: Goodluck Gozbert – Hao Hao


Muimbaji wa Gospel, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki, Goodluck Gozbert ambaye pia anafahamika kwa jina la Lollipop ameachia rasmi Video yake mpya ya wimbo unaitwa “Hao Hao”. ambao huu wimbo unapatikana katika album yake iitwayo ‘Ipo Siku’. Angalia hapa chini

Ndalichako aitaka bodi mpya ya TCU kukaza msuli

Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ameitaka bodi mpya ya tume ya vyuo vikuu TCU kushughulikia changamoto zilizopo katika tume hiyo baada ya ile iliyokuwepo kuvunjwa.

ndalichako
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo, Profesa Ndalichako, alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusiana na vyuo wanavyosoma hivyo ni wakati wa bodi hiyo kufuatilia kwa ukaribu malalamiko hayo na kuyafanyia kazi.
“Tunaelewa kuwa wanafunzi ni watu wa kulalamika kila wakati, lakini yapo malalamiko ambayo yana tija na ni lazima yatatuliwe,” alisema. “Kwa mfano nilipokea malalamiko kutoka chuo kikuu cha Ifakara mwezi Mei mwaka huu kuhusiana na walimu wa chuo hicho kuvuruga matokeo yao lakini chuo hicho hakijatoa maamuzi yoyote mpaka leo hivyo kuwaacha wanafunzi kubaki nyumbani na kutokujua nini hatma yao,” alieleza Profesa Ndalichako.
Aidha alisema TCU ina mamlaka ya kuvifuatilia vyuo vyote vikuu nchini, pamoja na kufuatilia utendaji kazi wa vyuo hivyo ikiwa unaendana na viwango vilivyowekwa.

Future kutumbuiza kwenye MTV MAMA pamoja na Diamond na Alikiba




cthe7wfxeaaduu2
Rapper wa Marekani, Future, ametangazwa kuwa msanii wa nje ya Afrika atakayetumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA, Oktoba 22.

Future ataungana na Alikiba na Diamond na wasanii wengine wa Afrika kwenye orodha ya wale watakaotumbuiza jioni hiyo jijini Johannesburg.
“We are proud to announce that @1future will be joining for the #MTVMAMA2016!!! #FutureMTVMAMA,” wameandika MTV Base kwenye Twitter.
Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Nayvadius DeMun Wilburn ana album nne hadi sasa, Pluto (2012), Honest (2014), DS2 (2015) na EVOL (2016).

VIDEO: Babu Tale ameongelea ukaribu wa Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz

Najua kama utakuwa mfuatiliaji wa mastaa wa bongoflevani utafahamu ukaribu aliyokuwa nao Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz hapo awali ambapo pia walishafanyaga collabo ya pamoja na mwanadada kutoka Kenya, Victoria Kimani ya ‘Prokoto‘ na walikuwa wakionekana mda mwingi wapo pamoja hata kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram wakipost picha wako pamoja.
Lakini kwa sasahivi imekuwa kimya na inaonekana kila mtu anafanya issue zake na hii imeleta utata kwa mashabiki kuhisi kuwa labda kuna beef kati yao ama vipi, a majibu yake…
>>>’Sijawah kuwaona hivi karibuni labda kwasababu kila mtu mmoja anapiga issue zake lakini me na Ommy tulisafiri wote na Naseeb mpaka uingereza na tukafanya video ya BamBam sijawahi…

PICHA : Ndege inayotajwa kwa ubora na yenye starehe kuliko zote duniani


 Ndege inayotajwa kuwa na starehe za kutosha ikiwa imetengenezwa ubora kuliko Ndege yoyote ile duniani. Ndege hii inafahamika kama “World’s Most Luxurious Commercial Jet ikiwa na jina la kibiashara Crystal
crystal-luxury-air-global-express-xrs
Crystal Plane ina mgahawa wa kisasa zaidi kuliko hata migahawa ya mitaani, Bar ambayo ni Classic sana, pamoja na huduma ya Internet yenye kasi zaidi ya Wi-Fi… Ndege hii inamilikiwa na kampuni kutoka nchini Marekani. 
Gharama za kuikodi ndege hii ni dola za Marekani elfu hamsini kwa siku moja huku abiria akipewa huduma ya hadhi ya hoteli ya five star. Ndege hii inatarajiwa kuanza kutumika na wateja ifikapo mwaka 2017.
Nimekusogezea hapa picha za ndani ya ndege hiyo mtu wangu.
cy2
cy3
cy4
cy5
cy6
cy7
cy8
jet-1
ULIPITWA NA KAULI YA BABU
Mtu wangu wa nguvu leo nimeipata hii ya Ndege inayotajwa kuwa na starehe za kutosha ikiwa imetengenezwa ubora kuliko Ndege yoyote ile duniani. Ndege hii inafahamika kama “World’s Most Luxurious Commercial Jet ikiwa na jina la kibiashara Crystal
crystal-luxury-air-global-express-xrs
Crystal Plane ina mgahawa wa kisasa zaidi kuliko hata migahawa ya mitaani, Bar ambayo ni Classic sana, pamoja na huduma ya Internet yenye kasi zaidi ya Wi-Fi… Ndege hii inamilikiwa na kampuni kutoka nchini Marekani. 
Gharama za kuikodi ndege hii ni dola za Marekani elfu hamsini kwa siku moja huku abiria akipewa huduma ya hadhi ya hoteli ya five star. Ndege hii inatarajiwa kuanza kutumika na wateja ifikapo mwaka 2017.
Nimekusogezea hapa picha za ndani ya ndege hiyo mtu wangu.
cy2
cy3
cy4
cy5
cy6
cy7
cy8
jet-1

Wednesday, 28 September 2016

Mo Dewji awatishia nyau Yanga ‘lazima wakae’


mohammed-dewji-702x336

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kupigwa kwa mechi ya wa watani wa jadi, Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumamosi ya Oktoba mosi, tayari tambo za mashabiki zimeanza.



Shabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’ ameandika ujumbe wa utani kwa mashabiki wa Yanga na kuwaambia kuwa siku hiyo watachezea kichapo.
mo-dewji
“Yanga lazima wakae, kandambili mahali pake ni uwani. #SimbaNguvuMoja,” aliandika MO.
Hivi karibuni uongozi wa Simba ulikub

Video: The Game – ‘Pest Control (Meek Mill Diss)’

The Game’s Meek Mill disses continue to pour in, but this time in visual form. After “92 Bars” and “Pest Control,” the Compton spitter unleashes a music video for the latter, a scathing barrage of bars over Young M.A.’s “Ooouuu” instrumenta

 

Tecno wazindua Phantom 6 na Phantom 6 Plus zinazoleta mapinduzi ya teknolojia

Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya simu Afrika, Tecno Mobile imezindua simu mbili matata za Phantom 6 na Phantom 6 Plus katika tukio lililohudhuriwa na watu maarufu kibao katika hoteli ya Armani ambayo ipo katika jengo refu zaidi duniani Burj Khalifa.

unveiling
Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO YA TECNO PHANTOM 6
“Imetuchukua takribani miaka 3 katika matengenezo yake na imehusisha zaidi ya wahandisi laki 5,” alisema Mkuu wa Masoko wa Tecno, Vane Ni.
“TECNO Phantom 6 inawapa watumiaji wa simu za mkononi utulivu bora pindi wanapotumia, kasi na kamera bora na nzuri ili kufurahia zaidi simu ya mkononi,” alisema Naibu Kiongozi wa Masoko wa Tecno Nigeria, Attai Oguche.
Uzinduzi ulifana sana ambapo kulikuwa na zaidi ya vyombo vya habari 70 tofauti kutoka nchi mbalimbali duniani kote na miongoni mwa mastaa waliohudhuria ni mwanamuziki mahiri wa Tanzania, Alikiba na mwanahabari ‘Mtuwa Nguvu’ Millard Ayo ambaye alishinda safari ya kwenda China.
millard
Pichani ni mwanahabari wa Tanzania Millard Ayo akitangazwa mshindi wa safari ya China
ali-kiba
Mwanamuziki wa kimataifa wa Tanzania, Alikiba akiwa na kifaa kipya cha Phantom 6 akifanya mauzungumzo
Baada ya uzinduzi huo Tecno Tanzania ikatangaza kwamba Phantom 6 na Phantom 6+ zitaanza kupatikana rasmi kuanzia tarehe 8 Oktoba 2016 katika duka la Tecno lililopo City Mall Posta ambapo wateja wote watakaonunua Phantom 6 siku hiyo watapatiwa vifurushi vya zawadi na kutakuwa na zawadi kubwa nono.
Pia wakatangaza kwamba kuanzia Jumatatu tarehe 3 Oktoba wateja watajaza fomu maalum ili kuweka oda zao na watazawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo T-Shirts, mabegi, T-Band na Sefie stick siku ya kuanza mauzo hiyo tarehe 8 Oktoba.
Kuhusu bei kwakweli Tecno wameangalia hali halisi ya uchumi kwa sasa ambapo gharama itakuwa kati ya Tsh 500,000 – Tsh 600,000.
untitled
Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno nahakikisha hukosi moja wapo ya simuhizi kali ambazo zimekuja kufanya mageuzi ya teknolojia.