HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Saturday, 18 June 2016

Vanessa Mdee kuwania tuzo ya msanii bora wa kike wa Afrika katika tuzo za NEA Awards 2016



Mkali wa wimbo ‘Niroge’, Vanessa Mdee amechaguliwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kike wa Afrika katika tuzo za NEA Awards 2016 za nchini Nigeria.
Vanessa
Muimbaji huyo amekuwa ni msanii pekee wa Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo huku Kenya ikiwakilishwa na Victoria Kimani katika kipengele hicho hicho.
Wasanii wengine anaoshindana nao katika kipengele hicho ni, Efya Ghana, Lira (SA), MZ Vee (GH), Sheebah Ndiwanjawulo (UG), Adiouza (SN) Knowless Butera (RW).
Aidha msanii bora wa kiume wa Afrika/ Nje ya Nigeria, kundi la wasanii wa Kenya, Sauti Sol linachuana vikali na wasanii wengine kama Stonebwoy na Sarkodie wote wa Ghana
Hi ndiyo list nzima.
Best Album
Y.A.G.I (Lil Kesh)
Applaudise (Iyanya)
Eyan Mayweather (Olamide)
Ghetto University (Runtown)
R.E.D. (Tiwa Savage)
Stories that Touch (Falz)
Seyi or Shay (Seyi Shay)
Mama Africa (Yemi Alade)
Wanted (Wande Coal)
Hottest Single
Oshinachi (Humblesmith)
Duro (Tekno)
Baba Nla (Wiz Kid)
Lagos Boys (Olamide)
Mama (Kiss Daniel)
Jagaban (Ycee)
Best Song
Pick Up (Adekunle Gold)
Oluwa Ni (Reekado Banks)
Vow (Timi Dakolo)
You Suppose know (Bez)
Type of Woman (Iyanya)
Go On (Niyola)
​Best Collabo
Moniegram (Mr. 2Kay ft. Timaya)
Romantic (Korede Bello ft. Tiwa)
My Woman, My Everything (Patoranking ft Wande Coal)
Yaya Oyoyo (Lil Kesh ft. DaVido)
Reggae Blues (Harry Song ft Others)
Your Number (Ayojay ft. Fetty Wap)
Sekem (MC Galaxy ft Swizz Beats)
Finally (Masterkraft ft. Sarkodie, Flavour)

Best Live Performer
Omawumi
Tuface
Solidstar
Yemi Alade
Dbanj
MC Galaxy

Best Music Video
Emergency (Dbanj Dir. Unlimited LA)
Right Now (Seyi Shay Dir. Meji Alabi)
Condo (Kuammy Dir. Moe Musa)
Karishika (Falz Dir. Aje Films)
Duro (Tekno Dir. Patrick Elis)
If I Start to Talk (Tiwa Dir. CP)
Quality (Pasuma Dir. HG2)
Sisi (Sexy Steel Dir. Chad Tennies)

African Male Artist (Non Nigerian /Africa)
Stonebwoy (GH)
FA (LIB)
Sarkodie (GH)
Sauti Sol (KQ)
Deng (LIB)
Papa Denis (KQ)
Bisa Kdei (GH)
Eric Geso (LIB)
Shattawale (GH)

African Female Artist (Non Nigerian /Africa)
Vannessa Mdee (TZ)
Efya (GH)
Lira (SA)
MZ Vee (GH)
Sheebah Ndiwanjawulo (UG)
Adiouza (SN)
Victoria Kimani (KQ)
Knowless Butera (RW)

Mtoto wa T.I akamatwa kwa kosa la kubeba silaha bila kibali



Mtoto wa kufikia wa rapper wa Marekani, T.I anayejulikana kwa jina la Zonnique Pullins alikamatwa siku ya Alhamisi kwenye uwanja wa ndege wa Hartsfield-Jackson Atlanta International Airport kwa kosa la kubeba silaha bila kibali.
02a41cbd1ae9e24aa9bc7871c95742d2
Zonnique Pullins (20) ambaye mama yake mzazi ni Tiny Harris alikamatwa baada ya kuonekana kwenye mitambo ya X-ray kuwa amebeba silaha hiyo na alipelekwa kwenye kituo cha Clayton County, lakini aliachiwa kwa dhamana siku ya Ijumaa.
Binamu yake na Zonnique Pullins, kupitia akaunti yake ya instagram aliandika:
My boo got the cutest mugshot in the game. Let me just clear a couple things up for you guys . Zonnique did get caught with her registered weapon but like most of us she just forgot it was in her really big purse. We were taught in my family that people are crazy out here and carrying a small gun to protect yourself is what’s needed . With the late shootings and death of a pop star all in Orlando just this week , I think it’s very appropriate that she carries a gun just not to the airport maybe lol. But my girl is home and good so please don’t start with the ignorant rumors , she was home and handled before you even heard about it. Zonnique has great parents that made sure she was okay from the moment she was caught. Not all celebrities keep security on them 24/7 they have to protect themselves just like regular people and we all have learned even security can’t always protect you . Her mugshot is still cute as hell lol
Hivi karibuni nchi ya Marekani imekumbwa na mauaji mengi ya watu waliouawa kwa silaha.

New Video: Calvin Harris f/ Rihanna – This Is What You Came For



Video ya wimbo wa mpya wa Calvin Harris aliomshirikisha Rihanna ‘This Is What You Came For.’

Machozi kwa Ray C, matumaini mapya kwa Chidi Benz



Wiki hii mioyo yetu inaweza kuwa imeanza kupoteza matumaini kwa dada yetu, Rehema Chalamila, wamjua zaidi kama Ray C au kama ukitaka kumpa jina lenye sifa zake, basi yafaa umuite ‘Kiuno Bila Mfupa.’
image
Ni baada ya kusambaa video inayomuonesha akiwa katika hali inayosikitisha akibebwa kwenye gari la polisi, si kwa kutenda kosa, bali kwa kumuokoa kutoka kwenye hatari ya kujidhuru yeye mwenyewe.
Inadaiwa kuwa muimbaji huyo alionekana akipiga kelele, kujitupa kwenye matope na kutafuta kisu ajichome. Hali aliyofikia Ray C inatisha na kiukweli vita yake dhidi ya uraibu wa madawa ya kulevya imekuwa ndefu, ngumu, inayokatisha tamaa na ni kama sasa ameamua kuweka silaha chini, ameshindwa.
image
Kwa kauli yake mwenyewe, Rehema alidai kuwa arosto wanayopata mateja si ya mzaha na ndio sababu kubwa inayowafanya washindwe kuacha. Mwili huuma kama unapondwa na kitu kizito, mambo hayendi bila kupata starter ya unga na kwao kuishi na arosto ni sawa na kuianza jehanamu kabla ya wakati. Hupata mateso makubwa na kwakuwa uraibu huo hauhusishi mwili tu, bali hisia na kisaikolojia, wengi hushindwa kuhimili nguvu yake.
Miaka mitatu iliyopita, Ray C aliacha kabisa madawa ya kulevya na kuwa mtetezi mkubwa na muhimu wa waathirika wa unga. Alianzisha taasisi yake na akawa anawatembelea waathirika wa madawa hayo akiwemo yule dada aliyekuwa model kwenye video ya Ice Cream ya Noorah. Ray C akawa ‘bad girl gone good’ na kuwa mvuvi mzuri wa mateja aliowahimiza kwenda kuchukua dawa ya Methadone aliyokuwa akitumia pia.
Baada ya miaka miwili, tetesi za kuwa amerejea tena kwenye matumizi ya madawa hayo, zikarudi. Alizikana vikali na kutishia kuishtaki kampuni ya Global Publishers iliyoandika habari hiyo. Ni hadi wiki hii iliposambaa video hiyo kila mtu akaamini tetesi hizi kumbe ni za kweli.
Wakati wengi wakitoka machozi ya huruma kwa Ray C na wasijue watamsaidiaje awamu hii, kuna matumaini mapya kwa Chidi Benz, kipaji kingine kilichopotezwa na uraibu.
Chidi Benz amewahi kujaribu njia nyingi na za aina tofauti tofauti za kutaka kujiondoa kwenye matumizi ya madawa hayo. Amewahi kwenda Kenya ambako swahiba wake Nonini alitumia gharama kubwa kufanya process ya kitaalaam kumsaidia lakini ilishindikana. Inasemekana pia kuwa Diamond amewahi kumsaidia katika hilo lakini walichemka.
Chidi amepitia mengi ya kutisha zaidi katika utumiaji wa madawa ya kulevya huku akiwa msanii wa kwanza kuwahi kushtakiwa na kesi ya kukutwa nayo. Kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege wa JNIA akielekea Mbeya iligeuka kuwa jinamizi ambalo kama angecheza lingempeleka jela.
Mungu alimsaidia kwa kupewa hukumu iliyokuwa na option ya faini na akawa mtu huru. Baada ya hapo Chidi akawa kimya tena licha ya kuwahi kutoa wimbo aliowashirikisha Diamond na AY. Alikuja kuwashtua mashabiki wa muziki miezi kama miwili iliyopita baada ya kuonekana kwenye interview na kipindi cha D’Weekend Chatshow cha Clouds TV ambapo afya yake ilikuwa ya kutisha.
Chidi hakuwa tena yule rapper mwenye mwili wa miraba minne. King Kong alikuwa amedhoofika utadhani mgonjwa wa Kifua Kikuu. Muonekano huo uliwatisha watu wengi na hivyo kumfanya Babutale aingilie kati na kumpeleka kwenye kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya cha Life and Hope Rehabilitation akishirikiana na Kalapina.
Fast forward.. Chidi ametoka na wiki hii ameonekana akiwa na muonekano tofauti unaotia moyo. Kupitia akaunti yake mpya ya Instagram, Chidi ameanza kurudisha matumaini mapya na kiukweli mashabiki wamefurahi. “Kesheni mkiniombea. Trust me, Your kingkong is coming back soon,” ameandika kwenye picha moja.
image
Rapper huyo ameonekana kuwa karibu na si Babutale tu, bali WCB kwa ujumla kiasi cha kuwepo na dalili kuwa huenda akaungana na akina Rich Mavoko, Raymond na Harmonize. Si jambo gumu kwakuwa kwa muda mrefu Diamond amekuwa akionesha nia ya kumsaidia rapper huyo.

imageWakati tukiendelea kumweka Chidi kwenye maombi yetu kama anavyotuomba, tumkumbuke pia dada yetu Ray C ambaye kwa hakika anahitaji maombi zaidi na matumaini mapya.

Kauli ya TCRA katika mchakato endelevu wa kuzima simu feki



Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy amesema kuwa mtambo wa kuzima simu bandia unaendelea na kazi kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazikuwa hewani zitakapowashwa hazitafanya.
????????????????????????????????????
Alisema kuwa simu feki ambazo hazikuwa hewani usiku wa kuamkia juzi zitakapowasha hazitafanya kazi kwa kuwa mtambo wa kuzima Imei bandia unaendelea kuhakiki simu hizo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy amesema jana kuwa mtambo wa kuzima simu bandia unaendelea na kazi kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazikuwa hewani zitakapowashwa hazitafanya.
“Kazi ya kuzima simu hizo ilianza usiku kumkia juzi saa sita usiku na kila kampuni ya mtandao wa simu ilipaswa kuzima simu za wateja wake ambazo ni feki na kazi ya mtambo ni kuhakikisha simu iliyozimwa inapowekewa kadi ya mtandao mwingine haifanyi kazi na kuhakikisha simu zote feki zitakazoingia nchini hazifanyi kazi,” amesema Mungy.
Baadhi ya wananchi waliozimiwa simu wameilalamikia Serikali kwa kuwasababishia hasara kwa madai ya kutokuwa makini katika kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki.
Pendo Mpomelo, mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam alisema simu yake ilikosa mawasiliano kuanzia saa saba usiku

Miley Cyrus avishwa pete ya uchumba na Liam Hemsworth



Msanii wa Marekani, Miley Cyrus amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake muigizaji wa filamu, Liam Hemsworth.
beyonce-detroit
Jumanne hii Miley alionekana akiwa na mpenzi wake huyo huko New York huku kwenye kidole chake cha mkono wa kushoto akionekana na pete inayodhaniwa ya uchumba yenye thamani ya dola laki moja.
11821164_1639903142954587_408394810_n
Kuvalishwa pete ya uchumba na Liam Hemsworth ni neema kwa Miley Cyrus kwani aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mtoto wa staa wa filamu duniani Arnold Schwarzenegger, Patrick Schwarzenegger na kudumu kwa miezi mitano pekee kwenye mahusiano lakini pia aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Justin Bieber.

Kutoka TCRA wametoa ufanunuzi wa kufungiwa kwa simu feki….

Mix


Ni June 16, 2016 ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki walizifungia simu feki zenye IMEI bandia
Sasa millardayo.com imepata meneja wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy na kueleza idadi ya IMEI zilizokamata na mtambo wao ambao umehusika kuzifungia simu feki.
‘Tukizungumzia ambavyo vimezimwa kinachofanyika kuzifunga zile IMEI bandia ambazo kwa jana tumefanikiwa kuzifunga simu zenye IMEI zipatazo laki sita na elfu 3 kwa maana ya kwamba unakuta simu moja ina IMEI mbili kwasababu simu yenye laini mbili ina IMEI mbili sasa ziko simu zenye IMEI hadi nne‘- Innocent Mungy
Kwahiyo ambacho tumeblock jana usiku ni IMEI laki sita ikiwa ina maana ni ambazo zinatumika kwenye simu feki, modem ya internet na IPAD, sasa sisi hatuwezi kutaja idadi ya simu ngapi tumezifungia ila tunachokijua ni kwamba IMEI laki sita ndio zimefungiwa zilizopo kwenye simu– Innocent Mungy
Zoezi hili bado linaendelea ambapo sasa hivi mtambo utakuwa unahakikisha simu zinazoingia bandia zitakuwa zinafungiwa, IMEI ni namba tambulishi  kama unakumbuka tulisema kwamba kila simu inayotengezwa inapewa namba tambulishi, sasa simu ili itengenezwe lazima ipite kwenye mchakato wa kuhakikisha kuna vitu ambavyo havitakiwi viwepo kwenye simu- Innocent Mungy
KAMA ULIIKOSA HII YA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ALIVYOGEUZA GARI AKIELEKEA KAZINI ITAZAME HII VIDEO HAPA

VIDEO: Dogo Janja yuko tayari Diamond ampigie hata mruzi tu iwe kolabo



Dogo Janja ni msanii wa bongofleva ambaye amerudi kwenye game baada  ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kufanya muziki, hapa alikaa kwenye OnAIR with Millard Ayo na kuongelea msanii anayetamani kufanya nae kolabo.
Unaweza kuangalia Video hii hapa chini
Dogo Janja ni msanii wa bongofleva ambaye amerudi kwenye game baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kufanya muziki, hapa alikaa kwenye OnAIR with Millard Ayo na kuongelea msanii anayetamani kufanya nae kolabo. Unaweza kuangalia Video hii hapa chini ULIKOSA HII EXCLUSIVE YA DOGO JANJA AMBAYO HATAYASAHAU, SHULE MUZIKI NA MAISHA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHIN

VIDEO: Ninayo takwimu ya madini yanayotafutwa kwa wingi duniani hivi sasa

Huwenda haijawahi kukufikia kuhusu thamani ya baadhi ya madini yaliyopo duniani, June 17 2016 nakukutanisha na Waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo alisimama bungeni Dodoma na kutusogezea hii takwimu ya baadhi ya madini yanayotafutwa sana kwa sasa duniani ULIIKOSA HII? WABUNGE WAWILI CHADEMA WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO KWA KULIDANGANYA BUNGE

Friday, 17 June 2016

Video: Ray C apewa msaada na Jeshi la polisi ya baada kuzidiwa


Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C usiku wa jana alikamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Kinondoni Manyanya almaarufu ‘Kinondoni kwa Mpemba’ jijini Dar es salaam baada ya kupiga makelele barabarani akidai anataka kutekwa.
Ray C akiwa kwenye gari la polisi
Ray C akiwa kwenye gari la polisi
Muimbaji huyo mahiri ambaye ameathirika na Matumizi ya madawa ya kulevya, alidaiwa kufika katika eneo hilo na kuomba msaada lakini baadae aliomba kisu ili ajichome kuhu akiongea vitu visivyoeleweka.
Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni msanii wa filamu, Esha Buheti kupitia instagram yake aliandika ujumbe huu:

Nashindwa hata niongee nini jamani, rayc Leo kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie rayc, I mean it jamani siku zote nlikua najua anaonewa ila nlichokishuhudia leoo nimeumiaa kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje? . Nilikuwa na Kabula Kinondoni kwa wapemba tumefata chips mara tukaskia mtu anasema me Rayc nataka kuvua nguoo, nikajua utani kushuka ni Ray C anasema nishikeni kuna watu wanataka kuniteka, alikua na nguvu sana watu kamshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaaanza kugaragara kwenye matope akipiga KELELE kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari YA polisi ikambeba ila kwa tabu sanaa alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpk rayc anaondoka na ile gari yapolisi sikujua anapelekwa wapi alikua kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?
Baada ya ujumbe huo, aliamua kupost video tena na kuandika:

Ray C hastahili haya jamani kweli Leo hii anafikia hatua hii? Najua hajitambui ila tumfikirie mwanamke mwenzetu ambae ni mamaake, anajiskiaje? Rayc nn kimekupata ? Hiii video inasambaa kila sehem kweli huyu ndo RAYC AMBAE NI NEMBO YA TAIFA? Plz tumsaidie manake tusimhukumu? MBONA sisi kila siku mungu tunamkosea na hesabu makosa yetu? We need to do something jamani @tzshaderoom @mangekimambi_ @divathebawse @babutale @ @mwanafa @linexsundaymjeda @paulmakonda naomba tumstiri huyu mtu plz plz @lisa_fickenscher ( tunafanyaje kumsaidia jamani tusichoke me natamani aende rehab mwaka mzima) Leo rayc umedhalilika najua haikua akili yako mama DAAAAH hata sijui amepelekwa wapi maskini 😢😢 atakua amelala wapi? Vipi kuhusu kesho Yake? Mamaake anajiskiaje? Inaumaa jamani tusikubali kumpoteza huyu dada nawaombaa 🙏🙏🙏 tusaidiane @millardayo @rayc1982 my love kama hauko sawa jamani ongea na watz wapo tayari kujitolea kwa hali na mali my love,

Video: Pool Party ya Trey Songz yazua ugomvi




Tumia pesa ikuzoee, msemo huu umekuwa ukitumiwa na mastaa wengi wa Marekani pindi wanapokuwa wana fedha nyingi lakini wengi waliutumia msemo huu mwisho wameishia kufilisika kama DMX, Soulja Boy na wengine wengi.
3549C67E00000578-3642164-image-m-42_1465959567184
Wikiendi iliyopita staa muziki wa R&B wa Marekani, Trey Songz aliandaa sherehe ya ‘Pool Party’ iliyofanyika ndani ya nyumba yake huko Virginia.
Trey Songz alitumia zaidi ya $80k kuandaa sherehe hiyo ikiwa ni pamoja na dola 50,000 aliyotumia kwa ajili ya vinywaji kwenye sherehe hiyo na dola 8,000 ya chakula. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na warembo kibao pamoja na staa wa mchezo wa kikapu Marekani, Kevin Durant.
Hata hivyo wakati wa sherehe hiyo ulitokea ugomvi kati ya warembo wawili waliopigana kwa sababu ya kila mmoja kuvutiwa na Trey Song kwa kila mmoja akimtambia mwenzake kwamba anampenda msanii huyo kuliko mwenzake.
Tazama video hapa.

VIDEO: Viatu vinavyotumia bluetooth kukuelekeza popote uendako



Taarifa hii ikufikie mtu wangu kama wewe utakuwa ni mpenzi wa kuvaa viatu, hii ni good news kwako, June 17 2016 nakusogezea moja kati ya viatu vinavyotumia bluetooth na venye uwezo wa kukuelekeza mahali uendapo na nimeona ni share na wewe mtu wangu, Viatu hivi  vyenye jina la ‘Sneakerairs‘  na vina  sensor ya umeme 
Teknolojia hii iliotengenezwa na kampuni ya Easy Jet ambapo unaambiwa kama ni mgeni wa sehemu uliofikia na hujui popote unatumia viatu hivyo kwa kuunganisha na simu yako kwa kuunganisha na kifaa hicho kwenye viatu vyako kwa bluetooth na vita kukupeleka popote utakapotaka kwenda kwa miguu yako mwenyewe bila kupotea.
Viatu hivi vimefanyiwa majaribio nchini Brazil kwa mara ya kwanza na vitaingizwa sokoni siku za mbeleni kwa ajili  ya watu kuvinunua na  kuvitumia kwa matumizi binafsi.
Tazama video hii kujua zaidi kuhusu viatu hivi….

Video: Diamond asema 90% ya bifu za wasanii wa bongo zinazozungumzwa sio bifu kweli


Mkali wa muziki na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amesema 90% ya bifu ambazo zinazungumzwa na waandishi wa habari na kukuzwa sio bifu za kweli.
Simba
Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni, Diamond amesema kuna bifu nyingi zinakuzwa na waandishi wa habari lakini kiundani unakuta sio bifu kweli.
“Mimi nikiangalia karibu 90% ya wasanii wa Tanzania ambao watu wanadhani wanamatatizo, sio kweli wanamatatizo,” alisema. Diamond. “Kuna baadhi ya vyombo vya habari vinatumia hiyo nyenzo ili kutengeneza maslahi binafsi, mimi nakwambia ukweli kabisa, kwa sababu watu wengi ambao wanasema wanamatatizo hawana matatizo, wangekuwa wana matatizo tungesikia mtu akisema mimi nikikutana na flani nitamtia ngumi ya meno,”
Aliongeza, “Ukitaka kuamini kama ni uongo, juzi tukilisikia kuna bifu kati ya Shilole na Vanessa lakini kesho yake wakafanya show, hamna ugomvi,”
Pia muimbaji huyo amevitaka vyombo vya habari kuandika habari ambazo zina tija kwa wasanii na taifa kwa ujumla.
“So kama tulivyowaomba mwanzo, tunaviomba vyombo vyetu, na tunawaomba sana sana mtutengenezee umoja kwa wasanii ili tuweze kusaidia familia zetu. Watu wanapogombana tunatia vita katika sanaa, familia, watu kulogana, tuwapumzishe nao waganga wanachoka, tunapeleka hela za bure,” alisema Diamond.

Thursday, 16 June 2016

Video: Chid Benz kaelezea maisha ya Sober House na mipango yake mipya.


Baada ya Chid Benz kutoka Sober House iliyopo Bagamoyo  kwa ajili ya kupata matibabu ya kuacha kutumia madawa kulevywa, June 16 2016 Chid benz ameeleza jinsi alivyokuwa anaishi katika nyumba ya Sober House na pia kaweka wazi mipango yake ya kurudi kwenye game ya bongofleva.
Mimi kule nilikuwa naishi kama staa kwasababu pia wale watu ambao nilikuwa naishi nao walikuwa wanajua mimi ni mtu ambaye walishawahi kuniona kwenye magazeti na TV kwa hiyo nilikuwa naishi vizuri hata hivyo Babu Tale aliwambia kuwa wanipe kipao mbele’ >>>Chid Benz
Kuhusu mimi nitakuwa kwenye lebel gani mimi namuachia Babu Tale kwasababu yeye ndio aliyeninyanyua upya na kunirudisha niwe kwenye muonekano huu yaani ni shine kwa mara nyingine, kwahiyo mimi na msikiliza yeye atakachoniambia‘>>>Chid Benz

Picha: Rihanna kuzindua perfume yake mpya mwezi Agosti




Msanii Rihanna ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika mitindo na viatu vyake vya ‘Puma clippers’ na ‘Trainer’ akiwa ameshirikiana na kampuni ya Puma alitangaza ujio wa perfume yake mpya aliyoipa jina la ‘Crush.’ Alitangaza kuwa June 14 kuwa itaingia sokoni mwezi Agosti mwaka huu.
riri2
riri
Rihanna kwa sasa ameamua zaidi kujikita kwenye mitindo ambapo amepanga kuzindua ‘Fenty Beauty by Rihanna’ mwakani, 2017.

Ibrah Da Hustler adai Jokate ndiye msichana anayempenda ‘She is so fly, she got nice lips



Rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Ibrah Da Hustler amesema staa wa kike anayetamani kuwa na uhusiano naye ni Jokate Mwegelo.
Jokate
Hustler amesema Jojo ana kila sifa anazozitaka kutoka kwa mwanamke. Na kiukweli amemmwagia sifa za kumwaga.
“Choice yangu mimi kama kudate na kastaa ka Bongo katakuwa kale kabinti kanachoitwa Jokate Mwegelo, she is fly meeen, I like her height, she got nice lips, she is so cute,” Ibrah alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Napenda smile yake, napenda style yake, napenda kila kitu chake, jinsi anavyoongea, anavyotembea, she is so high above the sea level, true say, no lie, mtoto mkali sana yaani,” aliongeza.
“Jokate Mwegelo you got me on my zone girl.”
Msikilize hapo chini.
Jokate ameupata ujumbe wa Ibrah na alikuwa na haya ya kusema:

TCRA: Kiama cha simu feki ni leo




‘Marehemu alikuwa mtiifu na alinipa michongo mingi enzi za uhai wake,’ watu wengi wanaomiliki simu feki watajikuta wakisema kauli hii Alhamis hii, June 16.
real-vs-fake
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA imesisitiza kuwa zoezi la uzimwaji simu feki unatekelezwa leo kama ilivyokuwa imepangwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, James Kilaba alisema kwa wale watakaofanya ujanja wa kubadilisha namba tambulishi (IMEA) watachezea kifungo cha miaka 10 jela au faini ya shilingi milioni 30 au vyote.
“Simu bandia zimepungua hadi chini ya asilimia 5! Hakuna kuongeza muda. Simu bandia ukomo wake pale pale 16 Juni,” TCRA wametilia mkazo kwenye Twitter.

Je! Chidi Benz naye kujiunga na lebo ya WCB?



Return of the King Kong. Baada ya kukosekana kwenye muziki kwa kipindi kirefu, msanii wa Hip Hop Bongo, Chidi Benz amerejea tena machoni mwa watu na muonekano mpya.
Chidi-Benz
Hivi karibuni kuliibuka tetesi kuwa rapper huyo ametoroka kwenye kituo cha LIFE AND HOPE REHABILITATION kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani alipokuwa akipata matibabu ya kupambana kujitoa kwenye uraibu wa madawa ya kulevya alipopelekwa kwa msaada wa Babu Tale na Kala Pina, lakini hilo lilionekana halikuwa na nguvu kutokana na hivi karibuni hali yake imeonekana kuimarika na kurejea kama awali.
Safari ya ‘sober house’ Bagamoyo
Babu Tale, Chidi Benz na Kalapina
Baada ya hali ya Chidi Benz kuonekana kuwa mbaya zaidi, March 21 mwaka huu Babu Tale
 na Kala Pina walichukuwa hatua ya kumpeleka kwenye kituo cha LHRC kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kupata tiba ya kujiondoa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya yaliyopelekea hali yake ya kiafya kuwa mbaya.
Kupitia akaunti ya Instagram ya Babu Tale aliandika: “Mwana amekubaLi kukaa Soba ila anasi
sitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii sa
fari ya matumaini.”
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Babu Tale alisema sababu yake iliyompelekea kumsaidia ChidI Benz kuwa alidhani msanii huyo kuwa ana ngoma [ukimwi].
“Kusema ukweli nilipoona picha ile nilipata wasiwasi nikidhani Chidi Benz labda ameungua na maradhi yetu ya sasa, sikuamini kama ni madawa ya kulevya ndiyo yamempelekea hali ile. Laki
ni sikuweza kuamini kesho yake ilibidi nimchukue Chid Benzi na kwenda nae kwenye kituo cha
afya na kufanya check up ya mwili mzima, lakini baada ya vipimo kutoka akaonekana yuko poa kabisa ila wakagundua tu ni hayo madawa.”
Baada ya siku 27 akiwa ndani ya kituo hicho, alipotembelewa na Kala Pina, Chidi alisema, “Sina mengi ya kuongea, niko sawa, nipo okay, niko fresh na msaada naupata.”
Tetesi za kutoroka sober house
Pina
May 25 zilisambaa tetesi za kutoroka kwa Chidi Benz kwenye kituo hicho alichopelekwa kwaajili
 ya kupata matibabu ya kupambana kujitoa kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.
Kwa kipindi hicho watu waliompeleka huko walishindwa kuongea chochote zaidi ya kusema
kuwa hakutoroka bali aliruhusiwa na uongozi wa kituo hicho kurudi nyumbani.
Tetesi za kujiunga na WCB
31
Chid Benz akiwa na Diamond kwenye studio ya WCB
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Chidi Benz amepost picha alizopiga kwenye studio ya WCB zinazomuonyesha akiwa na Diamond, Babu Tale na Harmonize hali inayozua shaka kuwa huenda King Kong akawa ameshamwaga wino wa kujiunga kwenye lebo hiyo ili kurudisha makali yake kama zamani.
12383209_646788105460940_1016128086_n
Chid Benz akiwa na Meneja wa WCB, Babu Tale
Aidha inadaiwa kuwa tayari Chidi ameshapika ngoma ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni japo bado haijajulikana iwapo wimbo huo umefanyika chini ya menejimenti ya WCB au laah.
11821164_1639903142954587_408394810_n
Chid Benz akiwa na Harmonize
Kila la kheri King Kong aka Chuma, naf

Tuesday, 14 June 2016

Picha: Professor Jay atembelea ‘WCB’ ya Diamond, afurahishwa na uwekezaji uliofanywa



Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi za WCB na kujionea uwekezaji uliofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platunmz.
Diamond akiwa na rais wa WCB, Diamond Platnumz
Rais wa WCB, Diamond Platnumz akiwa na Mbunge wa Mikumi, Professor Jay
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amemsifia Diamond kwa uwekezaji aliyoufanya.
“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu,” alisema Professor.
Aliongeza, “Kwa mfano pale kwa Daimond jana nimeenda nimekuta kuna studio hapo hapo, pamoja na kurecord lakini pia anachumba ambacho amekitengeneza cha kutengeneza photoshoot. Lakini pia ana sehemu ya kufanya editing ya kazi zake na ana watu special ambao amewaajiri kwa ajili ya kazi hizo, hii ni hatua kubwa sana kwa msanii,”
Babu Tale akiwa na Professor Jay
Babu Tale akiwa na Professor Jay
Jaymna Dojo
Professor Jay akiwa na Dogo Janja

Jay
Professor Jay na Raymond

PICHA & VIDEO: Kinavyohappen Wizkid na Chris Brown kwenye stage moja ya ‘One Hell Of A Night Tour’.



Wizkid ni kati ya wasanii  ambao wamevuka border na kuitambulisha vyema Africa. Siku kadhaa zilizopita Chris Brown alimtangaza Wizkid  kuwa kati ya wasanii atakaofanya nao perfomances kwenye tour yake ya ONE HELL OF A NIGHT TOUR. Mtu wangu wa nguvu nimezinasa picha na video za tour hiyo iliyofanyika nchi kadhaa za Ulaya.
Screen Shot 2016-06-13 at 10.32.04 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.18.23 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.18.00 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.34.16 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.34.00 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.28.26 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.27.50 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.27.21 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.27.07 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.26.45 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.26.12 AM
Screen Shot 2016-06-13 at 10.18.39 AM