HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Tuesday 14 June 2016

Picha: Professor Jay atembelea ‘WCB’ ya Diamond, afurahishwa na uwekezaji uliofanywa



Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi za WCB na kujionea uwekezaji uliofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platunmz.
Diamond akiwa na rais wa WCB, Diamond Platnumz
Rais wa WCB, Diamond Platnumz akiwa na Mbunge wa Mikumi, Professor Jay
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amemsifia Diamond kwa uwekezaji aliyoufanya.
“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu,” alisema Professor.
Aliongeza, “Kwa mfano pale kwa Daimond jana nimeenda nimekuta kuna studio hapo hapo, pamoja na kurecord lakini pia anachumba ambacho amekitengeneza cha kutengeneza photoshoot. Lakini pia ana sehemu ya kufanya editing ya kazi zake na ana watu special ambao amewaajiri kwa ajili ya kazi hizo, hii ni hatua kubwa sana kwa msanii,”
Babu Tale akiwa na Professor Jay
Babu Tale akiwa na Professor Jay
Jaymna Dojo
Professor Jay akiwa na Dogo Janja

Jay
Professor Jay na Raymond

No comments:

Post a Comment