Saturday 3 December 2016
Bombardier 3 mpya za Air Tanzania mbioni kutua nchini
Kampuni ya ndege ya Bombardier inatarajia kuzileta ndege tatu mpya kwaajili ya shirika la ndege la Tanzania, ATCL, imefahamika.
Ndege hizi mbili ni aina ya CS300 na moja ya Q400. Ndege hizo zina thamani ya dola milioni 203.
Mwishoni mwa Septemba mwaka huu, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli aliahidi kununuliwa kwa ndege zingine mbili kubwa kwaajili ya shirika la ndege la Tanzania, ATCL.
Alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa ndege mbili mpya za kwanza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Ndege hizo ni aina ya Bombadier Q 400 zilizotengenezwa nchini Canada.
Alisema ndege mbili kubwa zitakazonunulia hapo baadaye zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine kubwa zaidi itakayobeba abiria 240 pamoja na mizigo yao. Aliwahakikishia Watanzania kuwa fedha za kununua ndege hizo zipo.
Ndege za sasa zina uwezo wa kubeba abiria abiria 76, 6 wakiwa daraja la juu na 70 ni daraja la chini
Friday 2 December 2016
Picha,Mwanaume mwingine kachora tattoo ya jina la Shilole ubavuni….shishi
This Time ni huyu kujana ambaye mpaka sasa haijajulikana ni nani ila amejichora tattoo ya jina la Shilole kwenye ubavu wake.
Picha hii ilikuwa kwenye IG ya Shilole na ujumbe uliosema “Maswali stakiiiiii????”
PICHA : China wameanza kuitengeneza meli inayofanana na TITANIC
Meli ya Titanic iliyojengwa na
Harland na Wolff huko Belfast, iligonga mwamba wa barafu na kuzama
Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu
1,500 ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.
Leo ikiwa
ni takribani miaka mia na nne ‘104’ imepita tangu meli hiyo izame, China
wameamua kujenga meli inayofanana na Titanic, habari kuhusu meli hiyo
imewashangaza raia wengi wa China baada ya ujenzi huo wa meli hiyo yenye
urefu wa kina cha mita 269 kuanza.
Meli hiyo
ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic, itakuwa na sehemu
ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya watu maalum ambayo
itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika
eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
Source: Daily Mail, CNN
PART 1: Mfungwa mtanzania aongea kwa simu kutoka gerezani China, Bonyeza Play hapa Chini kusikiliza
PICHA : Magari yanayotumia umeme yanayotengenezwa China
Tunafahamu kuwa teknolojia inakuwa kila siku hasa katika nchi zilizoendelea ambapo China ni moja ya nchi hizo, Headlines zimetolewa na kituo kikubwa cha habari CNN kuripoti kutengenezwa kwa magari next level na kampuni ya NextEV ya China ambapo ni magari yanayotumia umeme na sio mafuta kama ilivyozoeleka.
Magari
hayo yanatumia battery ambazo zinachajiwa na umeme na kukaa na charge
ndani ya muda fulani na kutajwa kama magari yenye speed kubwa
yanayotumia umeme kuliko yote duniani na kutegemewa kuingia sokoni hivi
karibuni , nakusogezea picha za magari hayo hapa chini ujionee.
VIDEO: Idadi ya magari yanayotumia private number Arusha imetajwa, Bonyeza Play hapa chini kutazama
Monday 28 November 2016
New Video: Azma Mponda f/ Belle 9 – AstaraVaste
Video ya wimbo mpya wa rapper Azma Mponda aliomshirikisha Belle 9, AstaraVaste (I am in Love). Video imeongozwa na Kevin Bosco Jr
New Video: Dj Maphorisa x Wizkid – Good Love
Dj Maphorisa na Wizkid wameungana tena kwenye wimbo wa pamoja, Good Love. Umetayarishwa na Nana Rouges huku video ikiongozwa na Sesan Film Factory.
UFAFANUZI: Kuhusu kauli ya Waziri Ndalichako kwa wanaojiunga Vyuo Vikuu
Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea ya kuwa,
Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amezuia wanafunzi wenye Stashahada
(Diploma) kujiunga na masomo ya Shahada (Degree) katika vyuo vikuu.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella
Manyanya amesema kuwa, katazo lililotolewa na Waziri Prof. Ndalichako
siku ya mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania linawahusi wale tu
wanaosoma Foundation Courses ili kuweza kujipatia sifa za kujiunga na
chuo kikuu.
Taarifa
imeeleza kuwa awali wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne walikuwa
wakisoma Foundation Courses katika vyuo mbalimbali na kisha kujipatia
sifa za kujiunga na chuo kikuu kitu ambacho waziri alisema sasa
hakitakuwepo tena.
Utaratibu
huu ulikuwa ukitumika zaidi katika Chuo Kikuu Huria ambapo wanafunzi
walikuwa wakisoma programu maalum zilizokuwa zikiwapa sifa ya kusoma
Shahada.
“Kilichojitokeza
ni kuna taarifa zinasambaa kwamba kuanzia sasa wanafunzi watakaoenda
chuo kikuu ni wale ambao tu wamepitia form six sasa hiyo taarifa imeleta
presha kubwa, nimekuja hapa sio kukataa tamko hilo hapana nimekuja
kulitolea ufafanuzi.” – Naibu Waziri Eng. Stella Manyanya
VIDEO: Kilichowakuta Wezi waliokuwa wakifukua makaburi…
Kenya
ni moja ya nchi za Afrika Mashariki ambazo hazikosi matukio ya ajabu
kila mara. Hii imetokea kwenye mji wa Eldoret ambapo kuna watu wanne
walikamatwa wakifukua makaburi yaliyozikwa watu kuanzia wiki moja ili
kuchukua vitu vya thamani walivyozikwa navyo.
Inaelezwa
kuwa hiyo ni mbinu mpya ambayo imegunduliwa na wezi nchini Kenya
inapotokea mtu amefariki basi wezi huwa wanakwenda mpaka kwenye mazishi
na wanashiriki kama jamaa wa karibu ili tu kushuhudia marahemu
amevalishwa au kuwekewa nini kwenye jeneza lake na kisha hurudi baada ya
wiki moja kwaajili ya kubomoa na kuchukua vitu alivyozikwa navyo
marehemu.
Matukio ya
kuvunjwa makaburi yaliwashtua wakazi na ndugu wa karibu wa marehemu na
kuamua kuweka lindo ili kuona watu wanaoyavunja ambapo walifanikiwa
kuwakamata watu hao wakiwa wameshavunja kaburi moja na mmoja wapo akiwa
ndani ya kaburi kitendo kilichopelekea watu hao kuwapiga na kutaka
kuwafukia kwenye kaburi lililovunjwa.
Unaweza kutazama hapa chini kuona kilichotokea. Bonyeza Play
New Video: M-Rap f/ Mayunga – It’s Not Too Late
Akiwa chini ya uongozi mpya wa Mukii International, M-Rap ameachia kazi yake mpya iitwayo ‘It’s Not Too Late’ aliyomshirikisha Mayunga. Wimbo umetayarishwa na Bob Manecky wa AM Records huku video ikiongozwa na Msafiri wa Kwetu Studios.
Subscribe to:
Posts (Atom)