Meli ya Titanic iliyojengwa na
Harland na Wolff huko Belfast, iligonga mwamba wa barafu na kuzama
Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu
1,500 ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.
Leo ikiwa
ni takribani miaka mia na nne ‘104’ imepita tangu meli hiyo izame, China
wameamua kujenga meli inayofanana na Titanic, habari kuhusu meli hiyo
imewashangaza raia wengi wa China baada ya ujenzi huo wa meli hiyo yenye
urefu wa kina cha mita 269 kuanza.
Meli hiyo
ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic, itakuwa na sehemu
ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya watu maalum ambayo
itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika
eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
Source: Daily Mail, CNN
PART 1: Mfungwa mtanzania aongea kwa simu kutoka gerezani China, Bonyeza Play hapa Chini kusikiliza
No comments:
Post a Comment