Baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika na timu ya taifa ya Ureno inayoongozwa na nahodha wake Cristiano Ronaldo kutwaa taji hilo, headlines zimekuwa nyingi baada ya staa huyo kushinda Kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake.
Ronaldo baada ya kutwaa Euro 2016
aliripotiwa kutoa msaada bonansi yake yote aliyopewa, ila headlines za
staa huyo hazijaishia hapo, kwani ameamua kununua gari jipya ikiwa siku
chache zimepita toka afanikiwe kutwaa Kombe la Euro 2016, kitendo ambacho kinatafsirika kama kuamua kujizawadia zawadi hiyo.
Staa huyo wa Real Madrid amenunua gari aina ya Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport, gari ambalo lina thamani ya pound milioni 1.7 kiasi ambacho ni zaidi ya bilioni 4.9 za kitanzania, gari aina ya Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport aliyoinunua Ronaldo zinatajwa kuwa hadi sasa zimetengenezwa 450 tu, hiyo inatokana na thamani ya gari yenyewe.