Kuna fununu zilizosambaa kuwa tarehe 6 Septemba ndio uzinduzi rasmi
wa toleo jipya la Tecno Phantom huku ikitabiriwa kuwa ya kipekee kabisa
tofauti na matoleo mengine kutolewa. Uzinduzi huu umezusha uvumi mkubwa
miongoni mwa wale wapenzi simu. Kama inavyotarajiiwa, Tecno Phantom 6
itaweka rekodi katika soko la simu kimataifa.
Binafsi, bahati haikuwa yangu kupata fununu kamili mpaka
nilipodokezwa na baadhi ya vyanzo vya habari vya kuaminika kuwa Tecno
Phantom 6 imeboreshwa na itakuwa na nafasi kubwa ya kuhifadhi kumbukumbu
ikikadiriwa kuwa 6GB RAM na 32GB ROM.
Naweza nisiwe sahihi lakini pasi na shaka ninachotabiri ni kwamba
Tecno Phantom itakuwa imeboreshwa zaidi kwenye uwezo wake wa kuhifadhi
data yaani “Storage”. Ni adimu sana kupata simu yenye 6GB kama Tecno
Phantom itakuwa na uwezo huu, itakuwa ni gumzo.
INAAMAANA GANI SMARTPHONE KUWA NA RAM KUBWA
Kwa uzoefu wangu, kuwa na RAM kubwa inamaana simu ina uwezo mkubwa wa
kuchakata kulingana na matakwa ya mtumiaji, hii inamaanisha kwamba simu
yako (Endapo utaamua kununua Phantom 6 na ninakushauri uinunue)
haitokuwa inakwamakwama. Nafahamu matoleo kadhaa ya simu zenye uwezo
mkubwa wa kuchakata ambapo inaweza kuendesha hata Apps 30 tofauti kwa
mpigo bila kusuasua, lakini nikupe tahadhari kwamba matumizi yako ya
data yatakuwa ya kukwamakwama sana.
Wakati faida mojawapo ikiwa kuendesha App tofauti kwa mpigo, faida
nyingine ni kuwa ukubwa wa RAM ya Phantom 6 inaondoa tatizo la simu
kupata moto. Kwa ajili ya kawaida huu ni ujanja ambao watengenezaji wa
simu wametumia teknolojia na vifaa vinavyozuia simu kupata moto
kupitiliza. Hivyo, mtazamo wangu kuhusu Tecno Phantom 6 ni kwamba
inaweza ikawa sio tu yenye RAM ya 6GB pia prosesa ya hali ya juu.
Tunatumaini uzinduzi huu utamaliza mzozo na uvumi unaoendelea. endapo
unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno
kama ilivyoorodheshwa hapa chini.