Binafsi, bahati haikuwa yangu kupata fununu kamili mpaka nilipodokezwa na baadhi ya vyanzo vya habari vya kuaminika kuwa Tecno Phantom 6 imeboreshwa na itakuwa na nafasi kubwa ya kuhifadhi kumbukumbu ikikadiriwa kuwa 6GB RAM na 32GB ROM.
Naweza nisiwe sahihi lakini pasi na shaka ninachotabiri ni kwamba Tecno Phantom itakuwa imeboreshwa zaidi kwenye uwezo wake wa kuhifadhi data yaani “Storage”. Ni adimu sana kupata simu yenye 6GB kama Tecno Phantom itakuwa na uwezo huu, itakuwa ni gumzo.
Kwa uzoefu wangu, kuwa na RAM kubwa inamaana simu ina uwezo mkubwa wa kuchakata kulingana na matakwa ya mtumiaji, hii inamaanisha kwamba simu yako (Endapo utaamua kununua Phantom 6 na ninakushauri uinunue) haitokuwa inakwamakwama. Nafahamu matoleo kadhaa ya simu zenye uwezo mkubwa wa kuchakata ambapo inaweza kuendesha hata Apps 30 tofauti kwa mpigo bila kusuasua, lakini nikupe tahadhari kwamba matumizi yako ya data yatakuwa ya kukwamakwama sana.
Wakati faida mojawapo ikiwa kuendesha App tofauti kwa mpigo, faida nyingine ni kuwa ukubwa wa RAM ya Phantom 6 inaondoa tatizo la simu kupata moto. Kwa ajili ya kawaida huu ni ujanja ambao watengenezaji wa simu wametumia teknolojia na vifaa vinavyozuia simu kupata moto kupitiliza. Hivyo, mtazamo wangu kuhusu Tecno Phantom 6 ni kwamba inaweza ikawa sio tu yenye RAM ya 6GB pia prosesa ya hali ya juu.
Tunatumaini uzinduzi huu utamaliza mzozo na uvumi unaoendelea. endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa chini.
No comments:
Post a Comment