HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 2 September 2016

Video: Sultan King – Ngoma Inogile

Msanii Sultan King amechia video mpya ya wimbo unaitwa “Ngoma Inogile”, video imeongozwa na Kwetu Studio’s.

New Video: Dela na H_art The Band – Adabu

Kazi mpya ya msanii wa Kenya, Dela akiwa na Hart The Band ‘Adabu.’ Wimbo umetayarishwa na Cedo huku video ikiongozwa na Stanz Visuals

Video: Beka ibrozama – Mwanza

Msanii Beka ibrozama ameacha video mpya ya wimbo unaitwa “Mwanza”, Video imeongozwa na kampuni ya Fomular Picture.

Msanii wa Nigeria Kiss Daniel adai ameanza kumjua Harmonize kabla ya Diamond.

Msanii kutoka Nigeria ,Kiss Daniel ambaye hivi karibuni alikuja kufanya show
Tanzania amedai kuwa alianza kumsikia na kumjua Harmonize kabla ya Diamond.
Kiss alifunguka hayo kwenye mahojiano yake baada ya kuulizwa wasanii gani a
naowapenda
 ndani ya Bongo na kuwataja wawili hao na kudai kuwa alianza kusikia nyimbo za
 Harmonize kabla ya kusikia nyimbo za boss wa msanii huyo ambaye ni Diamond Platnumz. 
I love Harmonize,I love Diamond,basically Diamond and Harmonize i love them
 both,they are really doing good.Actually i heard Harmonize before I heard Diamond
,then i heard that Diamond is his boss” alifunguka Kiss Daniel

Mrembo anayedai kutishiwa bunduki na Chris Brown ana historia ya udokozi!


Mlimbwende wa kizungu anayemshutumu Chris kuwa alimtishia bunduki usoni, ana historia ya udokozi na anatafutwa kwa wizi kwenye hoteli ya The Plaza.
baylee-curran-chris-breezy
Baylee Curran, 25, alishtumiwa kumuibia rafiki yake, Rachel Getachew, 29, begi lake la Louis Vuitton likiwa na wallet ya Michael Kors ya $1,000 pamoja na fedha taslimu $200. Tukio hilo lilitokea mwaka 2013.
Jumanne, Curran alimshutumu Chris Brown kumtishia bunduki nyumbani kwake. Brown alikamatwa baada ya polisi kuizunguka nyumba yake kwa madai ya kutishia kwa silaha nzito.
Yupo nje kwa dhamana ya $250,000.

Diamond Platnumz ametaja biashara nyingine anayotaka kuifanya,Ifahamu hapa..



Msanii wa muziki wa bongo fleva,Diamond Platnumz ameweka wazi biashara nyingine ambayo ana mpango wa kuwekeza.
katika moja ya mahojiano yake,Diamond amesema ana mpango wa kufungua mtandao wake unaoitwa Afro Box ambapo watu wanaweza kungalia video exclusive kabla hazijatoka kwa gharama chache.
Kuna kitu kinaitwa Afro Box,kinahusisha maswala ya content za video,mbali na YouTube kutakuwa na platform nyingine kutoka Tanzania ambapo kabla video haijatoka watu wanapewa access ya kuiona kwa gharama chache,si unajua wengine wanapenda exclusive,pia tuko kwenye hatua za mwisho za kutengeneza headphones,maana nilishatangaza nitatoa headphone zangu” alifunguka Diamond

Video fupi Diamond akifanya video na Neyo Marekani

Diamond Platnumz yuko Marekani kwa ajili ya show yake September 2 Los Angeles lakini pia kufanya video ya kolabo na mwimbaji star wa Marekani Neyo ambayo waliirekodi audio yake Nairobi mwaka 2015.
Kipisi cha behind the scene kilichovuja wakati Diamond na Neyo wakiifanya hiyo video unaweza kukitazama kwenye hii video hapa chini…. Video: Diamond akutana na mchekeshaji wa US, Kevin Hart Diamond Platnumz ameianza vyema safari ya kutafuta tobo Marekani. Staa huyo ambaye yupo jijini Los Angeles, Marekani ambako tayari ameshoot video ya wimbo Marry You aliomshirikisha Ne-Yo, amekutana na mmoja wa mastaa maarufu sana Marekani. Amekutana na mchekeshaji na muigizaji wa filamu, Kevin Hart. Amepost kipande cha video Instagram akiwa na muigizaji huyo wa Central Intelligence anayesikika akiwasalimia followers wa Diamond.

Wednesday, 31 August 2016

video:Brownian wa maepo_ My Only _ Official video_ Directed by Mareys

Video:brownian 1-Nang'ang'ana

Music: Iyanya Ft. Victoria Kimani – Yoga

Here’s is another certified banger that just made its way online titled “Yoga” by one of Nigeria’s music sensation, Iyanya featuring Chocolate City’s music diva, Victoria Kimani.

The song was produced by DJ Coublon. Listen to Yoga by iyanya and kindly share your thoughts.

VideoMPYA: Rayvanny anakualika kuitazama video yake mpya ‘natafuta kiki’

Ni miongoni mwa waimbaji wa bongo wanaopewa sifa nyingi za utunzi na uimbaji kwenye bongofleva, lebo inayomsimamia ni WCB ya Diamond Platnumz, ukishamaliza kuitazama hii video usiache kutoa comment yako umeipokeaje ili akipita ajua Watu wake wamesemaje

VIDEO: Alichokiongea RC Makonda kuhusu September 1

August 30 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wananchi kuungana na Jeshi la Wananchi Tanzania katika maadhimisho ya miaka 52 ambayo yatafanyika September 1 2016.
Katika maadhimisho hayo Jeshi la Wananchi pamoja na wananchi wenyewe wataitumia siku hiyo kuchangia damu salama pamoja na kufanya usafi wa jiji.
Lakini RC Makonda amewataka wana Dar es salaam wote pamoja na watanzania kwa ujumla kuondoa hofu ya kuwepo kwa maandamano yanayoitwa ‘UKUTA’
Unaweza kuendelea kumsikiliza RC Makonda kwenye hii video hapa chini…

VideoFUPI: Diamond Platnumz anunua Rolls Royce ya $400,000 na zaidi?



Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines siku ya February
1 2016 ni hii ya msanii wa Bongofleva na CEO wa record label ya Wasafi Classic
 Baby (WCB) Diamond Platnumz kuweka
 wazi kuwa kabla ya mwaka 2016 kumalizika atanunua gari aina ya Rolls Royce.
 Kupitia account yake ya instagram usiku wa August 30 Diamond Platnumz  
 alipost clip video ya Rolls Royce yenye kivuli cha sura yake, inawezekana 
Diamond akawa ametimiza ahadi yake ya kumiliki gari hilo kabla ya mwaka 2016
kumalizika, kama Diamond atakuwa kanunua gari hilo atakuwa ni mtanzania wa pili
 anayefahamika kumiliki Rolls Royce baada ya makamu mwenyekiti wa zamani wa
Yanga Davies Mosha.
Baadhi ya mastaa Afrika wanaomiliki gari aina ya Rolls Royce ni Koffi Olomide na
 staa wa soka wa zamani wa Arsenal Emmanuel Adebayor ambaye kwa sasa anaichezea
 Crystal Palace, bado haijajulikana Rolls Royce aliyopost  Diamond ni toleo la mwaka gani
 ila stori kutoka autoguide.com inaeleza kuwa Rolls Royce inauzwa zaidi ya dola laki 3
ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600 pia inategemeana na toleo.

IMG_20160122_182043



Weka picha za utupu mtandaoni uende miaka 20 jela – TCRA









Untitled4


Unataka kwenda jela? Ni rahisi, weka picha za ngono mtandaoni, na utakuwa mkazi wa huko kwa kipindi cha miaka 20.

Kwa mara nyingine tena, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewakumbusha watanzania kutozichezea sharubu za sheria ya makosa ya mtandaoni, lasivyo wataishia pabaya.
“Ni vyema wananchi wakatambua kwamba uchochezi kwenye mitandao kwa kusambaza ujumbe wenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kuweka picha zisizofaa kwenye mitandao sheria ipo wazi na watu watajikuta wanaishia pabaya, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema,” alisema Mhandisi wa Mawasiliano wa Victoria Rulakara wakati akizungumza kwenye kipindi cha Hotmix cha EATV.
Wakati huo huo, mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ikiwa ni pamoja na kuwaonya watu wanaonzisha blog zenye majina ya uongo kutukana watu wengine.
Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ilipitishwa mwaka jana na rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

Breaking news: CHADEMA wasitisha maandamano ya UKUTA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesitisha maandamano ya UKUTA
 ambayo yalipangwa kufanyika Septemba 1 (kesho) baada ya kupokea maoni mbalimbali 
kutoka kwa viongozi wa dini.
ukuta.
Akiongea na waandishi wa habari muda huu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema chama kimeona kisitishe maandamano
 kwa muda ili kiwaachie viongozi wa dini watafute suluhu kuhusu suala hilo.
“CHADEMA tunaomba kuwatangazia watu wote kwamba tunahairisha mikutano ya kisiasa
 na maandamano yote kwa muda wa mwezi mmoja,” alisema Freeman Mbowe

Monday, 29 August 2016

Itazame hapa video mpya ya Chris Brown ‘Grass Ain’t Greener’ Enjoy.

Ata baada ya miezi kadha kupita baada ya kutoa wimbo wa  ‘Grass Ain’t Greener’ Chris Brown bado ameweza kutengeneza video ya wimbo huu, itazame hapa

Picha: Diamond ahama na kijiji Meru, Kenya

Diamond Platnumz ana miaka mingi ya kuvuna mapesa kutokana na show zake. Kutoka kwenye mapokezi yaliyovunja rekodi, Meru nchini Kenya hadi kuangusha show iliyohudhuriwa na makumi kwa maelfu ya mashabiki wenye kiu, staa huyo ameendelea kujiweka kwenye ligi yake mwenyewe.
13671777_319693035044213_233868961_n
Ilikuwa ni show ya mtu mmoja na kwa picha alizoweka kwenye page yake ya Instagram, inaonesha jamaa alihama na kijiji. Tazama picha hapo chini.

14156347_1775207089425751_1172340590_n
13671919_1282252215127601_1775648976_n
14027213_1095438053845281_641594979_n
14032811_1809578062607780_791686996_n

WCB Wasafi kufungua ofisi mpya Kijitonyama




Label ya WCB Wasafi ya Diamond Platnumz inafungua ofisi mpya Kijitonyama jijini Dar es salaam ambayo itakuwa inajihusisha na masuala ya kiuongozi zaidi.
13320130_708031909299557_1854325244_n
Akiongea katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Jumatatu hii, mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam, amesema wanafungua ofisi mpya ili kuipa nafasi ofisi ya zamani ya kufanya shughuli zake bila kuingiliana na shughuli zingine.
“Tunafungua ofisi nyingine ya WCB Kijitonyama,” alisema Sallam.“Hii itakuwa kwa ajili ya viongozi, halafu ile nyingine nitaendelea na kazi nyingine,”
WCB kwa sasa ni moja kati ya label za muziki ambazo zinafanya vizuri kutokana na wasanii wake wengi kufanya vizuri.