HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Saturday, 15 October 2016

Nyoka Hawa Wametoroka na Wamezua Hofu Kubwa Sana






Diamond ana mradi mpya na Usher Raymond

Spidi ya Diamond kulitafuta tobo la Marekani inatisha. Akiwa na collabo kibindoni na French Montana,
Yo Gotti na Ne-Yo ambaye watakuwa na ziara ya pamoja Uingereza Disemba mwaka huu, muimbaji
huyo wa ‘Salome’ ametoa hint ya mradi mwingine ujao na role model wake mwingine – Usher.
usher
Ametoa hint hiyo Ijumaa hii wakati akimpongeza muimbaji huyo wa ‘No Limit’ katika siku yake ya kuzaliwa.
“Happy Birthday Bro… Can’t wait for our Big day! @usher,” ameandika kwenye Instagram.
diamond
Kwa muda mrefu Diamond amekuwa akiwataja Ne-Yo na Usher kuwa ni watu anaowaangalia sana

Video: Chris Brown – Gravity (Fan Made)

Shabiki wa Chris Brown ametengeneza video yake ya wimbo ‘Gravity’ akitumia clips za video zake za mwanzo. Itazame hapo chini.

Thursday, 13 October 2016

Said Ally (aliyetobolewa macho) apewa pikipiki 5, Bajaji 2 na kuahidiwa nyumba

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha vitu alivyoviahidi kwa kijana Said Ally aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli jijini Dar es Salaam anavipata. Alhamis hii, ametimiza yote aliyoahidi na mengine.
14448203_1722673148053896_2851223501262553088_n
Said Ally akiwa na Diamond kwenye studio za Clouds FM
Katika ahadi zake, Makonda aliahidi kumchangia Said shilingi milioni 10 na leo hii amemkabidhi rasmi kiasi hicho. Pia amesema kupitia watu na taasisi mbalimbali, atapewa pikipiki tano na Bajaji mbili. Kama hiyo haitoshi, Makonda alisema kampuni ya GSM imeahidi kumnunulia nyumba kijana huyo .
“Nimeleta milioni 10 zangu siwezi kusahau lakini hili namuachia mwenyezi Mungu, naomba nikukabidhi, nashukuru na wale walioniunga mkono katika kumpatia Bodaboda 5 na Bajaj mbili ambazo zimetoka katika makampuni tofauti tofauti,” alisema Makonda.
“Jambo ambalo nilikuwa nikimlilia Mungu anipe nafasi ili niweze kulifanikisha – ni jambo ambalo lilikuwa likimsumbua kila mtu, ni jambo la Said kupata kiwanja na ukiangalia kwenye mji wetu huu kiwanja kinauzwa kwa bei ya juu sana, vinginevyo utaenda Magwepande na bado utakuwa nje ya mji,” aliongeza.
14624285_1287868034596841_5060916022513500160_n
Milioni 10 mezani: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijiandaa kumkumbatia Said Ally. Kushoto ni mama yake mzazi
“Shughuli za kibiashara zinafanyika katika ya mji, na hili jambo ulilisema ofisini kwangu na mimi nilikuwa nikimlilia Mungu anipe nafasi ya kufanikisha ndoto yako. Tumepata mdau ambaye amekubali na kumnunulia ndugu yetu Said nyumba, ambayo ni kampuni ya GSM na nimewambia wasikupeleke Magwepande, wasikupeleke Bunju, Mbagala, Gongo la Mboto. Nataka ukae mazingira yale yale ambayo umeyazoea. Iwe Tabata unakuja tena Buguruni, Mwenge. Nataka maeneo haya haya ambayo watu wamezoea kukuona. Kwahiyo ndugu zetu wa GSM wamekubali kuniunga mkono kumnunulia nyumba. Mi nakuombea neema ya bwana iendelee kutembea katika maisha yako,” alisisitiza Makonda.
Kwa upande wake, Said alishukuru na kusema, “Ukiona mtu anatoa chozi kwaajili ya mwananchi wake ni jambo zuri, alivyosikia kwenye vyombo vya habari hakuchelewa kuja. Lakini leo nashukuru sana kwa kila kitu alichonitendea, nashukuru sana.”
“Sina cha kumlipa zaidi ya kumuombea dua siku nyingine nisikie amekuwa waziri. Nashukuru sana namuombea kila siku na watu siwezi kuwasahau sana, Clouds ni watu ambao sitawasahau sana na Diamond sitamsahau sana,” alisema.
14705192_1588733588102424_2307701218224373760_n
Wakati huo huo wahenga wanasema ‘milima haikutani lakini binadamu hukutana.’ Hii likuwa kwa Said ambaye alipenda siku moja amuone mwanamuziki anayemkubali zaidi, Diamond Platnumz.
14705150_1861383707429526_3914097906952437760_n
Staa huyo anayemiliki label ya WCB, alitoa shilingi milioni mbili za kumkabidhi Said aliyezipokea kwa furaha.

Wednesday, 12 October 2016

Video: Masanja Mkandamizaji – Moyo Mweupe



Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi Masanja Mkandamizaji ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Gospel, ameachia video mpya ya wimbo ambao unaitwa “Moyo Mweupe”, video imeongozwa na Alex Josec

Video: Rick Ross – No U-Turns

Rick Ross turns into Renzel Washington as the star of his cinematic new visual for “No U-Turns.”
Donning a giant gold medallion around his neck, Rozay explains the importance of loyalty on “No U-Turns” and the Ryan Snider-directed clip brings his words to life.

Tuesday, 11 October 2016

Samsung yawaonya wateja ‘Zima na weka mbali Galaxy Note 7’



note7-fb
Samsung imetoa angalizo kwa wateja wake Jumatatu hii ikiwataka wazizime simu zao zao Galaxy Note 7 ambazo zimekuwa zikishika moto.




Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Samsung kusitisha utengenezaji wa simu hizo hatari kwa maisha ya watumiaji.
Kwenye maelezo yake rasmi, Samsung imesema itayaomba makampuni na mawakala wake dunini kote kuacha mauzo ya Galaxy Note 7, wakati inachunguza chanzo cha kushika moto.
Imewaomba pia wateja wenye simu za awali za Galaxy Note 7 au zile walizobadilishiwa, kuzizima na kuacha kuzitumia kabisa. Hatua hiyo imekuwa na matokeo hasi kibiashara kwa kampuni hiyo ya Korea Kusini. Hisa zake Jumanne hii zimeshuka kwa asilimia 5 mjini Seoul.
Mapema September, Samsung ilizirudisha kiwandani simu milioni 2.5 kutoka duniani kote na kuanza kutoa simu mpya kufidia, ambazo nazo zimegundulika kuwa na tatizo la kushika moto.
Jumatano iliyopita, moshi ulianza kutoka kwenye Galaxy Note 7 mpya kwenye ndege ya Southwest Airline kabla haijapaa na kulazimika kusitishwa kwa safari.

Kampuni ya kitanzania Simba Motors kuunda magari yake na kuyauza nchini

.




gari10


Kampuni ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu


Ahadi hiyo imetolewa leo mchana (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Jitesh Ladwa mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.
“Tumeamua kuunda magari aina ya pick-up kwa sababu ya mahitaji makubwa yaliyopo nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka Tanzania inanunua magari ya aina hii zaidi ya 4,000. Katika nchi za SADC mahitaji ni pick-up 35,000 kwa mwaka. Tutaanza na mtaji wa dola za Marekani milioni 200 na tumeomba ekari 200 katika eneo la EPZ,” alisema.
“Eneo la kiwanda cha kuunganisha magari peke yake linahitaji ekari 50, kwa hiyo tukiweka na yadi za kupaki magari, eneo la viwanda vingine, eneo la kushusha na kupakia makontena yatakayokuwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani, ni lazima tutahitaji eneo kubwa zaidi,” amesisitiza.
Amesema mradi huo wa majaribio, utaanza kwa kutengeneza magari 20 kila mwezi na kwamba kazi ya utengenezaji magari itaongezeka na kufikia 1,000 na baadaye 5,000 kwa mwaka.
Bw. Ladwa amesema uundaji wa magari hayo aina ya Foton-Tunland utafanyika kwa ubia baina ya kampuni yao, SUMA-JKT na kampuni Foton International ya China kwa kutumia teknolojia ya Kichina na kwamba magari hayo yanayotumia 4-Wheel Drive, yana uwezo wa kupita kwenye barabara za aina zote.
Kwa upande wake, akizungumza mara baada ya kulikagua gari la mfano aina ya Foton-Tunland, Waziri Mkuu amesema anawakaribisha kwenye uwekezaji huo hasa ikizingatiwa kuwa magari hayo yana uwezo wa kupita kwenye maeneo ya vijijini ambako barabara zake siyo nzuri.

Monday, 10 October 2016

Video: Chekedaa Ft Joto Dar es Salaam – Starehe

Wasanii Chekedaa na Joto Dar es Salaam ambao wanaunda kundi la The Family Team. Hii hapa ni video ya ngoma yao mpya ambayo inaitwa “Starehe”. Video imeongozwa na kampuni ya Kwetu Studio.

Video: Matonya – Sugua Benchi

Msanii Matonya ameachia video mpya ya wimbo “Sugua Benchi”, video imeongozwa na Mims. Angalia hapa

Video: Alikiba adai ana wasiwasi alifanyiwa ‘figisu figisu’ kwenye tamasha la Mombasa Rocks


14583290_1432447270118773_1063408828470525952_n

Hatimaye Alikiba ameeleza sababu ya kukatizwa kwa show yake kwenye tamasha la Mombasa Rocks ambalo Chris Brown pia alitumbuiza.


Kwenye tamasha hilo, Kiba alitumbuiza nyimbo mbili tu kabla ya mic aliyokuwa anaitumia kuonekana kupata mushkeli/kuzimwa na kumlazimu kuondoka jukwaani.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya, Willy Tuva akiwa bado Mombasa, Alikiba amedai kuhusi kufanyiwa hujum

NECTA yatoa ratiba ya ukaguzi wa vyeti mkoa kwa mkoa


p1-katuni_0
Hatua ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.


Katika taarifa yake ya sasa Baraza la Mitihani nchini, limetangaza kuwafuata katika maeneo yao ya kazi watumishi wote walioko katika mamlaka za mikoa, halmashauri na manispaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa vyeti vyao hivyo vya kitaaluma.
Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na Edga Kasuga kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwenda kwa Makatibu tawala wa Mikoa, uhakiki utafanyika katika ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 mwaka huu, ingawa ratiba nyingine ya uhakiki imeonyesha zoezi hilo litafikia tamati Novemba 7 mwaka huu.
“Ili kufanikisha zoezi hilo Baraza limetaka kupata orodha (nakala- laini ya soft copy) ya watumishi wote wa umma waliopo katika mkoa, halmashauri na manispaa.
“Nakala za vyeti vya kidato cha nne, cha sita na ualimu vya watumishi wote walioandikishwa na chumba cha kufanyia uhakiki,” inaeleza taarifa hiyo ya Baraza la Mitihani.
RATIBA YA UHAKIKI
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani, uhakiki huo utafanywa katika makundi matano katika mikoa tofauti tofauti.
Oktoba 10, mwaka huu kundi la kwanza litafanya uhakiki katika Mkoa wa Mtwara, kundi la pili Singida, kundi la tatu Rukwa, kundi la nne Katavi na kundi la tano litakuwa Geita.
Oktoba 17 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Lindi, la pili Manyara la tatu Songwe, la nne Kigoma na la tano litakuwa Mwanza.
Oktoba 24 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Morogoro, la pili Arusha, la tatu Mbeya, la nne Tabora na la tano Mara.
Oktoba 31 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Pwani, la pili Kilimanjaro, tatu Ruvuma, la nne Shinyanga na la tano Simiyu.
Novemba 7 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Dar es Salaam, la pili Tanga, la tatu Njombe, la nne Dodoma na la tano Iringa.
JOTO LA UHAKIKI
Kabla Baraza la Mitihani halijatangaza ratiba hiyo, tayari watumishi wa umma ambao wanatumia majina matatu lakini vyeti vyao vya elimu vinasomeka majina mawili walikuwa wamepewa maelekezo ya kwenda kutafuta hati ya kiapo kwa ajili ya kuapa mahakamani ili kuthibitisha majina yao.
Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mmoja wa watumishi hao alisema: “Wakati tunaanza kazi sisi ambao vyeti vyetu tulikuwa tunatumia majina mawili shuleni, tuliambiwa tutumie matatu ambayo pia yanatumika hata kwenye ‘salary slip’, sasa tumeambiwa tunatakiwa kwenda mahakamani kuthibitisha.”
Alisema zoezi hilo tayari limeleta changamoto kubwa mbali na kuzua hofu kwa baadhi ya watu ambao taarifa zao za kitaaluma hazipo sawa sawa.
“Mimi binafsi sina hofu zoezi linakwisha kesho lakini kinachoniuma ni kwamba hiyo hati ya kiapo (affidavit) tukienda Mahakama ya Mwanzo tunaambiwa ni lazima tulipie shilingi 10,000 na kibaya zaidi hatupewi risiti lakini kwa watumishi wengine ambao wanafahamiana wanapata huduma bure,” alisema mtumishi huyo.
Tangu Serikali itangaze kuwafuatilia watumishi wake wote wenye vyeti feki hali ya wasiwasi na sintofahamu imetawala miongoni mwa vigogo, maofisa na watumishi wengine ambao vyeti vyao vya kitaaluma haviko sawa sawa au haviendani na kazi au nyadhifa wanazoshikilia.
Source: Mtanzania

Sunday, 9 October 2016

VideoMPYA: Mchekeshaji Stan Bakora kairudia nisamehe ya Baraka the Prince

Mchekeshaji Stan Bakora ambaye ameshawahi kuzirudia ngoma za wakali kama Mrisho Mpoto leo anazichukua headlines baada ya kuirudia hitsingle ya Mkali mwingine  kutoka Bongoflevani Baraka the Prince mdundo wa Nisamehe aliomshirikisha Alikiba.
Pia mtu wangu usisahau kuniachia comment yako hapa chini na mkali huyu ataiona hapa.

Video: Chris Brown, Alikiba, Wizkid, Vanessa wanogesha tamasha la Mombasa Rocks

14448268_1797915360467373_2150686740120076288_n 

Wapenzi wa muziki mjini Mombasa, Kenya, Jumamosi hii walishuhudia moja ya matamasha makubwa zaidi kuwahi kufanyika. Tamasha la Mombasa Rocks, lilimdondosha msanii wa Marekani, Chris Brown kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki.

ALIKIBA - MAC MUGA LIVE PERFORMANCE IN MOMBASA 2016.

VIDEO: Vanessa Mdee alivyotumbuiza kwenye Mombasa Rocks Music Festival


Unakaribishwa kuona Vanessa Mdee alichokifanya kwenye stage ya Mombasa Rocks Music Festival Mombasa Kenya ambako Chris Brown, Wizkid, Alikiba na Navio walitumbuiza,

Tazama hii video hapa chini

ULIIKOSA HII YA BARABARA 3 KUFUNGWA KUTOKANA NA SHOW YA CHRIS BROWN BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA