HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Tuesday 11 October 2016

Kampuni ya kitanzania Simba Motors kuunda magari yake na kuyauza nchini

.




gari10


Kampuni ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu


Ahadi hiyo imetolewa leo mchana (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Jitesh Ladwa mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.
“Tumeamua kuunda magari aina ya pick-up kwa sababu ya mahitaji makubwa yaliyopo nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka Tanzania inanunua magari ya aina hii zaidi ya 4,000. Katika nchi za SADC mahitaji ni pick-up 35,000 kwa mwaka. Tutaanza na mtaji wa dola za Marekani milioni 200 na tumeomba ekari 200 katika eneo la EPZ,” alisema.
“Eneo la kiwanda cha kuunganisha magari peke yake linahitaji ekari 50, kwa hiyo tukiweka na yadi za kupaki magari, eneo la viwanda vingine, eneo la kushusha na kupakia makontena yatakayokuwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani, ni lazima tutahitaji eneo kubwa zaidi,” amesisitiza.
Amesema mradi huo wa majaribio, utaanza kwa kutengeneza magari 20 kila mwezi na kwamba kazi ya utengenezaji magari itaongezeka na kufikia 1,000 na baadaye 5,000 kwa mwaka.
Bw. Ladwa amesema uundaji wa magari hayo aina ya Foton-Tunland utafanyika kwa ubia baina ya kampuni yao, SUMA-JKT na kampuni Foton International ya China kwa kutumia teknolojia ya Kichina na kwamba magari hayo yanayotumia 4-Wheel Drive, yana uwezo wa kupita kwenye barabara za aina zote.
Kwa upande wake, akizungumza mara baada ya kulikagua gari la mfano aina ya Foton-Tunland, Waziri Mkuu amesema anawakaribisha kwenye uwekezaji huo hasa ikizingatiwa kuwa magari hayo yana uwezo wa kupita kwenye maeneo ya vijijini ambako barabara zake siyo nzuri.

No comments:

Post a Comment