HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday 21 October 2016

Prof Ndalichako aiagiza Bodi ya Mikopo kurudisha mfumo wa zamani wa utoaji mikopo


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kurejesha mfumo wa zamani wakutoa fedha kwa wanafunzi wa chuo.
necta
Akizungumza katika mahojiano maalum Alhamisi hii katika runinga ya TBC Taifa, Waziri Ndalichako alikiri kutokea mapungufu katika mchakato wa ugawaji wa mikopo.
“Kama waziri nimeshaiagiza Bodi ya Mikopo kwamba kwa sababu wanafunzi tayari wapo mashuleni, warudi katika utaratibu ule huwa wanawapa, kwa maana kwamba wanaangalia
uhitaji ili mtu ambaye anastahili kupata apatiwe fedha bila kufanya makosa kwenye chakula
 angalau kwa muhula wa kwanza. Halafu kama kutakuwa kuna haja yakufanya kulingana na
uwezo, vile vigezo viwekwe wazi na wanafunzi waelimishwe lakini lengo letu lipo pale pale
 kwamba wanafunzi wenye uhitaji watapatiwa mkopo,”
Waziri huyo alisema Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu imelazimika kubadili
 mfumo wa utoaji mikopo ili kukabiliana na mapungufu mbalimbali ambayo yamekuwa
 yakijitokeza. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kubwa kwa wanafunzi
wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu nchini baada ya wengi wao kukosa mikopo huku
wachache wakipewa kiasi kidogo ambacho kinadaiwa hakitoshele

AUDIO: Alichokizungumza Rais Magufuli kuhusu mikopo ya wanafunzi vyuo vikuu

Baada ya kuwepo kwa hatua mbalimbali za wanafunzi wa vyuo kudai ongezeko la fedha ya kujikimu na kupatiwa mkopo kwa wanafunzi ambao hawajapatiwa mikopo na baadae Wizara kuahidi kushughulikia suala hilo.
Leo October 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Rais Magufuli wakati akihutubia amegusia suala la mikopo ya wanafunzi ambapo amesema……..
>>>’Vyuo vyote vya elimu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua, ukishafungua kwa haraharaka wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawaambia kufanya usajili lazima walipe wakati bodi haijatoa orodha ya majina ya vijana watakaokopeshwa, lazima kuwepo na mawasiliano kati ya bodi ya mikopo, TCU, wizara ya Elimu na wizara ya fedha’
>>>’lengo la serikali si kuleta usumbufu kwa wanafunzi, lakini ni ukweli pia haitatoa mkopo kwa wanafunzi wenye uwezo, mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo?, mtoto wa katibu mkuu Kijazi naye apate mkopo? haiwezekani, mkopo huu umelenga kwa ajili ya kutoa watoto maskini lakini nasikia kule kuna upendeleo fulani katika kutoa mkopo sasa hili Waziri na bodi zinazohusike msimamie’;-JPM
Baada ya kuwepo kwa hatua mbalimbali za wanafunzi wa vyuo kudai ongezeko la fedha ya kujikimu na kupatiwa mkopo kwa wanafunzi ambao hawajapatiwa mikopo na baadae Wizara kuahidi kushughulikia suala hilo. Leo October 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Rais Magufuli wakati akihutubia amegusia suala la mikopo ya wanafunzi ambapo amesema…….. >>>’Vyuo vyote vya elimu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua, ukishafungua kwa haraharaka wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawaambia kufanya usajili lazima walipe wakati bodi haijatoa orodha ya majina ya vijana watakaokopeshwa, lazima kuwepo na mawasiliano kati ya bodi ya mikopo, TCU, wizara ya Elimu na wizara ya fedha’ >>>’lengo la serikali si kuleta usumbufu kwa wanafunzi, lakini ni ukweli pia haitatoa mkopo kwa wanafunzi wenye uwezo, mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo?, mtoto wa katibu mkuu Kijazi naye apate mkopo? haiwezekani, mkopo huu umelenga kwa ajili ya kutoa watoto maskini lakini nasikia kule kuna upendeleo fulani katika kutoa mkopo sasa hili Waziri na bodi zinazohusike msimamie’;-JPM ULIKOSA HAYA MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI KWA TCU KUHUSU ONGEZEKO LA VYUO VIKUU NCHINI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Diamond Platnumz ft Rayvanny Salome behind the Scene (part 4)

Diamond Platnumz - utata wa mavazi ya video ya salome (behind the scene)

Thursday 20 October 2016

Vanessa Mdee azungumzia sakata la Alikiba kuzimiwa mic na mapozi ya Chris Brown


VIDEO: Baadhi ya wanafunzi UDSM walivyofika wizarani kuwasilisha hoja zao kuhusu mikopo


Wakati magazeti ya leo yakitoka na habari iliyosema kuwa wanafunzi wa vyuo 66,000 kukosa mikopo, taarifa hizo zilidai kuwa wanafunzi 88,000 walioomba mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, wengi hawatapata.
Taarifa hizo zilizochapishwa na gazeti la mwananchi la October 20 2016 zimesema kuwa uwezo wa bodi hiyo ni kutoa mikopo kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia 24 na waliopatiwa hadi sasa ni wanafunzi 11,000 sawa na asilimia 12.
Wakati hayo yakielezwa leo October 20 2016 baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wakiongozwa na viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho ‘DARUSO’ wamefika Wizara ya elimu wakiwa na hoja kuu mbili, uchache wa majina ya wanuafaika wa mikopo yaliyotoka  mpaka hivi sasa na hoja ya pili ni kuhusu vigezo ambavyo vimetumika kwenye fedha ya kujikimu kwa wanafunzi.
Hata hivyo baada ya kufika wizarani hapo wanafunzi hao wamesema hawakupata nafasi ya kumuona waziri wa elimu lakini wamefikisha hoja zao kwa katibu mkuu wa wizara na ametoa ahadi ya kushughulikia hoja hizo.

Virgin America 'First Class' shoes include seat buckle, WiFi, TV

 

With about 15 percent more style points than Steph Curry's infamous hospital shoes and all the swag of an earthbound astronaut, a new, on-of-a-kind shoe debuted this week called the Virgin America First Class Shoe

 The agency only created one pair, and the latest bid, as of this writing, stands at $4,950 on eBay, with just a little less than eight days left

No, these probably don't represent the high-end style most imagine when thinking of riding in first class, but as an incredibly rare mix of fashion and tech, it's hard not to consider a bid.

 

Picha: Rose Ndauka azindua label ya muziki na kutambulisha msanii mpya

img_2187

Muigizaji na Mkurugenzi wa kampuni ya Ndauka Advert Limited, Rose Ndauka Alhamisi hii ameitambulisha rasmi label yake itakayowasimamia wasanii wa Bongo Fleva ‘Ndauka Music’ pamoja na kumtambulisha msanii wake mpya, Kassim Casso aka Casso mbele ya waandishi wa habari.
img_9995
Rose Ndauka akiwa na Casso wakionyesha CD ya wimbo wake mpya kwa waandishi wa habari
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Ndauka amesema kuwa ni muda mrefu amekuwa akitamani kusaidia vijana wenye vipaji.
“Kwa muda mrefu nilikuwa natamani kuwasaidia vijana wenye vipaji, takribani mwaka mmoja au miwili iliyopita tulianza kuifanya kazi hiyo mimi pamoja na menejimenti nzima ya Ndauka Advert. Kwahiyo leo tunaannounce lebo ya Ndauka Music pamoja na kumtangaza msanii wetu wa kwanza anaitwa Casso pamoja na kutambulisha wimbo wake mpya ‘Kitonga’. Kuna mengi yanakuja kupitia Ndauka Music chini ya Ndauka Adverts,” amesema Ndauka.
Mkurugenzi huyo alieleza pia sababu ya kuingia kwenye muziki na si kuibua vipaji vya wasanii wa filamu huku soko lake likionekana kutofanya vizuri.
“Mimi kama muigizaji naamini sanaa inagusa sehemu kubwa, nikiongelea Ndauka Adverts chini yake kuna Ndauka’s Family ambapo kuna wasanii 15 wakiwemo wanamuziki na waigizaji. Mei 31, mwaka huu tulibahatika kutoa filamu ambayo inaitwa ‘Angela’ na staa aliyekuwepo ndani ya filamu hiyo alikuwepo Bi Hindu peke yake lakini waliobakia walikuwa ni underground waliokuwa chini ya Ndauka’s Family,” alifafanua Ndauka.
Kwa upande wake msanii huyo mpya wa Ndauka Music, [Casso] ameishukuru lebo yake hiyo kwa kumsaini pamoja na kuwaahidi mashabiki kuachia kazi nzuri.
Naye Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Aneth Mosha ameitaja sababu ya msanii huyo kuwa wa kwanza kutangazwa kwenye lebo yao hiyo ni kutokana na nidhamu aliyokuwa nayo, jitihada zake pamoja na kujituma.
img_2196
Casso akiongea na waandishi wa habari
img_2189
img_2187

Wizara ya Elimu: Mikopo tumetoa kwa vigezo. Wanafunzi wengine hutumia mikopo kununulia Tv na pombe

Wizara ya elimu imefafanua kuwa wametoa mikopo kulingana na vigezo vya wanafunzi na pia sio wote wenye vigezo watapata kwa kuwa bajeti ina ukomo.

Naibu waziri amesema wanafunzi wengi walikuwa wanapata mikopo pasipo na vigezo na walikuwa wakitumia mikopo kufanyia mambo mengine kama kunywa pombe kununulia tv na kutembea ambavyo sio kusudio la mikopo hiyo.

Sunday 16 October 2016

Maneno ya Diamond kwa Harmonize baada ya kushinda tuzo ya AFRIMMA


Tuzo za AFRIMMA ambazo hutolewa kila mwaka kwa Waafrika mbalimbali waliofanya 
vizuri kwenye sekta mbalimbali hasa za burudani, zimetolewa Dallas Texas Marekani 
leo ambapo kwenye list yote Watanzania walioshinda ni watatu.
Watanzania walioshinda ni Dj D Ommy wa CloudsFM kupitia show mbalimbali
ikiwemoXXL na AMPLIFAYA ambapo ameshinda tuzo ya Dj bora Afrika,
mwimbaji Harmonize akishinda tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 
2016 huku Diamond Platnumzakishinda ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.
Sasa miongoni waliotoa pongezi kwa Harmonize ni Diamond Platnumza ambae kupitia i
nstagram alipost picha na kuyaandika haya>>>>hii picha inanikumbusha mwaka jana
 ulipokuja nipokea airport kutokea@afrimma …ukaniuliza “hivi ipo siku nami 
nitachaguliwa tunzo yoyote ya kimataifa”….nikakwambia “Ukifanya kazi kwa bidii’
‘Ukimuheshimu kila mtu, ukamuamini na kumuomba Mwenyez Mungu basi 
Mollah atakufungulia ndoto zako….na leo hii kweli Tunafurahia Ushaindi wako
 wa Msanii Bora Chipkizi Africa….. Hongera sana @harmonize_tzna shukra sana sana
Mashabiki zetu pendwa kwa kura na @Afrimmakwa kuendelea
                      kuvinyanyua vipajia vyaAfrica

 🙏

Diamond, Harmonize na DJ D-Ommy washinda tuzo za Afrimma 2016


Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy, wameibuka washindi kwenye
 tuzo za  Afrimma 2016, zilizofanyika Dallas, nchini Marekani Jumamosi hii.
afrimma
Diamond ameibuka tuzo ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, Harmonize
Msanii bora chipukizi na D- Ommy, DJ bora wa Afrika.“Team Tanzania Mungu
ni mwema siku zote,” ameandika Harmonize baada ya ushindi huo.
14723585_204730183290000_6229108837392056320_n
Harmonize akiwa na Akothee aliyeshinda tuzo ya msanii bora wa kike Afrika
 Mashariki na  Willy M Tuva Diamond na D-Ommy hawakuwepo kwenye tuzo hizo.

Mbwana Samatta atajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika


Mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya K.R.C. Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, ametajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF. 13256965_514911378696194_1578856451_n
Majina hayo 30 yametangazwa Jumamosi hii kupitia tovuti ya shirikisho hilo la soka barani.
caf-1
caf-2
caf-3