HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday 21 October 2016

Prof Ndalichako aiagiza Bodi ya Mikopo kurudisha mfumo wa zamani wa utoaji mikopo


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kurejesha mfumo wa zamani wakutoa fedha kwa wanafunzi wa chuo.
necta
Akizungumza katika mahojiano maalum Alhamisi hii katika runinga ya TBC Taifa, Waziri Ndalichako alikiri kutokea mapungufu katika mchakato wa ugawaji wa mikopo.
“Kama waziri nimeshaiagiza Bodi ya Mikopo kwamba kwa sababu wanafunzi tayari wapo mashuleni, warudi katika utaratibu ule huwa wanawapa, kwa maana kwamba wanaangalia
uhitaji ili mtu ambaye anastahili kupata apatiwe fedha bila kufanya makosa kwenye chakula
 angalau kwa muhula wa kwanza. Halafu kama kutakuwa kuna haja yakufanya kulingana na
uwezo, vile vigezo viwekwe wazi na wanafunzi waelimishwe lakini lengo letu lipo pale pale
 kwamba wanafunzi wenye uhitaji watapatiwa mkopo,”
Waziri huyo alisema Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu imelazimika kubadili
 mfumo wa utoaji mikopo ili kukabiliana na mapungufu mbalimbali ambayo yamekuwa
 yakijitokeza. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kubwa kwa wanafunzi
wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu nchini baada ya wengi wao kukosa mikopo huku
wachache wakipewa kiasi kidogo ambacho kinadaiwa hakitoshele

No comments:

Post a Comment