HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Saturday 8 October 2016

Video: Mariah Carey & Jussie Smollett – Infamous


1f8f4f8d32b18a1e05ba7172aa53871d-696x392 Msanii mkwongwe wa R&B, Mariah Carey ameonekana kwenye episode mpya ya tamthilia maarufu ya Empire. Mariah katika tamthilia ya Empire anatumia jina la ‘Kitty’ aliungana na Jussie Smollett au Jamal Lyon kuimba wimbo wa pamoja ambao unaitwa “Infamous” uliandaliwa na Jermaine Dupri.
Tangu kuanza kwa msimu mpya wa tamthilia hiyo tayari kumekuwa na appearance za mastaa wakubwa wakiwemo Birdma, French Montana, Xzibit na Romeo Miller.

Video: Snura – Chura

chura
Msanii Snura hatimaye ameachia video yake mpya ya wimbo wa “Chura”, baada ya kufunguliwa kwa wimbo huo. Angalia hapa alafu toa koment yako.

Mwanafunzi aliyepigwa na walimu Mbeya afunguka A – z.

mwanafunzi

Mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyekuwa akisoma Mbeya Day, Sebastian Chinguku ameelezea jinsi alivyoshambuliwa kwa kupigwa na walimu zaidi ya mmoja
Anadai mkasa mzima ulianza baada ya kupewa kazi na mwalimu wake lakini kutokana na kuwa mgonjwa alishindwa kuifanya mapema. “Wakati Jumatano nawasili naenda shule, mwalimu yeye ndio alikuwa anadai hiyo kazi siku hiyo, baada ya yeye kudai hiyo kazi, mwalimu akasema ‘ambao hawajafanya hiyo kazi wapite hapa mbele’ mimi ni kawa ni mmoja wapo, nikapita mbele. Nikamuelezea mwalimu jinsi ilivyokuwa, nikamwambia mwalimu ‘nilikuwa naumwa na ndio maana sikuweza kufanya kazi yako.’ Mwalimu hakunisikiliza akasema sisikilizi maelezo ya mtu yeyote, basi nikaona tu haina haja nikakubali kuadhibiwa na wenzangu,” alisimulia. “Huyo mwalimu Frank Msigwa akawa amenichapa fimbo tatu round ya kwanza wote, kabla ya kuanza kutuchapa aliwaita walimu wenzake waje kumsaidia kutuadhibu. Wale walimu walipofika walikuwa wanne kwa wakati mimi nilipoadhibiwa fimbo tatu za mara ya kwanza, wakati wenzangu wanarudiwa kupigwa fimbo kwa mara ya pili, kuna mwalimu tu mwingine kwa jina simfahamu akawa ameniita nyuma ya darasa maanake walimu wote wakati wote wakati huo tulikuwa mbele lakini mwalimu huyo aliniita nyuma ya darasa. Basi nilivyoenda pale kumsikiliza,akaniambia ‘unanikumbuka?’ Nikamwambia ‘hapana’ kama unakumbuka kipindi kile sisi tunafanya mitihani waliniambia kwamba nivue sweta nikagoma, nikawaambia ‘hapana sikugoma’ nikamwambia ‘mbona nilikuelezea kwamba nilikuwa naumwa kifua ndio maana nikashindwa kuvua sweta!’ “Basi akatokea huyo mwalimu Msigwa akadakia ‘mi mhuni mhuni’ akawa anatoa hizo kauli akasema kwamba nipige magoti. Sasa na mimi nikataka kujua nikamuuliza ‘mwalimu kwani nina kosa gani kama nikutokufanya kazi yako si ndo hii ambayo umetuadhibu kwa pamoja?’ Basi mwalimu hakutaka kunielewa. Akasema ‘kwahiyo unabisha?’ nikamwambia ‘hapana mwalimu nilichotaka kujua kosa langu ni kosa gani basi.’ “Mwalimu akaanza kunirushia ngumi za kwenye bega wanafunzi wakawa wamemshika mwalimu na walimu wale watatu walikuwa wamenishika mimi. Baada ya kunishika hapo wale wanafunzi wenzangu wakawa wamemuachia yule mwalimu, mimi wale walimu wakawa hawajaniachia wakaanza kuniburuza toka darasani mpaka staff room ofisi ya walimu. Tulivyofika staff wakanifungia mlango na kuanza kunipiga kama inavyoonekana kwenye clip. Walivyonipiga kuna mwalimu aliyekuwa anashuti ile video akawa ananiombea msamaha ‘msameheni’ lakini walimu wale hawakusikia. Baada ya yule mwalimu kuniombea sana wakaona waniadhibu tu fimbo kama fimbo wakati huo nimeshapigwa kama kwenye ile clip inavyoonekana. Wakaniadhibu tena fimbo saba baada ya kupigwa hapo tena,” aliendelea kueleza. “Wakaniambia wanitoe staff wanipeleke tena darasani wakaniadhibu tena mbele ya wanafunzi kwa mara nyingine tena. Sasa wakati tunatoka kwanza mimi nikamwambia ‘mwalimu mbona mmenichapa sana na kila sehemu ya mwili wangu sasa hivi inauma, naomba basi mnipe adhabu nyingine.’ Wale walimu hawakunielewa wakawa wamenibeba wamenishika wanataka kunipeleka darasani, sasa wakati tunatembea tunakaribia kufika darasani na mimi nikaona nijitetee nikakimbia. Wakati nakimbia mwalimu akawa amenishika mkono alivyonishika mkono akanirudisha tena darasani. Nilivyopelekwa darasani wakaniambia nikae chini. Nikawa nimekaa chini, walimu wakawa wanaongea tena na wanafunzi. Sikukaa dakika chache tu mwalimu yule akanirudia tena mbele ya wanafunzi akanipiga teke sehemu ya jicho. Jicho likawa limevimba na kukawa na mchubuko unatoa damu na nikawa natoka damu puani na mdomoni pia.” Tayari Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ametangaza kufukuzwa chuo walimu hao waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika shule hiyo. Pia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, HELSB, imetoa taarifa ya kusitisha mikopo kwa walimu hao.

Diamond: Ne-Yo, Wizkid, Tekno, Flavour wameipa saluti ‘Salome’


daimond-x-rayvanny

Hit maker wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amemtaja Ne-Yo, WizKid, Tekno pamoja na Flavour kuwa ni miongoni mwa mastaa walioukubali wimbo wake mpya ‘Salome’.

Muimbaji huyo amedai kila mmoja kwa wakati wake alivyoona video ya wimbo huo, alionesha kupendezwa na kile alichokifanya.
“Kabla ya wimbo kutoka Wizkid alikuwa Tanzania wakati nipo naye nilimpa ule wimbo aisee ulimvuruga sana, “Diamond alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.
“Hata baada ya wimbo kutoka wasanii wakubwa kama akina Tekno, Flavour walinitumia ujumbe mfupi kuonyesha kupenda, nakumbuka hata Ne-Yo naye aliniambia ‘I like the song Pia muimbaji huyo alisema amepokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali akiwemo Rais mstaafu Jakaya Kikwete. Video ya wimbo huo hadi sasa ina views milioni 4.3 kwenye mtandao wa Youtube.

Video: Bruno Mars – 24K Magic

Msanii Bruno Mars baada ya ukimya wa muda mrefu bila kutoa wimbo, ameachia video mpya ya wimbo unaitwa “24K Magic”

VIDEO: Chris Brown alivyowasili hotelini baada ya kutua Mombasa……

cuphnqewgaaruso

breezy


Mwimbaji staa kutoka Marekani Chris Brown amewasili Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kutumbuiza leo October 8, 2016 kwenye tamasha lililopewa jina la Mombasa Rocks Festival ambapo jukwaani atasindikizwa na wakali akiwemo Alikiba, Vanessa Mdee, Navio, na wengineo.
Itazame hii video hapa ujionee jinsi alivyowasili Hotelini baada ya kutua Mombasa nchini Kenya

Friday 7 October 2016

Top 10 Richest Countries in the World 2016

Top 10 Richest Persons of the World 2016

BILL GATES CAR

Vanessa Mdee aipiga chini show ya Chris Brown Mombasa



14448268_1797915360467373_2150686740120076288_n


Ndoto ya Vanessa Mdee kutumbuiza kwenye jukwaa moja na msanii wa Marekani, Chris Brown kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Jumamosi hii imepeperuka.


Hitmaker huyo wa ‘Niroge’ ameweka wazi kupitia mtandao wake wa Instagram sababu ya kutotumbuiza kwenye tamasha hilo ni kutofikia makubaliano na waandaaji wa tamasha hilo.
14478527_1592720981023421_8041592067165519872_n
Kwa sasa macho ya Vanessa yatakuwa ni kwenye tamasha la One Africa Music litakalofanyika jijini Houston, Texas, Marekani, October 22 ambapo anatarajiwa kupanda kwenye jukwaa moja na wasanii wengine kama 2 Face, Flavour, P –Square, D’Banj, Kcee, Mafikizolo, Fally Ipupa na Cabo Snoop.


Rais Magufuli ampongeza Bakhresa


Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza Said Salum Bakhresa kwa kuwa mzalendo na kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi kupitia biashara zake.
ay4
Alisema hayo katika kijiji cha Mwandege wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani wakati akizindua kiwanda cha kusindika matunda kilichopo chini ya Kampuni ya Food Products mali ya kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) ya Dar es Salaam.
magufulibakressa
“Leo hapa kwenye kiwanda hiki cha kusindika matunda pekee, kimetoa ajira kwa Watanzania takribani 800, bado viwanda na kampuni zake nyingine zinazozalisha bidhaa kama vile maji na juisi ambazo zimetoa ajira kwa Watanzania wengi nchi nzima. Huu ndio uwekezaji ambao awamu ya tano tunauhitaji,” alisema.
Rais Magufuli pia alimpongeza Bakhresa kwa kuwa Mtanzania na mzalendo wa kwanza kuanzisha viwanda mbalimbali, ambavyo pamoja na kuchangia katika pato la taifa kwa kulipa kodi, lakini pia vinatengeneza ajira kwa watu wengi.

Said Ally, aliyetobolewa macho Buguruni Sheli hatoweza kuona tena



14474203_1683307165319633_2232738297854033920_n



Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana
 Said Ally aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena.
 
Makonda akimliwaza Said Ally baada ya madaktari kusema kuwa hakuna namna ya 
kumfanya awe kuona tena
Makonda ametoa majibu hayo ofisini kwake Ijumaa hii.
“Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote,” alisema Makonda.
“Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake,” alisema.
Pia Makonda amesema serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni kumi kama sehemu ya mtaji wake. “Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja,” aliongeza.
Kupitia Instagram pia, Makonda ameandika: Watanzania wengi tulitamani Said uone tena ila tumeshindwa, tuna mwachia Mungu.
Tayari mtu aliyemfanyia Ukatili huo yupo mahabusu.

New Video: Victoria Kimani – My Money


Malkia wa Chocolate City, Victoria Kimani ameachia video ya wimbo wake wa pili kutoka kwenye album ijayo, Safari. Unaitwa My Money na video imeongozwa na Mazi Cijizzle.

Thursday 6 October 2016

Video: Chris Roby – Pana Cover Swahili

Msanii Chris Roby ameafanya Cover ya Kiswahili ya wimbo wa “Pana”, wa msanii Tekno kutoka Nigeria, ameachia Video ya wimbo huo angalia hapa chini alafu toa koment yako. Video imeongozwa na Steve Man Rizo.

Video: Kid Ink – Die In It

Kid Ink transforms into a wolf in his new video for “Die in It,” which arrives just in time for Halloween.

New Video: Linah – Raha Jipe Mwenyewe


Malkia wa muziki Linah Sanga ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Raha Jipe Mwenyewe’. Ndani ya video hiyo mchekeshaji Idris Sultan amecheza vitendo. Audio imeandaliwa na producer Mr T Touch na video imeandaliwa na director, Khalfani Khalmand

VideoMPYA: DJ Khaled ametuletea hii Video yake mpya – Do You Mind


Baada ya kuhost show ya utoaji wa tuzo za BET Hip Hop 2016 zilizorushwa usiku wa kuamkia October 5, 2016 na kuibuka na tuzo tatu ikiwemo ya DJ of The Year, MVP of The Year na Hustler of The Year, DJ Khaled hatimaye ameachia mzigo huu unaopatikana kwenye albam yake mpya ya Major Key “Do You Mind” akiwa na mastar wengine kama Nicki Minaj, Chris Brown, August Alsina, Jeremih, Future & Rick Ross. Don’t play yourself

VideoMPYA: Shilole anatukaribisha kuitazama hii video yake mpya

Ni October 5, 2016 ambapo Shilole anaziandika headlines kwenye Bongo Fleva kwa kuachia video mpya ya  single iitwayo Mtoto mdogo aliyomshirikisha mkali wa nyimbo za Singeli maarufu kama Man Fongo. imetayarishwa na directo

Monday 3 October 2016

VideoMPYA : Baraka Da Prince na Alikiba wametuletea video yao mpya


Ni Single mpya iitwayo Nisamehe ambayo ilirekodiwa April 27, 2016 kwenye studio za producer Emma The Boy  na wakali kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 Baraka Da Prince na Alikiba
Sasa leo kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa Alikiba aliwasuprise mashabiki wao baada ya kuachia video mpya ya single hiyo iitwayo Nisamehe.
kibasss
Ukishamaliza kuitazama hii video sio mbaya ukituachia na comment yako wakali hawa watapita hapa kujua Watanzania wameipokeaje.

New Video: Davido – Gbagbe Oshi

Davido ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Gbagbe Oshi’ ambao utapatikana kwenye albamu yake ya ‘Son of Mercy’ iliyoanza kupatikana kama Ijumaa iliyopita. Tazama hapa chini video hiyo.

Alikiba na Vanessa Mdee kutumbuiza na Chris Brown Mombasa

.
vanessa
Alikiba na Vanessa Mdee watapanda jukwaa moja na nyota wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown
Wawili hao watatumbuiza pamoja na Chris Brown, Oktoba 8, mwaka huu kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music.
“Mombasaaaaaa it’s ME N U this weekend. @mombasarocksfestival 👌💜🎤👑 #Juu #Niroge,” ameandika Vanessa kwenye Instagram.
Nyota wa Nigeria, Wizkid naye atatumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa.

Sunday 2 October 2016

Simba na Yanga zapigwa marufuku na serikali kuutumia uwanja wa Taifa


mabomu-ya-machozi


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ametembelea Uwanja taifa Jumapili hii na kuzipiga marufuku mechi zote za Yanga na Simba kufanyikia uwanjani hapo kutokana na uharibifu wa mageti na viti uliojitokeza siku ya jana katika mechi hiyo ya watani hao wa jadi.


Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi hapo jana baada ya kufanya uharibufu wa viti
Pia Nape amezuia mapato ya timu hizo ya mchezo wa jana kutokana na uharibifu huo.
“Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu,” alisema Nape. alisema Nape.
Amri hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung’oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Tazama kionjo cha video ya ‘Nisamehe’ ya Barakah The Prince na Alikiba

  14359964_1289890031044389_8005694855059603456_n

Video ya wimbo wa Barakah The Prince aliomshirikisha Alikiba, Nisamehe itaanza kuoneshwa kwa mara ya kwanza, Jumanne, Oktoba 4 kupitia MTV Base. Video hiyo ilifanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Meji Alabi. Chini ni kionjo chake.

Video: Bondia afariki dunia baada ya kupokea kichapo ulingoni

 towell-mike

Bondia Mike Towell (25) amefariki dunia baada ya kupoteza pambano lake na Dale Evans kwenye mzunguko wa tano. Pambano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa St Andrews Sporting Club Alhamisi iliyopita. Baada ya kupoteza pambano hilo hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ambako baadaye alifariki dunia. Ripoti ya madaktari imeonesha kifo cha Mike kimesababishwa na kuvujiwa na damu nyingi kwenye ubongo baada ya fuvu lake kupata madhara. Kabla ya kupoteza pambano hilo bondia huyo aliangushwa mara mbili kwenye mzunguko wa kwanza kabla ya kuangushwa tena kwa konde zito na kushindwa kuendelea na pambano.

Video: Diamond abaki na nguo ya ndani ‘boxer’ wakati akisherekea birthday yake


diamond

Jumamosi hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya staa wa muziki, Diamond Platnumz ikiwa ni wiki moja toka atoke visiwani Zanzibar kusherekea birthday ya mama watoto wake, Zari.






Muimbaji huyo alikata keki mbele ya wasanii wake wa WCB huku akiwaacha midomo wazi mashabiki wake wa kwenye mitandao jamii kwa kitendo cha kusherekea birthday hiyo huku akiwa na nguo ya ndani ‘boxer’ akidai alikuwa anaogopa kumwagiwa maji. Pia mastaa mbalimbali walimtumia salamu za heri na baraka staa huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Salome’. Rich Mavoko Happy Birthday Big Nna Zawadi Yako Ya Gari Lakini La Udongo 😂😂 So Wambie Hao Wanaokumwagia Maji Nikilileta Waache Kwanza Harmonize Happy birthday my brother #simbaa nikisema niandike mengi sitomaliza ila unajuwa vyenye nakuzimia na na kukuheshimu….🙏🙏🙏 maisha marefu furahiya siku yako 🎂🔥🔥 Rayvanny Jus me and birthday boy @diamondplatnumz Bigie Mungu Akupe Maisha Marefu ndugu yangu maana ukinasa hatunasuliki mwiiiiiiiiingiiiiiiiii wa materials enjoy your day