HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday 7 October 2016

Said Ally, aliyetobolewa macho Buguruni Sheli hatoweza kuona tena



14474203_1683307165319633_2232738297854033920_n



Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana
 Said Ally aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena.
 
Makonda akimliwaza Said Ally baada ya madaktari kusema kuwa hakuna namna ya 
kumfanya awe kuona tena
Makonda ametoa majibu hayo ofisini kwake Ijumaa hii.
“Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote,” alisema Makonda.
“Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake,” alisema.
Pia Makonda amesema serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni kumi kama sehemu ya mtaji wake. “Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja,” aliongeza.
Kupitia Instagram pia, Makonda ameandika: Watanzania wengi tulitamani Said uone tena ila tumeshindwa, tuna mwachia Mungu.
Tayari mtu aliyemfanyia Ukatili huo yupo mahabusu.

No comments:

Post a Comment