Friday, 7 October 2016
Rais Magufuli ampongeza Bakhresa
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza Said Salum Bakhresa kwa kuwa mzalendo na kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi kupitia biashara zake.
Alisema hayo katika kijiji cha Mwandege wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani wakati akizindua kiwanda cha kusindika matunda kilichopo chini ya Kampuni ya Food Products mali ya kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) ya Dar es Salaam.
“Leo hapa kwenye kiwanda hiki cha kusindika matunda pekee, kimetoa ajira kwa Watanzania takribani 800, bado viwanda na kampuni zake nyingine zinazozalisha bidhaa kama vile maji na juisi ambazo zimetoa ajira kwa Watanzania wengi nchi nzima. Huu ndio uwekezaji ambao awamu ya tano tunauhitaji,” alisema.
Rais Magufuli pia alimpongeza Bakhresa kwa kuwa Mtanzania na mzalendo wa kwanza kuanzisha viwanda mbalimbali, ambavyo pamoja na kuchangia katika pato la taifa kwa kulipa kodi, lakini pia vinatengeneza ajira kwa watu wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment