HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Saturday 24 September 2016

Picha za birthday pati ya Zari The Boss Lady huko Zanzibar.



Diamond Platnumz amemfanyia pati ndogo Zari The Boss lady kati siku yake ya kuzaliwa, pati hii imefanyika visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na watu maarufu kama Mose Iyobo, Aunty Ezekiel.
Mtoto wao Princes Tiffah naye alikuwepo kwenye pati hio.
1 2 3 5 6 7

VIDEO: Alivyoperfom Vanessa Mdee kwenye kituo cha TV cha Citizen Kenya

Ni fahari kubwa kuona wasanii wa nyumbani kuvuka mipaka ya Tanzania na muziki wao kukubalika mpaka nchi za nje ya Tanzania, Msanii wa kike kutoka Bongoflevani, Vanessa Mdee amezikamata headlines baada ya kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaoperfom kwenye Coke Studio ambayo atafanya collabo na msanii wa Marekani, Trey Songs nchini Kenya.
Licha ya kuchaguliwa Coke Studio alifanya pia interview na kituo kikubwa cha kenya cha Citizen na alifanya perfomance ambayo ilivutia watu wengi, kama ulimiss kuona perfomance hii nakusogezea video hapa chini pamoja na interview ilivyokuwa.

Clinton ambuluza Trump kwenye kura za maoni



Hillary Clinton ameongoza kwa pointi 6 zaidi dhidi ya mpinzani wake Donald Trump wakati wakielekea kuchuana kwenye mdahalo wa kwanza Jumatatu ijayo.
Clinton, Trump pick up big wins
Kura hizo za nchi nzima zimetolewa Ijumaa hii. Kura za McClatchy-Marist zilionesha kuwa Clinton ana 45% huku Trump akiwa na 39%.
Wiki hii kura za maoni za Wall Street Journal/NBC zilionesha Clinton anaongoza kwa 43% dhidi 37% za mpinzani wake. Clinton anaendelea kuwa na kura nyingi zaidi kutoka kwa wapiga kura weusi akiwa na asilimia 93% na Trumo 3%.
Clinton pia ana wapiga kura wengi walatino kwa asilimia 74% dhidi ya 16% za mpinzani wake.

Video: Trey Songz azungumzia muziki wa Afrika, ubaguzi Marekani na mengine





14294766_1765695427047048_7130037601355956224_n


Trey Songz alipata fursa ya kuzungumza na mtangazaji wa NTV, Larry Madowo kuhusu mambo kibao kuanzia Afrika na muziki wake, alivyojisikia kwenda Kenya na kurekodi na wasanii wa Afrika akiwemo Vanessa Mdee na wengine, ubaguzi wa rangi unavyoendelea Marekani na mengine kibao.


Amezungumzia pia jinsi alivyo na hamu ya kufanya wimbo na Beyonce.
Akiwa Kenya staa huyo alipata fursa ya kupanda matatu na kuzunguka Nairobi.
14294784_958858954242469_3282623618634219520_n
14276418_1479539792063112_1134167972290494464_n

Video: Tox Star Ft. Barnaba – Chillax

Msanii Tox Star ameachia video mpya ya wimbo unaitwa “Chillax”, amemshirikisha Barnaba. Video imeongozwa na Kwetu Studios.

Video: J.Martins Ft. Ferre Gola – Ekelebe

Don Family Music Group Presents J.Martins With his new Visuals Dubbed ‘Ekelebe’ Which he Teams up with the Sensational DR Congo singer Ferre Gola.

Video: Abela Music ft Izzo Bizness – Balaa

 Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Abela Music ameachia wimbo aliomshirikisha member mwenzake wa kundi la The Amazing, Izzo Bizness. Wimbo unaitwa Balaa na video imeongozwa na Extra Films.

Video: Juma Nature – Mtumba

Msanii mkongwe katika mziki wa bongo fleva Juma Nature ameachia video mpya ya wimbo unaitwa “Mtumba”. Video imeongozwa na kampuni ya EMPTYSOULZ PRODUCTION.

Hizi ndio Kampuni 10 za Ndege zenye usalama zaidi duniani



Hi ni jinsi ajali za ndege zilivyochukua headlines miaka michache iliyopita, hali hiyo imefanya makampuni ya usafirishaji wa ndege duniani kuboresha huduma zao kwa kununua ndege za gharama na imara ili kuweka ushindani wa kibiashara na kuongeza usalama kwa wateja wao. Mpaka sasa usafiri wa ndege ndio pekee unaotajwa kuwa salama zaidi kuliko usafiri wa aina nyingine yeyote. 
flight-takeoff-hd-20
Ripoti iliyotolewa na JACDEC Airline Safety Ranking 2016, imezitaja kampuni 60 za ndege zenye usalama zaidi duniani. Leo nakuletea Top 10 ya kampuni hizo mtu wangu. JACDEC inasimama badala ya Jet Airliner Crash Data Tathmini Centre, ambao hutoa uchambuzi juu ya usalama wa kimataifa kwenye biashara za anga tangu 1989.
ndege
Hii ni kampuni ya usafirishaji kutoka Ureno, imekamata nafasi ya 10 ikifatana na kampuni ya Japan Airlines. TAP wameshikika nafas hii baada ya kuongeza idadi ya ndege kubwa pamoja na kupewa kibali cha kuongeza safari zao ambazo zinafikia asilimia 75 ya viwanja wanavyotua kila siku duniani. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni 0,015 unaowaweka kwenye nafasi ya 10 ya ndege salama duniani.

Japan Airlines sio tu ni salama, hawa wana sifa nyingine nzuri, kufanya kazi zao on time. Mwaka 2015 walipewa tuzo ya kufikisha aslimia 89.44% ya ndege zao kufanya safari ndani ya muda uliopangwa, na kuwa ndege za kwanza barani Asia na upande wa Pacific kuweka rekodi hiyo. Ulinzi pia imetajwa kama sifa yao kubwa, Uwezekano wa ndege zao kupata ajali umetajwa kuwa 0.015 kwa mwaka 2016 kinachowaweka kwenye nafasi ya 9.

Hii ni kampuni kutoka Abu Dhabi ambayo slogan yao ni “From Abu Dhabi to the World”. Etihad inafanya safari zakr kwenye mabara matano kati ya saba duniani. Kampuni hii imefungua pia chuo cha marubani ambako kinawatrain wanafunzi ili kupata marubani wapya siku za usoni watakaofanya kazi kwenye ndege za umoja wa falme za kiarabu. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni kwa asilimia 0.013.

Kwanza ndio kampuni ya ndege pekee duniani zenye rangi nyeusi ikiwa na safari zake kwenye miji ya Osaka, Houston na Vietnam, huku wakishirikiana na Trans-Tasman, Air China, Singapore pamoja na United Airlines ili kusafiri kwenye nchi nyingi zaidi. maeneo ambayo wanafanya safari nyingi zaidi ni Adeline, Melbourne, Sydney na Tasmania huko Australia, pamoja na Bali. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni asilimia 0.011 kwa mwaka 2016, hii inawafanya washike nafasi ya 7 kwenye list ya ndege salama zaidi duniani.

6. KLM
Moja kati ya brands kubwa kutoka nchini Uholanzi: KLM Royal Dutch Airlines. Inafanya safai zake Ujerumani, ndani ya Uholanzi, Norway, nchi za Ulaya pamoja na Marekani, ni moja kati ya kampuni kongwe kwenye usafiri wa ndege duniani, KLM ilianzishwa October 7, 1919, na wanakaribia kufikisha miaka 100 ya kutoa huduma za usafiri wa ndege. Hii inakamata nafasi ya 6th ikiwa na uwezekano wa ndege zake kupata ajali kwa asilimia 0.010, imefungamana na Hainan Airlines.
Sifa kubwa ya Hainan Airlines ni kutunza utamaduni wa nchi yao, hawa wanatokea Japan, basi hata wahudumu wake muda wote wanakua wamevalia mavazi yenye utamaduni wa Kijapan. Pia muonekano wa ndani ya ndege zao zote umenakshiwa kwa mapambo ya Kijapan. Hainan inafanya safari zake kwenye nchi za Marekani, Canada, Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa, Umoja wa Ulaya, Italia, Jamhuri ya Czech, Urusi, Kazakhstan, Israel, China, Taiwan, Japan, Hong Kong, Thailand na Australia. Iko nafasi ya 5th ikiwa na uwezekano wa kupata ajali kwa asilimia 0.010 ya viwango vya usalam wa ndege.

Qatar Airways ilianzishwa miaka 25 iliyopita. Na ilianza safari zake mwaka 1994 ikiwa inamilikiwa na familia ya kifalme ya Catari. Kampuni hii inamiliki brands nyingine nyingi za ndege ikiwa ni pamoja na hisa kubwa zaidi za uwanja wa ndege wa Doha, The International Airport of Doha. Kazi yao nzuri imewaweka kwenye naffasi ya 4th wakiwa na morali ya kupanda zaidi siku zijazo. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni asilimia 0.009.

 3. EVA Air
Kampuni ya Hello Kitty ndio wamiliki wa Eva Air. Ni kampuni ya Kijapan ambayo iko tofauti sana kwenye ndege zake zote, kila ndege ya kampuni hii imegawanywa sehemu ya kukaa watoto peke yao na wanapewa midoli huku sehemu za kukaa watu wazima kuna specila treatment ya nyama na mboga mboga. Hii iko nafasi ya 3 na uwezekano wa ndege zake kupata ajali ni asilimia 0.008.

2. Emirates
Inafahamika pia kama Fly Emirates. Asili yake ni Dubai, na inamilikiwa na serikali ya United Arab Emirates. Hii ina sifa kubwa kutoa huduma kwa kiwango cha kifalme na ifanya safari zake kwenye viwanja zaidi ya 150 katika mabara 6. Uwezekano wa ndege zake kupata ajali ni chini ya asilimia  0.007, na wanapambana kumantain au kupanda zaidi kwenye nafasi ya pili.

Hii ni kampuni kutoka Hong Kong na inafanya safari zake kutoka Hong Kong kwenda, Taipei, Bangkok na Singapore. Kitu cha kipekee kwenye ndege hizi ukiwa mteja wa mara kwa mara unapewa Club Membership Card ambayo inakufanya uweze kupata huduma za starehe bila malipo ya ziada. Imetajwa kwenye nafasi ya 1 huku kiwango cha uwezekano wa ajali ni mdogo kufikia 0.006.

Friday 23 September 2016

Maajabu ya Mombasa: joka kubwa linalovalia vifuli lapatikana baharini

Bilionea aliyewekeza Tanzania kaongelea mpango wake wa kuinunua Arsenal


Bado headlines za mfanyabiashara na bilionea namba moja Afrika mpango wake wa kutaka kuinunua Arsenal haujafa katika kichwa chake na bado ana imani ipo siku atakamilisha mpango huo Aliko Dangote, bilionea huyo tayari ameweka wazi tena katika interview zake kuwa lengo lake bado lipo palepale.
Aliko Dangote ambaye ni bilione namba moja Afrika ni miongoni mwa raia wa kigeni waliowekeza Tanzania, Dangote ndio mmiliki wa kiwanda cha Cement kilichopo Mtwara, kwa mara ya kwanza Dangote alitaka kuinunua Arsenal mwaka 2010 lakini lengo lake hilo halikutimia.
030812-global-african-billionaires-aliko-dangote
Bilionea namba moja Afrika ambaye ni raia wa Nigeria Aliko Dangote
Bilionea huyo ambaye ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 10.9 unaotokana na biashara zake mbalimbali zikiwemo za Cement na bidhaa mbalimbali amenukuliwa kituo cha TV cha New York bado hajaonesha kukata tamaa na mpango wake.
“Bado na matumaini ipo siku kwa bei sahihi nitainunua Arsenal, naweza kuinunua ipo siku bali sio kwa pesa kidogo ila ni kwa bei ambayo wamiliki hawatotaka kuikataa, najua mipango yangu labda katika kipindi cha miaka mitatu au minne baadae”
Asilimia 67 ya hisa za Arsenal inamilikiwa na bilionea wa kimarekani Stan Kroenke na mabilionea wawili wengine  Alisher Usmanov na Farhad Moshiri wao wanamiki asilimia 30 ya hisa za Arsenal.

Juma Nature adai muziki umetawaliwa na rushwa, ‘roho inauma sana’


Msanii mkongwe wa muziki nchini, Juma Nature amefunguka kwa kusema kuwa muziki umetawaliwa na rushwa ambapo amewataka wamiliki wa redio na runinga kuweka wazi viwango vya ‘promo’ kwa nyimbo za wasanii ili kila msanii ajipange jinsi ya kukabiliana na janga hilo.
Juma-Nature
Akizungumza na waandishi Alhamisi hii katika maandalizi ya Tamasha la Siku ya msanii litalofanyika katika Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho kuanzia Septemba 24 hadi 26 mwaka huu, Juma Nature alisema anashangaa kuona hata yeye nyimbo zake hazipigwi katika baadhi ya radio.
“Kama wanataka fedha ili wapige nyimbo katika redio zao waweke wazi itambulike kuwa mtu anapokuja na nyimbo ama albamu yake ili ipigwe anatakiwa alipie kiasi fulani badala ya hali mbaya ilivyo sasa katika muziki,” alisema Nature.
“Roho inauma wasanii tunateseka sana, lakini nyimbo hazipigwi. Kama mimi ni msanii mkubwa nyimbo zangu zisipopigwa roho yangu hainiumi sana, lakini hawa chipukizi wanaotakiwa watoe pesa ndiyo nyimbo zao zipigwe, wanapata wapi hizo fedha ni bora watangaze kiasi kimoja lijulikane moja,”
Pia msanii huyo alisema vituo vingi vinapiga nyimbo nyingi za Nigeria kuliko za ndani hali ambayo inaudhoofisha muziki wa ndani.
Juma Nature sio msanii wa kwanza kulalamika rushwa kwenye vituo vya redio, pia Ben Pol aliwahi kulalamikia suala hilo.

VIDEO: Baada ya Daraja la Kigamboni, Daraja lingine kujengwa Dar es salaam

4


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya Mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young, Ikulu Jijini Dar es Salaam na baada ya mazungumzo hayo Rais Magufuli amepokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salender litakalojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi huyo.
Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na daraja hilo litasaidia kupunguza adha ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Ujenzi wa Daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo Agha Khan kupitia baharini Jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza Mwezi Juni Mwakani baada ya Serikali ya Tanzania kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa fedha za ujenzi kutoka benki ya Exim ya Korea. 
>>>’Mchakato wa kulijenga hili daraja la Salender unaendelea vizuri kwa sababu hivi sasa kampuni ya Kikorea ambayo inafanya usanifu ipo kwenye hatua za mwisho na zabuni zinategemewa kutangazwa mwezi wa tatu Mwaka kesho na zitakwenda haraka, kwa hiyo mambo yakienda vizuri ujenzi unaweza kuanza mwezi wa sita, bahati nzuri fedha zote zipo na zimeshatolewa na Benki ya Exim ya Korea’:- Rais Magufuli.

Zari ajipongeza kwa zawadi ya mjengo toka wa Diamond

Diamond Platnumz ameingia kwenye headlines tena baada ya kupost nyumba kwenye instagram yake leo September 23 2016 ambayo ni siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake Zari ambayo amemfanyia kama suprise aliyomnunulia nchini South Afrika, na kuweka caption nzito na hivi ndivyo alivyotiririka.
>>’They are busy bragging them selves that they are Rich while their Kids staying in the Renting House… and today a person that, they are daily abuse and saying that he’s broke & Poor Bought a House, so that their Kids can have a better life, as they always wish on Social Media….. Happy Birthday Mama tee i hope you like our new South African House….Can’t wait for your Big weekend in Zanzibar tomorrow….I love you So much mama tee, we ndio Salome wa Moyo wangu pekee @zarithebosslady 😙🌷🎉🎂🎂🎉🌷 (Wanakazana kujisifu Matajiri Ilhali watoto zao wanaishi kwenye Nyumba zakupanga… halaf leo yuleyule wanaemtukana kutwa kwenye Mitandao kuwa Masikini, kajawa na shida, Kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi Maisha bora kama wanayoyatamani… Heri ya siku ya Kuzaliwa Mama tee wangu…. Nakupenda sana na unalifahamu hilo…natumai umeipenda Nyumba yetu hii mpya South Africa… nasubiria kwa hamu kusheherekea nawe siku yako hii kubwa kesho zanzibar….😙🌷🎉🎂🎂🎉🌷)@VodacomTanzania#VodacomKaziNiKwako#VodacomHapaKasiT

zari


Umewahi kumzawadia nini mpenzi wake katika siku yake ya kuzaliwa?

Tyga alimpa Kylie Jenner gari la kifahari, lakini Diamond kampa Zari mjengo! Ndio maana raia huyo wa Uganda anasema, wenye wivu?



Sikiliza Mzee Majuto Akitongoza Mrembo Ucheke hadi Ulie

Cheka Uongeze Siku

Thursday 22 September 2016

Ukiachana na tuzo za MTV, Diamond katajwa tena kwenye tuzo nyingine

Baada ya Diamond Platnumz kutajwa kuwania tuzo  za MTV MAMA 2016 zinazotolewa na kituo cha TV cha MTV Base Africa, sasa Tuzo nyingi zinazidi kutambua juhudi na kazi yake kwenye muziki wa Tanzania ambapo good news ni kwamba amepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za Ghana Music Awards UK.
Tuzo za Ghana Music Awards UK zinazoandaliwa kwa ushirikiano wa kampuni mbili za Alordia Promotion & West Coast UK Entertainment za nchini Ghana na Uingereza.
Diamond Platnumz anawania tuzo hii kupitia kipengele cha AFRICAN ARTIST OF THE YEAR akichuana na mastaa wengine akiwemo Patoranking, Fally Ipupa, Davido, AKA, Wizkid, Olamide na Tekno Milles.
Sherehe za utoaji wa tuzo hizi zimepangwa kufanyika jijini London, Uingereza mnano November 5 2016.
Hii ni List nzima ya wasanii waliotajwa kuwania tuzo hizo kwenye vipengele 26.
AFRICAN ARTISTE OF THE YEAR
Patoranking
Fally Ipupa
Davido
AKA
Wizkid
Diamond Platnumz
Olamide
Tekno
BEST CLUB DJ OF THE YEAR
DJ Bibi
DJ Fiifi
DJ Invisible
DJ Sawa
DJ Billy
DJ Chris Vibez
GOSPEL SONG OF THE YEAR
Hour by Hour – SP Kofi Sarpong ft. Joyce Blessing
M’asem (Yoboyo) – Kofi Gyan
Wowo Nkwa Wo Wo Ade3 – Mary Owusu
Hyebre Sesafo – Obaapa Christy
Wafom Kwan – Patience Nyarko
Aporsor – Nicholas Omane Acheampong
GOSPEL ARTISTE OF THE YEAR
Obaapa Christy
Nicholas Omane Acheampong
Joe Mettle
SP Kofi Sarpong
Patience Nyarko
Preachers
NEW ARTISTE OF THE YEAR
Nero X
Kofi Kinaata
Wisa
Atom
Mr. Eazi
Nii Funny
MUSIC PRODUCER OF THE YEAR
Mobeatz – Skolom
Bisa Kdei – Brother Brother
Kaywa – Mansa
Beatz Dakay – Mightylele
Dr. Ray – Yewo Krom
Kin Dee – Susuka
The Maker – Chop Kiss
BEST MUSIC VIDEO OF THE YEAR
MzVee – Hold Me Now
Joey B – U And Me
Obrafour – Nkontompo
YaaYaa – Dumb Drum
Edem – Girlfriend
Teephlow ft. Sarkodie – The Warning
Mr Eazi ft. Sarkodie – Anointing
Becca ft. Bisa Kdei – Hwe
VVIP ft. Samini – Dogo Yaro
BEST GROUP OF THE YEAR
VVIP
R2Bees
Keche
4×4
BEST RAPPER OF THE YEAR
EL
Guru
Yaa Pono
M.anifest
Pappy Kojo
Flowking Stone
Obrafour
Edem
Sarkodie
Omar Sterling
HIPLIFE SONG OF THE YEAR
Atom – Yewo krom
EL – Koko
Wisa – Ekikimi ft. Luther
VVIP – Skolom ft. Sena Dagadu
Guru – Pooley Swag
Mr. Eazi – Hollup
HIGHLIFE SONG OF THE YEAR
Bisa Kdei – Mansa
R2Bees – Makoma
Bisa Kdei – Brother Brother
Kofi Kinaata – Susuka
Ofori Amponsah – Alewa ft Sarkodie
Kwabena Kwabena – Tua Mu Daa
HIGHLIFE ARTISTE OF THE YEAR
Bisa Kdei
Afriyie
Ofori Amponsah
Nero X
Kwabena Kwabena
MOST POPULAR SONG OF THE YEAR
Mansa – Bisa Kdei
Brother Brother – Bisa Kdei
Go Higher – Stonebwoy
Ekikimi – Wisa ft. Luther
Baby (Chop Kiss) – Shatta Wale
Yewo Krom – Atom ft. Jhunea
Susuka – Kofi Kinaata
Kakai – Shatta Wale
REGGAE / DANCEHALL SONG OF THE YEAR
Go Higher – Stonebwoy
Enemies – Jupitar ft Sarkodie
Mightylele – Stonebwoy
Kakai – Shatta wale
Hold it – Shatta Wale
Pumpum – Rudebwoy Ranking ft Episode
REGGAE / DANCEHALL ARTISTE OF THE YEAR
Stonebwoy
Jupitar
Samini
Episode
Mzvee
Shatta wale
AFROBEATS ARTISTE OF THE YEAR
Mr. Eazi
D-Cryme
Pappy Kojo
Kofi Kinaata
R2Bees
Wisa
BEST COLLABORATION OF THE YEAR
Mr. Eazi ft. Efya – Skin Tight
VVIP ft. Sena Dagadu – Skolom
Sarkodie ft. Akwaboah – Mewu
Pappy Kojo ft. Sarkodie – Aye Late
Wisa ft. Luther – Ekikimi
D-Cryme ft. Sarkodie – Koko Sakora
Mr Eazi ft. Eugy – Dance For Me
Jupitar ft. Sarkodie – Enemies
Becca ft. Bisa Kdei – Hwe
ALBUM OF THE YEAR
Mary – Sarkodie
Elom – EL
Breakthrough – Bisa Kdei
I Believe – SP Kofi Sarpong
After The Storm – Shatta Wale
Necessary Evil – Stonebwoy
Breaking News – Samini
ARTISTE OF THE YEAR
Shatta Wale
Nero X
Sarkodie
Stonebwoy
Bisa Kdei
SP Kofi Sarpong
EL
Mr. Eazi
BEST UK BASED GROUP
Kwamz & Flava
Vibez Squad
NSG
Kraze
CXCV
IRAY MVNT
BEST UK BASED AFROBEATS ARTISTE
Jaij Hollands
Mista Silva
K Weezy
Scob Original
Charsey
Kwamz & Flava
BEST UK BASED AFRO-POP ARTISTE
Zafi B
Eugy
Areatha Anderson
Tinchy Stryder
Prince Rapid
Fuse ODG
Stormzy
NSG
BEST UK GOSPEL SONG
Amazing God – Sonnie Badu
We Love You – Louisa Annan
Yebe Duru – Nhyira Hemaa
Jesus the Reason for the Season – Kwame Amponsah
Bisa Awurade – Betty Acheampong
Work In Progress – Diana Antwi Hamilton
BEST UK BASED GOSPEL ARTISTE
Sonnie Badu
Mama Fausty
Ohemaa Jackie
Antwi Diana Hamilton
Louisa Annan
Nhyira Hemaa
Osei Kofi
Kwame Amponsah
Betty Acheampong
Ohene Darko
BEST UK BASED MUSIC VIDEO
Tina – Fuse ODG ft. Angel
New Girl – Reggie N Bollie
Pinga – Jaij Hollands ft NSG
B.A.D (Best Achieving Don) – Mr Silva
Watch Nobody – Atumpan ft. Paigey Cakey
UK BASED GHANAIAN INTERNATIONAL ARTISTE
Fuse ODG
Tinchy Stryder
Sonnie Badu
Reggie N Bollie
Lethal Bizzle
Stormzy

Video: Pryshon ft Nem – Thinking

A video that is directed by J blessing is always considered worth by many of his East African followers. Clearly, Pryshon ft Nem are the new talk of East Africa. This new video was recently launched with Mseto East Afric

Video: Lady Gaga – Perfect Illusion

Msanii wa muziki wa Pop Marekani, Lady Gaga ameachia video yake mpya ya wimbo wa Perfect Illusion. Video imeongozwa na Andrea Gelardin pamoja na Ruth Hogben. Tazama hapa chini video hiy

Video: Trey Songz amuita Vanessa Mdee ‘baby’,

Akisifika kama bingwa wa nyimbo za kutafutia watoto chumbani na pia akiwa na mashabiki wengi zaidi wa kike, Trey Songz akimuita mpenzi wako ‘baby’ ni lazima moyo ukudunde!

Muimbaji huyo wa ‘Nana’ yupo Nairobi, Kenya alikoenda kurekodi kipindi cha Coke Studio Africa msimu wa nne. Vanessa ambaye ni miongoni mwa wasanii takriban kumi wanaorekodi naye wimbo, amepost video ikiwaonesha wakiwa na staa huyo. Trey anaonekana kuwapanga waimbaji hao kwaajili ya video ya pamoja na anasikika akimwambia Vanessa ‘baby you are not following the rules’ na kukaribisha kicheko kwa wote. Vanessa anakiri kumkubali mno Trey na kwamba kukutana naye ni mwanzo wa dalili za yeye kutimiza ndoto yake ya kuja kushinda tuzo ya Grammy kama yeye. “Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo,” alisema Vanessa. Kwa upande wake Trey, ameandika kwenye Instagram: Had an amazing day in Nairobi. Exhausted as ever but feeling very full of life. So many blessed moments here and heavy on my heart is home. Caught this image in the studio while working with some great people. Sending prayers up for love and positivity to you all, cause we all need it. Love.”

Video: Brown Mauzo Ft. Alikiba – Nitulize

Msanii kutoka nchini Kenya ajulikanae kama Brown Mauzo ameachia video mpya wimbo unaitwa “Nitulize”, amemshirikisha King kutoka Tanzania Alikiba. Video imefanyika South Africa imeongozwa na Nicorux.

Wednesday 21 September 2016

Trey Songz atua Nairobi kushiriki Coke Studio Africa msimu wa 4


Muimbaji wa RnB kutoka Marekani, Trey Songz ametua mjini Nairobi, Kenya kushiriki kwenye msimu wan nne wa kipindi cha Coke Studio Africa.
14262650_862277083907144_2037035864_n
Trey Songz baada ya kutua uwanja wa ndege nchini Kenya
Muimbaji huyo anatarajiwa kurekodi nyimbo na baadhi ya wasanii wengine wa Afrika ambao watashiriki kwenye kipindi hicho akiwemo Vanessa Mdee (Tanzania), Rema Namakula (Uganda), Yemi Alade (Nigeria), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), Nyashinski (Kenya) na Emtee (South Africa).
lunch
Trey Songz akila chakula cha mchana na washiriki wengine wa kipindi cha Coke Studio
Uongozi wa kipindi hicho umeandika ujumbe kwenye mtandao wao wa Instagram unaosomeka, “Welcome to Nairobi Kenya Trey Songz, it is a great honour to host you for #cokestudioafrica.”
Hii ni mara ya tatu kwa msanii kutoka Marekani kushiriki kwenye kipindi hicho, wengine waliowahi kushiriki ni pamoja na Wyclef Jean na Ne-Yo.