HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Thursday, 22 September 2016

Video: Trey Songz amuita Vanessa Mdee ‘baby’,

Akisifika kama bingwa wa nyimbo za kutafutia watoto chumbani na pia akiwa na mashabiki wengi zaidi wa kike, Trey Songz akimuita mpenzi wako ‘baby’ ni lazima moyo ukudunde!

Muimbaji huyo wa ‘Nana’ yupo Nairobi, Kenya alikoenda kurekodi kipindi cha Coke Studio Africa msimu wa nne. Vanessa ambaye ni miongoni mwa wasanii takriban kumi wanaorekodi naye wimbo, amepost video ikiwaonesha wakiwa na staa huyo. Trey anaonekana kuwapanga waimbaji hao kwaajili ya video ya pamoja na anasikika akimwambia Vanessa ‘baby you are not following the rules’ na kukaribisha kicheko kwa wote. Vanessa anakiri kumkubali mno Trey na kwamba kukutana naye ni mwanzo wa dalili za yeye kutimiza ndoto yake ya kuja kushinda tuzo ya Grammy kama yeye. “Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo,” alisema Vanessa. Kwa upande wake Trey, ameandika kwenye Instagram: Had an amazing day in Nairobi. Exhausted as ever but feeling very full of life. So many blessed moments here and heavy on my heart is home. Caught this image in the studio while working with some great people. Sending prayers up for love and positivity to you all, cause we all need it. Love.”

No comments:

Post a Comment