Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume.
Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza
kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua
wanaume wengi duniani.
Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni KUKOSA MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOSA KABISA NGUVU,
huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili
ambalo linawasumbua zaidi wanaume, ingawa na wanawake wanakabiliwa na
sehemu ndogo ya tatizo hili.
Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume
wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
umeonesha kuwa, sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia
zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na
matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo
bila hata kutumia vidonge wala dawa za miti shamba.
Ingawa Matabibu wanataja magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la
damu, magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi, umri mkubwa kuwa ndiyo
chanzo cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume, lakini imebainika kuwa
idadi kubwa ya wanaume wanaofika hospitalini kutafuta nguvu za kiume
hawana magonjwa hayo
Huu ni ushahidi kuwa wanaokabiliwa na janga hili wamebeba tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume kimawazo zaidi kuliko hali halisi.
Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini kuwa, wale
wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni
mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa
tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na kwamba wanaishi kwa kusikia
zaidi ya kujitambua.
Katika hali ya kawaida kila mwanadamu ameumbwa kwa njinsi yake na
inapotokea kushabihiana basi ni bahati, lakini mara nyingi usawa
hupatikana kwa mmoja kujifunza au kusaidiwa kufikia kiwango cha mtu
anayemuhitaji kuwa nae katika maisha hasa ya kimapenzi. Jambo hili
wataalamu wanasema kuwa miili iko tayari kutii mafunzo na kubadilisha
tabia zake kulingana na utashi wa mhusika.
Tatizo kubwa lililopo kwa wapenzi wengi wanaolalamikia upungufu wa
nguvu ni kwamba maisha yao wanayachezea kwenye viwanja vya wenzao
wanaokutana nao katika vijiwe na sehemu za kazi.
Usikivu wa mazungumzo toka kwa wanaume wengine wenye uwezo wa
kwenda mara nne hadi saba katika tendo au wanatumia dakika arobaini
kufika kileleni umewafanya wanaume wengi kujihisi tu kuwa wao wanakasoro
eti kwa kuwa huishia mara mbili au moja katika kufanya tendo.
Dhana ya kujiona ni mwenye kasoro inapojengeka akilini mwa
mwanaume, huchipua hofu na hatimaye kumfanya ashindwe kabisa kusisimka
anapofikiria au kukutana na mwanamke. Matokeo ya hangaiko la akili
hushusha uwezo wa mwili na kumuongoza mtu kwenye kuwaza ugonjwa kisha
kukimbilia hospitali au kwa waganga kutafuta tiba ya ugongwa ambao
kimsingi hanao.
Lakini ukweli uko wazi kwamba kukimbilia kutafuta uwezo wa
kufanya mapenzi mara sita au saba hakumfanyi mwanaume awe mlinganifu
mwenye kusifiwa na wanawake wengi, kwani si wanawake wote wana uwezo wa
kufanya mapezi kwa raundi hizo na si wote wanapenda kutumia takika 30
kucheza mpira wa kikubwa, wengine hukinai mapema na huona kero kuwa na
wanaume ving’ang’anizi wenye sifa za kuganda wanapopewa.
No comments:
Post a Comment