HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday, 8 June 2016

Siku 20 baada ya ndege ya Misri kupoteza mawasiliano, leo June 8 nyingine imetua Uzbekistan kwa hofu ya bomu


Leo June 8 2016 CCTV Africa wameripoti habari nyingine tena inayohusu ndege ya Misri iliyokuwa inatoka Cairo kuelekea Beijing China, ikiwa zimepita siku 20 toka ndege ya EgyptAir Flight 804 kuripotiwa kupoteza mawasiliano ikitokea Paris Ufaransa kuelekea Cairo, leo tena June 8 EgyptAir imegonga tena headlines.
Ndege ya EgyptAir leo June 8 iliyokuwa inatoka Cairo kuelekea Beijing China imelazimika kutua kwa dharura Uzbekistan kutokana na kuripotiwa kuwa na hofu ya bomu, maafisa wa anga wa Uzbekistan wameripoti ndege aina ya Airbus A330-220 imetua kwa dharura Uzbekistan ikiwa na abiria 118 na watumishi wa ndege 17.
Maafisa wa Misri walipigiwa simu Airport Cairo na mtu asiyejulikana na kutoa taarifa kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A330-220 iliyokuwa inaelekea Beijing ina bomu ndani, hivyo ikabidi itue kwa dharura Uzbekistan  ili kupatiwa msaada, abiria na watumishi wa ndege hiyo wameripotiwa kuwa salama

No comments:

Post a Comment