HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday 8 February 2017

BREAKING: Wabunge wa upinzani watoka nje ya Ukumbi wa Bunge

Kutoka Dodoma Bungeni sasa hivi naambiwa Wabunge wa Upinzani wametoka nje ya ukumbi wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Naibu Spika Dr. Tulia.
Inaripotiwa kwamba Naibu Spika Dr. Tulia aliamuru kutolewa nje kwa Mbunge Halima Mdee na mwenzake waliopaza sauti ndani ya bunge baada ya Naibu spika kukataa mwongozo wa kujadili sababu za kukamatwa kwa Mbunge Tundu Lissu jana.
Baada ya amri ya kuwatoa nje Halima Mdee na mwenzake inaripotiwa na Wabunge wengine wa upinzani wakachukua uamuzi wa kutoka nje ambapo hapa chini kwenye hii video fupi wanaongea Zitto Kabwe na Halima Mdee.
.

PICHA:Kutana na orodha ya nchi zenye joto kali zaidi duniani.


Kila nchi duniani ina sifa zake kwenye ishu ya hali ya hewa ambapo kwenye nchi nyingine kuna Joto na kwengine kuna baridi pia wengine wakiwa na hali ya hewa ya wastani, sasa leo February 7, 2017 nimekukusanyia hizi sehemu 10 zilizotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha joto duniani.
1.QATAR
Wakati wa msimu wa joto, nchini Qatar kumeripotiwa kuwa na joto kali na kuna muda hali ya joto hupanda mpaka kufikia nyuzi joto 50 ambapo pamoja na kuwa na joto kiasi hicho Qatar imebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini, mafuta na gesi. 
Rasilimali hizi zimeifanya Qatar kuwa nchi ya kwanza duniani kwa utajiri.
2. BOTSWANA
Botswana inashika nafasi ya pili kwa kuwa nchi yenye joto kali duniani ambalo linafika nyuzi joto 40 na inaelezwa kuwa 70% ya joto hilo huchangiwa na jangwa la Kalahari.
3. VIETNAM
Vietnam ni nchi yenye mfumo wa utawala wa Kisoshalisti kutoka bara la Asia, mji mkuu wa nchi hiyo ni Hanoi unatajwa katika nafasi ya tatu katika maeneo yenye joto kali duniani, inaelezwa kuwa kiwango cha chini cha joto ni nyuzi joto 20 wakati kiwango cha juu kinafikia nyuzi joto 42.
4. UNITED ARAB EMIRATES (UAE)
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unatajwa kuwa kati ya sehemu zenye uchumi unaokua kwa haraka zaidi duniani, moja ya falme zake (Abu Dhabi) inatajwa kuwa na joto linalofikia nyuzi joto 45 wakati kiwango cha chini ni nyuzi joto 25.
5. BAHRAIN
Bahrain ni moja kati ya nchi ndogo barani Asia, inatajwa kuwa joto lake hufikia nyuzi joto 40 wakati kiwango cha chini ni nyuzi joto 17.
6. JAMAICA
Jamaica inashika nafasi ya sita katika nchi zenye joto kali ikiwa na kiwango cha chini cha nyuzi joto 27.
7. MALAYSIA
Malaysia ni moja kati ya nchi za Kiislamu na mji mkuu wake ni Kuala Lumpur wakati Putrajaya ni jiji kubwa zaidi nchini humo, hali ya hewa ni joto linaloanzia nyuzi joto 25-35 mpaka kufikia nyuzi joto 40.
8. INDIA
India ni nchi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu kwenye barala Asia, kiwango cha juu cha joto kinazidi nyuzi joto 48 wakati kiwango cha chini ni nyuzi joto 28, ingawa kuna maeneo ya milima hupata baridi mpaka nyuzi 1.
9. INDONESIA
Indonesia inatajwa kuwa ndio nchi kubwa ya kiislamu duniani na mji wake mkuu ni Jakarta ukiwa na visiwa vingi huku kukiwa na rekodi ya joto linalofikia nyuzi 30.
10. ETHIOPIA
Ethiopia ni nchi ya Kiafrika na mji mkuu wake ni Addis Ababa ambao unatajwa kuwa na joto linalofikia nyuzijoto 35 wakati kiwango cha chini ni nyuzi joto 25.

Breaking: Mbowe, Gwajima, Idd Azan, Manji watajwa kwenye orodha ya pili ya Makonda



Mbunge wa Hai Freeman Aikaely Mbowe, mfanyabiashara mkubwa nchini, Yusuf Manji na Mchungaji Josephat Gwajima wametajwa kwenye orodha ya pili ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya watu mashuhuri wanaohusishwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya.

Makonda amemtaja pia mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azan na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pambakali kwenye orodha hiyo.
Ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo.
Watu hao watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.
Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.
Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.