HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Saturday, 28 May 2016

Top 10: Android Apps for Android Wear Users, May 2016


Last week during Google I/O 2016, the Internet giant had a lot to announce, but where Android Wear was concerned, they introduced us to Android Wear 2.0. While this new version of Android Wear is currently in a preview, it has a lot of new features and redesigned UI elements that we'll have to get used to this Fall, when it launches in earnest. For now, however, we're going to go over some of the best Android apps out there for Android Wear users that want to do more with their smartwatches.
Android Wear
This choice might seem incredibly obvious, but Android Wear doesn't ship on Android devices by default, so if you have an Android Wear device burning a whole in your pocket, you'll need to download Android Wear from the Play Store. Even if this is an obvious download for some, there are some settings buried within the Android Wear app that will be essential, such as the ability to mute your device when connected to your watch as well as control just which apps are allowed to pop up on your watch.
WatchMaker Premium
One of the main attractions of Android Wear is the ability to spend time messing around with all sorts of watch faces, and while there's a huge amount of them available in the Play Store, it's nice to also make your own or play around with the work of others. This is where WatchMaker comes in, the Premium version allows for much more control and such with your watch faces, but its main attraction is the ability to have one watch face turn into hundreds at a moment's notice. There's a huge community surrounding WatchMaker, and a really good one on Google+ that has all manner of watch faces to choose from, the majority of which are free to download and use.
Google Fit – Fitness Tracking
Wearable devices of any kind always have something to do with keeping fit and logging your activity, which is just what Google Fit offers users. There's a small app installed on Android Wear by default, but installing the full Google Fit app on your phone will update that Android Wear component and give you a central place to manage all of your activity and help you meet your fitness goals. Google Fit also plays nice with lots of other health services out there, and is well worth looking into if you want a smartwatch-cum-fitness tracker.
Wear Black when Charging
A lot of Android Wear watches out there will have a sort of animation or charging display to show users when their watch is tucked in for the night, but these can be annoying. Especially if it's close to where you sleep or is just too bright. This simple little app does away with the annoying bright light and just makes your watch as dark as the rest of the room when charging. Perfect for watches with a fancy charging stand and an animation to match, this will keep your watch dim overnight.
Wear Store for Wear Apps
Android Wear, just like Android proper is always moving, always being updated and there are always new apps arriving. That's why it can be quite difficult to pin down the essential apps, as there are always apps that are coming out of the woodwork. This one app will make it easy – by using your phone – to find all manner of Android Wear apps, including the absolute latest ones. Wear Store is designed exclusively to tell you which apps are designed for Wear and it takes you to the Play Store to install them.
Parrot – Voice Recorder
Parrot is predominantly an Android phone app, but it also has an Android Wear side to it, and it's a great voice recorder app all around, which makes it great for meetings and the like. Where the Android Wear side of things come in, Parrot can be used to make some covert recordings, record a meeting without getting your phone out or whatever else you need to do. This is one app that makes great use of the microphone that is made available on all Android Wear devices, and is well worth looking into.
WatchMaster – Watch Face
WatchMaster is an Android app that brings together all of the great-looking Android Wear watch faces from a number of different developers. This makes it nice and simple to find a really well-made and polished watch face for your Android Wear watch. What's great about this is the sheer variety that's on offer, whether or not you're looking for something like a more classic watch, or something a little playful or digital, WatchMaster will have something you want.
Google Keep
The whole point of having a small screen on your wrist all the time is arguably to be able to quickly and easily glance at all sorts of information and make sure that you take it in without having to dig out your phone all of the time. Google Keep is one of the best apps on Android Wear for that sort of thing, it has an always-on mode, it's easy to navigate and is really easy to use in frantic situations where you've forgotten everything except for how to be human.
Facer
Facer is similar to WatchMaker and depending on who you ask is better than WatchMaker, but then some people say the same about WatchMaker. Either way, this is an app that allows artists to create their own watch face designs as well as choose from hundreds upon thousands of other designs out there, something that a lot of people will find a big help when looking for watch faces for their new Android Wear device. Free to download and use, there is also a premium version available as well.
Runtastic
Runtastic is another great fitness app to use on Android Wear, and it's got all sorts of neat features on both the phone and watch app, but crucially for runners and long-walkers, the Android Wear app updates you on pace, time and so on. These can be customized in the settings on the phone app, and Runtastic has a number of other apps out there that offer other features that can be helpful for those looking to keep fit. It's free to download and try out, but there is a Premium version available as well.
The post Top 10: Android Apps for Android Wear Users, May 2016 appeared first on AndroidHeadlines.com |.

Friday, 27 May 2016

#AUDIO Ni marufuku kuvaa nguo fupi Sanya Hoye, sheria za viboko na faini zimetajwa

Moja ya matukio ambayo yanamake headlines katika Wilayani Siha Kilimanjaro ni pamoja na adhabu zinazotolewa kwa wale wanaovunja sheria, kingine ni kwamba kijiji cha Sanya Hoye kimepitisha adhabu ya faini ya Shilingi 50,000 pamoja na viboko 15 kwa atakayekutwa baa na mtoto mdogo au kuvaa nguo fupi. 
Mwenyekiti wa kijiji cha Sanya  Hoye, Moses Mnuo ametoa ufafanuzi wa maazimio waliyokubaliana katika kikao cha kijiji cha Sanya Hoye………
>>>tumepitisha sheria kwa mtu yeyote anayevaa nguo fupi kwa watoto wa kike ni marufuku tangu siku ile ya kikao kile, wanawake hao wanapotembea hapa usiku wana ajenda walizonazo wanafanya machafu yao kwa hiyo tutawapiga faini na hizo hela watapewa risiti’

Diamond achukua taji la Lip Sync Africa ya MTV

Diamond Platnumz amechukua taji la kipindi cha Lip Sync Africa kinachorushwa na kituo cha MTV SA. 13248947_844312172340600_275142530_n
D’Banj ambaye ni host wa show hiyo akimpongeza Diamond kwa ushindi
Alikuwa akichuana na mshkaji wake, Theo wa kundi la Mafikizolo. Kwenye kipindi hicho, wasanii wawili hushindana kuziimba nyimbo za wasanii wengine kwa kugandamizia na kupatikana mshindi mmoja.
Baada ya kuchukua ushindi huo na kupewa mkanda wake, Diamond aliandika kwenye Instagram: Ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuwajuza kuwa kijana wenu nimewawakilisha vyema kwenye mashindano ya LIP SYNC BATTLE AFRICA ya @MtvBaseAfrica na kuweza kuibuka kidedea kwenye Mashindano ya Stage hiyo na kunyakua Mkanda.”
13181345_179733292424560_2022858402_n
Naye Theo alikubali kushindwa na kumpongeza Diamond kwa ushindi huo.
13267326_1112449035442570_1532958103_n
Lip Sync Battle ni show iliyoanzia Marekani na kuongozwa na rapper LL Cool J na mke wa John Legend, Chrissy Teigen. Kwa Afrika show hiyo inaongozwa na

Video: Korede Bello – One & Only

Msanii kutoka Nigeria Korede Bello kutoka Record Lebo ya Mavin Records ameachia video mpya ya wimbo unaitwa “One & Only

Nakukaribisha kuisikiliza hii single mpya ‘Natafuta kiki’ ya msanii kutoka WCB Raymond

Ni Mei 25 ambapo msanii kutoka kwenye label ya WCB, Raymond anazimiliki spika za radio mbalimbali baada ya kutambulisha rasmi single yake mpya iitwayo Natafuta Kiki ambayo imetayarishwa katika studio za Wasafi Record.

Thursday, 26 May 2016

VIDEO: Kutana na Trafiki mwenye mbwembwe Dar, foleni haigandi akiwepo

Kama makazi yako ni Dar es salaam inawezekana umeshakutana nae askari huyu wa usalama barabarani, jina lake ni Ashraf Abas Shaban na maeneo yake ya kazi ni Bagamoyo Road, Sayansi na kama umegundua akiwa kazini foleni haigandi, ameipa heshima AyoTV na kuongea kidogo kuhusu yeye na kazi yake.
Anasema >>> ‘Ninavyoongoza magari kuna baadhi ya watu hawaendi na kasi yangu napenda watu waende na ile kasi yangu, Madereva wengine ni wazembe wanachat kwenye simu’ 


Bonyeza play kwenye hii video hapa chini kukutana nae

VIDEO: Smartphone ya kwanza ya Robot Duniani imeanza kuuzwa leo, Check uwezo wake

Teknolojia inazidi kukua kwa kasi na uvumbuzi wa vifaa mbalimbali vya urahisishaji wa kazi vinatengenezwa, kwa mara ya kwanza duniani simu iliyotengenezwa kama roboti imeanza kuuzwa rasmi leo May 26 2016, Simu hiyo imeitwa RoBoHon na imetengenezwa katika size kama simu nyingine isipokuwa tu muundo wake ambao ni kama binadamu ambaye anatembea na mwenye uwezo wa kucheza pia.roo
Simu hiyo iliyotengenezwa na kuzinduliwa huko Japan inauzwa paundi 1200 ambazo ni zaidi ya milioni 30 za kibongo . RoboHon ina uwezo wa kukusaidia kupokea simu unapokua busy na kujibu meseji kwa niaba yako na kuwa kama msaidizi wako binafsi pia inakukumbusha juu ya matukio muhimu unayopaswa kuyafanya.
roboh
robohon
Kampuni ya Sharp inasema itatengeneza simu 5000 za aina hiyo kila mwezi na inadhamiria kuwa kampuni inayoongoza katika mauzo ya simu za ai

VIDEO: Risasi zapigwa katikati ya show ya T.I New York Marekani, mmoja auwawa

Rapper T.I ambaye pia aliwahi kuja bongo kwenye FIESTA, alikuwa na show New York Marekani katika show usiku wa May 25 2016 akisindikizwa na Maino na Uncle Murda ambapo kabla T.I hajapanda kwenye stage, ilisikika milio ya risasi.
Taarifa ya polisi imesema mtu mmoja alifariki kwenye tukio hilo na wengine watatu kujeruhiwa ambapo Rapper Troy Ave amekuwa ni mmoja wa majeruhi baada ya kupatwa na moja ya risasi mguuni.
Mpaka sasa Polisi hawajamdaka yeyote aliehusika na ufyetuaji huo wa risasi na uchunguzi bado unaendelea huku ikisubiriwa kauli ya Rapper T.I kuhusu tukio hilo lililotokea kwenye show yake hiyo, unaweza kutazama hii video fupi hapa chini ya jinsi ilivyotokea.

Mayunga asema kwa sasa ana nafasi ya kufanya hata albamu na Akon

Msanii wa muziki wa Tanzania aliyefanya kazi na Akon baada ya kushinda shindano la Airtel Trace Music, Mayunga amesema nafasi ya kukutana na Akon na kufanya naye kazi imemhakikishia nafasi ya kufanya kazi nyingi zaidi.
Mayunga na Akon
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Mayumba amesema amejihakikishia nafasi ya kufanya hata albamu na msanii huyo mahiri kutoka Marekani.
“Nataka kushare na watanzania wasije wakaona Akon ndiyo basi tena, sijui nimeichezea bahati kwa Akon, labda ningemuacha na Akon aweke mistari yake mule no. Niseme tu kwamba na uwezo wa kufanya ngoma na Akon zaidi ya mbili, tatu, nne hata albamu naweza. Na hiki ni kitu ambacho nilikuwa nataka mimi, kwamba nikukutana na Akon lazima nitegeneza mahusiano ya kazi nyingine,” alisema Mayunga.

China yagundua teknolojia mpya itakayorahisisha usafiri

Wakati serikali ya Tanzania ikipambana kupunguza tatizo la usafiri na msongamano wa foleni kwa wananchi wake, Wachina wameanza kugundua teknolojia mpya ya usafiri ambayo itasaidia kupunguza foleni barabarani.
BASI
Teknolojia hiyo mpya ya usafiri haitaathiriwa na foleni za barabarani ambayo yatakuwa ni mabasi mapana ambayo kwa chini yanaruhusu magari kupita na kupishana bila wasiwasi wowote, huku yenyewe yakisafiri bila kulazimika kusimama kusubiri magari yapite, isipokuwa kwenye njia panda na kwenye taa za barabarani pekee.
Aidha basi hilo litakuwa na uwezo wa kubeba watu 1,200 kwa mara moja. Linatajwa kuwa ufumbuzi wa msongamano wa magari barabarani. Pia, lilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza wiki iliyopita huku magari mengine madogo yenye urefu wa futi 6.6 yanapita chini ya gari hilo jambo ambalo linaelezwa hupunguza idadi ya magari kwenye msongamano. Basi hilo linalotumia umeme na inaelezwa kwamba, linaweza kusafiri kilomita 60 kwa saa moja.
Shenzhen Hashi ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya China TBS Limited iliyohusika kutengeneza magari hayo amesema wametumia kiasi cha dola 74.1 kutengeneza basi hilo moja ambalo utengenezaji wake ulianza tangu mwaka 2010.
Tazama video hapa

Nitakuja tena Tanzania wimbo wetu na Diamond ukitoka – Ne-Yo (Audio)

Kuna uwezekano mkubwa staa wa Marekani, Ne-Yo akaja tena Tanzania kwa mara ya pili.
13269419_1109188999169399_1336650774_n
Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ baada ya show ya Jembeka Festival Jumamosi iliyopita, Ne-Yo alisema wimbo huo utaachiwa hivi karibuni.
“Baada ya wimbo kutoka ni lazima nije tena kwasababu tutautumbuiza,” alisema muimbaji huyo wa Miss Independent. “I will definitely be back,” alisema.
Wawili hao waliutumbuiza wimbo huo pamoja kwenye tamasha hilo lililofanyika jijini Mwanza. Msikilize zaidi hapo chini.

Wednesday, 25 May 2016

Maamuzi ya kesi ya Chriss Brown kuhusu malezi mabovu ya mtoto wake ‘Royalty

Kesi iliyokuwa inamkabili  staa kutoka  Marekani Chriss Brown juu ya malezi mabovu ya mtoto wake ambayo ilifunguliwa na mzazi mwenzake Nia Guzman, May 24 maamuzi yalitolewa na Mahakama ya Califonia.
Mama mtoto wa Royalty alidai kuwa Chris hana malezi sahihi na muongozo unaostahili juu ya mtoto wao, amesema Chris amekuwa akivuta sigara na bangi yeye na marafiki zake mbele ya mtoto wao na imempelekea Royalty kupata maradhi ya pumu.
cbbbb
Nia Guzman aliomba mahakama impunguzie Chris muda wa malezi ya mtoto huyo na kuomba yeye ndiye achukue jukumu la usimamizi wa mtoto wao kwa kipindi hiki. Chriss Brown ameshinda kesi hiyo ambapo maamuzi ya jaji yaliruhusu malezi sawa kutoka kwa wawili hao ambapo Chriss anaruhusiwa kuspend siku 12 na mtoto wake kila mwezi bila masharti yoyote.
brown
Hata hivyo Nia Gozman alidai kuongezewa fedha za malezi ya mtoto kutoka USD2500 ambazo ni kama milioni 5 za kibongo mpaka USD16000 sawa na milioni 35 kwa mwezi kitu ambacho Chris alisema mzazi mwenzie anamtumia mtoto kupata pesa za kujikimu binafsi.

VIDEO: Diamond Platnumz kafunguka kuhusu Mbunge aliyetaka sanamu yake

Msanii kutoka kiwanda cha bongofleva Diamond Platnmuz amekutana na Ayo TV na kufunguka kuhusiana na Headline za yeye kuchaguliwa kwenye tuzo za BET pia kuhusiana na kwanini wasanii wa Afrika wanapewa tuzo backstage katika tuzo hizo.
Kingine kikubwa alichokizungumzia Diamond platnumz ni kuhusu Mbunge aliyetaka sanamu yake iwepo ikiwa ni njia moja ya kuthamini mchango wake kwa Taifa, unaweza kuingalia video hii hapa chini kujua alichokisema Diamond Platnumz.
ULIKOSA HII YA DIAMOND KUTANGAZWA RASMI KUWA BALOZI WA REDGOLD? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Video: Unamkumbuka mrembo aliyempata Nuh baada ya kuachana na Shilole? Wameachana lakini kuna kitu bado kinawaunganisha

Unamkumbuka yule msichana mrembo ambaye Nuh Mziwanda alimpata muda mfupi tu baada ya kuachana na Shilole? Okay, wawili hao hawapo pamoja tena lakini wana kitu muhimu wanashare.
Mziwanda-new-4
“Yule alikuwa girlfriend wangu lakini kuna kushindwana kitabia, nipo naye lakini tunachokifaya niwe naye siwezi kukisema lakini ni mtu ambaye bado tunawasiliana kwasababu kuna jambo linanifanya lazima niwasiliane naye. Lakini yeye anaendelea na mishe zake na mimi naendelea na mishe zangu,” Nuh ameiambia Bongo5.

Video: Adele – Send My Love (To Your New Lover)

Fresh off her win for Top Billboard 200 Album at the Billboard Music Awards, Adele debuted the video for her new single “Send My Love (To Your New Lover)” during Sunday’s live broadcast. Donning a floral dress, the British songstress keeps it simple in the Patrick Daughters-directed clip, using layered effects of herself spinning and dancing.

Video: Real Jofu Ft. Nay Wamitego – Unanionea

Video mpya ya msanii Real Jofu amemshirikisha Nay Wamitego wimbo unaitwa “Unanionea”.

TOP ten biggest Airplanes

http://top101news.com/wp-content/uploads/2016/05/Top-10-Biggest-Aeroplanes-Infographics.jpg

Tuesday, 24 May 2016

PICHA 4: Teknolojia inavyochukua headlines, nyumba kujengwa chini ya mwamba, Swimming pool juu yake


Teknolojia kila siku inazidi kuchukua headlines, nyumba kujengwa chini ya mwamba!!! halafu bwawa la kuogelea ndio linakuwa kama paa vile, stori kutoka kutoka CNN kuhusu nyumba hiyo ambayo itakuwa ya kwanza Duniani kujengwa ndani ya mwamba  huko Lebanon,imeingia kwenye headlines ambapo ramani yake ilitengenezwa mwaka 2015.
Nyumba hiyo inayosemekana kujengewa bwawa la kuogelea juu na kuwekea kioo kwa chini kama dari la nyumba hiyo iliyo ndani ya mwamba, bwawa lake la kuogelea linatajwa kuwa na ukubwa mara mbili zaidi ya nyumba yenyewe. Lebanon kujivunia na mpango wa nyumba hiyo.
nyumba
nyumba1 nyumba2

Nokia wapania kuteka soko la Smartphones na simu zao mpya



Leo kampuni kubwa ya simu ya Nokia imetangaza rasmi kuanza kutengeneza smart phone za kisasa kutoka kwenye kampuni yao itakayotengeneza simu hizo ya Global HMD. Kampuni hii itawasaidia Nokia kuweza kutengeneza na kuuza simu za Android na tablets.
Kumbuka kuwa kampuni ya Microsoft ndio ina haki za kuuza na kutengeneza Nokia handset toka mwaka 2014, na kwa sasa inauza haki hizo kwa kampuni ya Foxconn’s FIH  kwa dola milioni $350 millio

Harmonize na Jacqueline Wolper: Ni mapenzi ya kweli au show off?

Harmonize na Jacqueline Wolper ni couple mpya town. Kwa wengi katika hatua za mwanzoni walidhani wawili hao si wapenzi bali wanatafuta tu kiki.
c79e987f-01b7-4137-abf1-e66acf4f90cf
Lakini kadri siku zinavyoendelea kwenda, tumeshuhudia kuwa ni kweli wawili hao ni wapenzi na wanaonekana kudatishana haswaa. Kuna sababu nyingi zilizofanya watu wasiamini uwepo wa couple hiyo na kubwa zaidi likiwa ni miezi michache iliyopita Wolper alichumbiwa na mwanaume mwingine na tukaamini kuwa sasa mrembo huyo ameamua kuanzisha familia.
wolp2
Hivyo baada ya kumuona akiwa na bwana mdogo Harmonize, maswali yalikuwa mengi ya kuhusu kipi kilichotokea katika uchumba wake na mwanaume huyo. Na kwakuwa sasa tunaona kuwa wawili hao wameamua kuuweka wazi uhusiano, jibu ni kuwa Wolper na mwanaume huyo walivunja uchumba wao. Wolper anatarajiwa kuzungumza zaidi kuhusu sababu za kuachana mwanaume huyo tajiri kwenye show ya Take One ya Clouds TV leo usiku.
Sababu ya pili ni utofauti wa umri kati ya wawili hao. Harmonize ni mdogo mno kwa Wolper japo wanasema mapenzi hayaulizi kwanini na umri si kitu bali ni namba tu.
13108964_1022099581207667_748339794_n
Wakati ambao kila mtu ameshathibitisha kuwa wawili hao ni wapenzi, baadhi ya watu wanadhani kuwa mapenzi yao yamekuwa na chumvi nyingi ndani ya muda mfupi na ni kama wanalazimisha watu waamini kuwa wanapendana.
Katika wiki mbili hizi, post nyingi za Wolper ni za picha yake akiwa na mpenzi wake huyo ambaye yeye amuita Raj. “Pale mahaba yanapozidi paka macho yanaanza kufanana, u have my heart Raj,” ameandika kwenye picha moja. Harmonize bado ana aibu kiaina kuanika penzi lao lakini amekuwa akitupia picha mbili tatu za Wolper anayemuita pacha wake.
Lakini wawili hao wamekuwa gumzo zaidi wiki baada ya kuhudhuria kwenye birthday ya mtoto wa Aunty Ezekiel na Mose Iyobo, Cookie aliyetimiza umri wa mwaka mmoja. Wakiwa mbele ya Diamond na wageni wengine waalikwa, hawakuonekana kutoshana kwakuwa muda mwingi walikuwa wakishikana na kubadilisha mate bila aibu. Video inayowaonesha ‘love birds’ hao wakibadilishana mate hadharani imesambaa mtandaoni na kuzusha maswali mengi kuhusiana na jinsi wanavyoupeleka uhusiano wao. Kwa wengi wanaona kama wana show off zaidi na kwamba uhusiano wao umebeba picha ya kiki kuliko uhalisia wa watu wawili wanaopendana. Kwenye video hiyo Diamond anaonekana kutojali kilichokuwa kikiendelea kulia kwake wakati kijana wake Harmo alikuwa akishushiana mabusu na mafrench kiss ya kumwaga na ex wa bosi wake. “Mkwe leo mmejua kutuchafulia insta… yani kama sabuni ya unga uliyontolea watu MAPOVU,” ameandika Diamond kwenye post yake. 13167199_1038803779540713_504515015_n Hata hivyo kwa showbiz, uhusiano huo utamfaidisha zaidi Harmonize ambaye anaonekana kufuata nyayo za bosi wake kwa kuziteka headlines kwa story za uhusiano na mastaa.
13167199_1038803779540713_504515015_n

Drake anajenga nyumba kubwa mno kwao Toronto kiasi ambacho halmashauri itakaa kuamua iwapo aruhusiwe

Drake anajenga jumba kubwa la kifahari ambalo ukubwa wake umeufanya uongozi wa Toronto ukae chini kujadiliana iwapo aruhusiwe kuendelea na ujenzi.
13108724_727100560765504_1238839032_n

Mkutano huo utafanyika May 26 kupitia iwapo watampa ruhusa ya kuporomosha kasri lake. Mipango ya ujenzi wa nyumba hiyo ni mikubwa kuliko sheria ya Toronto inavyoruhusu.
Drake aliwasilisha mipango ya kujenga nyumba yenye ukubwa wa futi za mraba 21,000 ambako tayari ametumia zaidi ya dola milioni 6 kwenye eneo hilo lenye heka 2.
Ndani ya nyumba hiyo kutakuwa na uwanja wa kikapu, bwawa la kuogelea, jumba la sinema, jumba la makumbusho kuweka vitu vyake na vingine.

Monday, 23 May 2016

Rais Magufuli kafanya uteuzi mwingine leo May 23 2016

May 23 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wawili wa serikali, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo imeeleza kuwa Rais wa Magufuli amemteua Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Kabla ya Uteuzi huo,  Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk), Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi. Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na uteuzi huu umeanza mara moja.

Spika wa Bunge Kauweka wazi mpango huu ili kuwatambua walevi bungeni

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
May 23 2016 tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine, moja ya habari kubwa ni kutoka Gazeti la Nipashe yenye Kichwa cha habari ‘Spika afichua wabunge wavutao bangi, unga‘.
nipashe 3
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe baada ya kufanya nae mahojiano juu ya hatua ya Rais Magufuli kumtimua Kitwanga katika baraza lake la mawaziri kwa sababu aliingia bungeni na kujibu swali la Wizara yake akiwa amelewa.
Kutokana na hali hiyo Spika Ndugai amelieleza gazeti la Nipashe sasa wanafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa watunga sheria hao na kutafuta wataalamu wa ushauri nasaha watakaowapa msaada wa kisaikolojia.

PICHA 5: Icheki hapa Ndege inayotumia umeme imetengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani

Nchini Ujerumani wametengeneza Ndege aina ya LILIUM  kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yenye siti mbili, shepu ya yai na inatumia umeme, imetengenezwa na  mainjinia wanne wakijerumani wakidai kuwa ndege hiyo yenye kupunguza matumizi na kurahisisha usafiri kwa watu.
Ndege hii inasemekana kuwa na uwezo wa kwenda hadi spidi ya kilometa 400 kwa saa, kutumika  kwenye eneo tambarare, kupaa na kutua kwa mita 15. Kingine kikubwa ni kwamba inatumia umeme na inachajiwa kama simu pia haina kelele pia ni kwa ajili matumizi ya mchana tu kwenye hali ya hewa tulivu na sio usiku.
Mmoja wa msaidizi wa mmiliki wa ndege hiyo, Daniel weigand amesema wana mpango wa kuiingiza sokoni mwaka 2018, ameyazungumza haya …………
>>>”tunataka ndege isiyo na gharama kubwa wala isiyokuwa na tatizo la utumiaji wa miundombinu yake, pia iweze kutumika na watu wengi wenye uwezo wowote ule sio watu wenye uwezo mkubwa tu ndo waweze kununua ndege hii”.
lilium1
lilium2


lilum5
lilium3