HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Thursday 26 May 2016

Mayunga asema kwa sasa ana nafasi ya kufanya hata albamu na Akon

Msanii wa muziki wa Tanzania aliyefanya kazi na Akon baada ya kushinda shindano la Airtel Trace Music, Mayunga amesema nafasi ya kukutana na Akon na kufanya naye kazi imemhakikishia nafasi ya kufanya kazi nyingi zaidi.
Mayunga na Akon
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Mayumba amesema amejihakikishia nafasi ya kufanya hata albamu na msanii huyo mahiri kutoka Marekani.
“Nataka kushare na watanzania wasije wakaona Akon ndiyo basi tena, sijui nimeichezea bahati kwa Akon, labda ningemuacha na Akon aweke mistari yake mule no. Niseme tu kwamba na uwezo wa kufanya ngoma na Akon zaidi ya mbili, tatu, nne hata albamu naweza. Na hiki ni kitu ambacho nilikuwa nataka mimi, kwamba nikukutana na Akon lazima nitegeneza mahusiano ya kazi nyingine,” alisema Mayunga.

No comments:

Post a Comment