Wakati serikali ya Tanzania ikipambana kupunguza tatizo la usafiri na
msongamano wa foleni kwa wananchi wake, Wachina wameanza kugundua
teknolojia mpya ya usafiri ambayo itasaidia kupunguza foleni barabarani.
Teknolojia hiyo mpya ya usafiri haitaathiriwa na foleni za barabarani
ambayo yatakuwa ni mabasi mapana ambayo kwa chini yanaruhusu magari
kupita na kupishana bila wasiwasi wowote, huku yenyewe yakisafiri bila
kulazimika kusimama kusubiri magari yapite, isipokuwa kwenye njia panda
na kwenye taa za barabarani pekee.
Aidha basi hilo litakuwa na uwezo wa kubeba watu 1,200 kwa mara moja.
Linatajwa kuwa ufumbuzi wa msongamano wa magari barabarani. Pia,
lilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza wiki iliyopita huku magari
mengine madogo yenye urefu wa futi 6.6 yanapita chini ya gari hilo jambo
ambalo linaelezwa hupunguza idadi ya magari kwenye msongamano. Basi
hilo linalotumia umeme na inaelezwa kwamba, linaweza kusafiri kilomita
60 kwa saa moja.
Shenzhen Hashi ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya China TBS Limited
iliyohusika kutengeneza magari hayo amesema wametumia kiasi cha dola
74.1 kutengeneza basi hilo moja ambalo utengenezaji wake ulianza tangu
mwaka 2010.
Tazama video hapa
No comments:
Post a Comment