HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday 25 May 2016

Maamuzi ya kesi ya Chriss Brown kuhusu malezi mabovu ya mtoto wake ‘Royalty

Kesi iliyokuwa inamkabili  staa kutoka  Marekani Chriss Brown juu ya malezi mabovu ya mtoto wake ambayo ilifunguliwa na mzazi mwenzake Nia Guzman, May 24 maamuzi yalitolewa na Mahakama ya Califonia.
Mama mtoto wa Royalty alidai kuwa Chris hana malezi sahihi na muongozo unaostahili juu ya mtoto wao, amesema Chris amekuwa akivuta sigara na bangi yeye na marafiki zake mbele ya mtoto wao na imempelekea Royalty kupata maradhi ya pumu.
cbbbb
Nia Guzman aliomba mahakama impunguzie Chris muda wa malezi ya mtoto huyo na kuomba yeye ndiye achukue jukumu la usimamizi wa mtoto wao kwa kipindi hiki. Chriss Brown ameshinda kesi hiyo ambapo maamuzi ya jaji yaliruhusu malezi sawa kutoka kwa wawili hao ambapo Chriss anaruhusiwa kuspend siku 12 na mtoto wake kila mwezi bila masharti yoyote.
brown
Hata hivyo Nia Gozman alidai kuongezewa fedha za malezi ya mtoto kutoka USD2500 ambazo ni kama milioni 5 za kibongo mpaka USD16000 sawa na milioni 35 kwa mwezi kitu ambacho Chris alisema mzazi mwenzie anamtumia mtoto kupata pesa za kujikimu binafsi.

No comments:

Post a Comment