HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Monday, 23 May 2016

Rais Magufuli kafanya uteuzi mwingine leo May 23 2016

May 23 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wawili wa serikali, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo imeeleza kuwa Rais wa Magufuli amemteua Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Kabla ya Uteuzi huo,  Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk), Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi. Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na uteuzi huu umeanza mara moja.

No comments:

Post a Comment