Akizungumza na waandishi Alhamisi hii katika maandalizi ya Tamasha la Siku ya msanii litalofanyika katika Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho kuanzia Septemba 24 hadi 26 mwaka huu, Juma Nature alisema anashangaa kuona hata yeye nyimbo zake hazipigwi katika baadhi ya radio.
“Kama wanataka fedha ili wapige nyimbo katika redio zao waweke wazi itambulike kuwa mtu anapokuja na nyimbo ama albamu yake ili ipigwe anatakiwa alipie kiasi fulani badala ya hali mbaya ilivyo sasa katika muziki,” alisema Nature.
“Roho inauma wasanii tunateseka sana, lakini nyimbo hazipigwi. Kama mimi ni msanii mkubwa nyimbo zangu zisipopigwa roho yangu hainiumi sana, lakini hawa chipukizi wanaotakiwa watoe pesa ndiyo nyimbo zao zipigwe, wanapata wapi hizo fedha ni bora watangaze kiasi kimoja lijulikane moja,”
Pia msanii huyo alisema vituo vingi vinapiga nyimbo nyingi za Nigeria kuliko za ndani hali ambayo inaudhoofisha muziki wa ndani.
Juma Nature sio msanii wa kwanza kulalamika rushwa kwenye vituo vya redio, pia Ben Pol aliwahi kulalamikia suala hilo.
No comments:
Post a Comment