Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya Mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young, Ikulu Jijini Dar es Salaam na baada ya mazungumzo hayo Rais Magufuli amepokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salender litakalojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi huyo.
Daraja hilo litakuwa na urefu wa
kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake
unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani na unatarajiwa kukamilika mwaka
2020 na daraja hilo litasaidia kupunguza adha ya msongamano wa magari
katika Jiji la Dar es Salaam.
Ujenzi wa
Daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo Agha
Khan kupitia baharini Jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza Mwezi Juni
Mwakani baada ya Serikali ya Tanzania kukamilisha mchakato wa
upatikanaji wa fedha za ujenzi kutoka benki ya Exim ya Korea.
>>>’Mchakato
wa kulijenga hili daraja la Salender unaendelea vizuri kwa sababu hivi
sasa kampuni ya Kikorea ambayo inafanya usanifu ipo kwenye hatua za
mwisho na zabuni zinategemewa kutangazwa mwezi wa tatu Mwaka kesho na
zitakwenda haraka, kwa hiyo mambo yakienda vizuri ujenzi unaweza kuanza
mwezi wa sita, bahati nzuri fedha zote zipo na zimeshatolewa na Benki ya
Exim ya Korea’:- Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment