HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday 21 September 2016

Trey Songz atua Nairobi kushiriki Coke Studio Africa msimu wa 4


Muimbaji wa RnB kutoka Marekani, Trey Songz ametua mjini Nairobi, Kenya kushiriki kwenye msimu wan nne wa kipindi cha Coke Studio Africa.
14262650_862277083907144_2037035864_n
Trey Songz baada ya kutua uwanja wa ndege nchini Kenya
Muimbaji huyo anatarajiwa kurekodi nyimbo na baadhi ya wasanii wengine wa Afrika ambao watashiriki kwenye kipindi hicho akiwemo Vanessa Mdee (Tanzania), Rema Namakula (Uganda), Yemi Alade (Nigeria), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), Nyashinski (Kenya) na Emtee (South Africa).
lunch
Trey Songz akila chakula cha mchana na washiriki wengine wa kipindi cha Coke Studio
Uongozi wa kipindi hicho umeandika ujumbe kwenye mtandao wao wa Instagram unaosomeka, “Welcome to Nairobi Kenya Trey Songz, it is a great honour to host you for #cokestudioafrica.”
Hii ni mara ya tatu kwa msanii kutoka Marekani kushiriki kwenye kipindi hicho, wengine waliowahi kushiriki ni pamoja na Wyclef Jean na Ne-Yo.

No comments:

Post a Comment