HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Saturday, 8 October 2016

Mwanafunzi aliyepigwa na walimu Mbeya afunguka A – z.

mwanafunzi

Mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyekuwa akisoma Mbeya Day, Sebastian Chinguku ameelezea jinsi alivyoshambuliwa kwa kupigwa na walimu zaidi ya mmoja
Anadai mkasa mzima ulianza baada ya kupewa kazi na mwalimu wake lakini kutokana na kuwa mgonjwa alishindwa kuifanya mapema. “Wakati Jumatano nawasili naenda shule, mwalimu yeye ndio alikuwa anadai hiyo kazi siku hiyo, baada ya yeye kudai hiyo kazi, mwalimu akasema ‘ambao hawajafanya hiyo kazi wapite hapa mbele’ mimi ni kawa ni mmoja wapo, nikapita mbele. Nikamuelezea mwalimu jinsi ilivyokuwa, nikamwambia mwalimu ‘nilikuwa naumwa na ndio maana sikuweza kufanya kazi yako.’ Mwalimu hakunisikiliza akasema sisikilizi maelezo ya mtu yeyote, basi nikaona tu haina haja nikakubali kuadhibiwa na wenzangu,” alisimulia. “Huyo mwalimu Frank Msigwa akawa amenichapa fimbo tatu round ya kwanza wote, kabla ya kuanza kutuchapa aliwaita walimu wenzake waje kumsaidia kutuadhibu. Wale walimu walipofika walikuwa wanne kwa wakati mimi nilipoadhibiwa fimbo tatu za mara ya kwanza, wakati wenzangu wanarudiwa kupigwa fimbo kwa mara ya pili, kuna mwalimu tu mwingine kwa jina simfahamu akawa ameniita nyuma ya darasa maanake walimu wote wakati wote wakati huo tulikuwa mbele lakini mwalimu huyo aliniita nyuma ya darasa. Basi nilivyoenda pale kumsikiliza,akaniambia ‘unanikumbuka?’ Nikamwambia ‘hapana’ kama unakumbuka kipindi kile sisi tunafanya mitihani waliniambia kwamba nivue sweta nikagoma, nikawaambia ‘hapana sikugoma’ nikamwambia ‘mbona nilikuelezea kwamba nilikuwa naumwa kifua ndio maana nikashindwa kuvua sweta!’ “Basi akatokea huyo mwalimu Msigwa akadakia ‘mi mhuni mhuni’ akawa anatoa hizo kauli akasema kwamba nipige magoti. Sasa na mimi nikataka kujua nikamuuliza ‘mwalimu kwani nina kosa gani kama nikutokufanya kazi yako si ndo hii ambayo umetuadhibu kwa pamoja?’ Basi mwalimu hakutaka kunielewa. Akasema ‘kwahiyo unabisha?’ nikamwambia ‘hapana mwalimu nilichotaka kujua kosa langu ni kosa gani basi.’ “Mwalimu akaanza kunirushia ngumi za kwenye bega wanafunzi wakawa wamemshika mwalimu na walimu wale watatu walikuwa wamenishika mimi. Baada ya kunishika hapo wale wanafunzi wenzangu wakawa wamemuachia yule mwalimu, mimi wale walimu wakawa hawajaniachia wakaanza kuniburuza toka darasani mpaka staff room ofisi ya walimu. Tulivyofika staff wakanifungia mlango na kuanza kunipiga kama inavyoonekana kwenye clip. Walivyonipiga kuna mwalimu aliyekuwa anashuti ile video akawa ananiombea msamaha ‘msameheni’ lakini walimu wale hawakusikia. Baada ya yule mwalimu kuniombea sana wakaona waniadhibu tu fimbo kama fimbo wakati huo nimeshapigwa kama kwenye ile clip inavyoonekana. Wakaniadhibu tena fimbo saba baada ya kupigwa hapo tena,” aliendelea kueleza. “Wakaniambia wanitoe staff wanipeleke tena darasani wakaniadhibu tena mbele ya wanafunzi kwa mara nyingine tena. Sasa wakati tunatoka kwanza mimi nikamwambia ‘mwalimu mbona mmenichapa sana na kila sehemu ya mwili wangu sasa hivi inauma, naomba basi mnipe adhabu nyingine.’ Wale walimu hawakunielewa wakawa wamenibeba wamenishika wanataka kunipeleka darasani, sasa wakati tunatembea tunakaribia kufika darasani na mimi nikaona nijitetee nikakimbia. Wakati nakimbia mwalimu akawa amenishika mkono alivyonishika mkono akanirudisha tena darasani. Nilivyopelekwa darasani wakaniambia nikae chini. Nikawa nimekaa chini, walimu wakawa wanaongea tena na wanafunzi. Sikukaa dakika chache tu mwalimu yule akanirudia tena mbele ya wanafunzi akanipiga teke sehemu ya jicho. Jicho likawa limevimba na kukawa na mchubuko unatoa damu na nikawa natoka damu puani na mdomoni pia.” Tayari Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ametangaza kufukuzwa chuo walimu hao waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika shule hiyo. Pia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, HELSB, imetoa taarifa ya kusitisha mikopo kwa walimu hao.

No comments:

Post a Comment