Baada
ya kuwepo kwa hatua mbalimbali za wanafunzi wa vyuo kudai ongezeko la
fedha ya kujikimu na kupatiwa mkopo kwa wanafunzi ambao hawajapatiwa
mikopo na baadae Wizara kuahidi kushughulikia suala hilo.
Leo
October 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli
za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Rais Magufuli wakati
akihutubia amegusia suala la mikopo ya wanafunzi ambapo amesema……..
>>>’Vyuo
vyote vya elimu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua, ukishafungua
kwa haraharaka wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawaambia kufanya
usajili lazima walipe wakati bodi haijatoa orodha ya majina ya vijana
watakaokopeshwa, lazima kuwepo na mawasiliano kati ya bodi ya mikopo,
TCU, wizara ya Elimu na wizara ya fedha’
>>>’lengo la
serikali si kuleta usumbufu kwa wanafunzi, lakini ni ukweli pia haitatoa
mkopo kwa wanafunzi wenye uwezo, mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo?,
mtoto wa katibu mkuu Kijazi naye apate mkopo? haiwezekani, mkopo huu
umelenga kwa ajili ya kutoa watoto maskini lakini nasikia kule kuna
upendeleo fulani katika kutoa mkopo sasa hili Waziri na bodi
zinazohusike msimamie’;-JPM
Baada ya kuwepo kwa hatua mbalimbali za wanafunzi wa vyuo kudai ongezeko la fedha ya kujikimu na kupatiwa mkopo kwa wanafunzi ambao hawajapatiwa mikopo na baadae Wizara kuahidi kushughulikia suala hilo.
Leo October 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Rais Magufuli wakati akihutubia amegusia suala la mikopo ya wanafunzi ambapo amesema……..
>>>’Vyuo vyote vya elimu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua, ukishafungua kwa haraharaka wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawaambia kufanya usajili lazima walipe wakati bodi haijatoa orodha ya majina ya vijana watakaokopeshwa, lazima kuwepo na mawasiliano kati ya bodi ya mikopo, TCU, wizara ya Elimu na wizara ya fedha’
>>>’lengo la serikali si kuleta usumbufu kwa wanafunzi, lakini ni ukweli pia haitatoa mkopo kwa wanafunzi wenye uwezo, mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo?, mtoto wa katibu mkuu Kijazi naye apate mkopo? haiwezekani, mkopo huu umelenga kwa ajili ya kutoa watoto maskini lakini nasikia kule kuna upendeleo fulani katika kutoa mkopo sasa hili Waziri na bodi zinazohusike msimamie’;-JPM
ULIKOSA HAYA MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI KWA TCU KUHUSU ONGEZEKO LA VYUO VIKUU NCHINI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment