Wakati
magazeti ya leo yakitoka na habari iliyosema kuwa wanafunzi wa vyuo
66,000 kukosa mikopo, taarifa hizo zilidai kuwa wanafunzi 88,000
walioomba mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,
wengi hawatapata.
Taarifa
hizo zilizochapishwa na gazeti la mwananchi la October 20 2016 zimesema
kuwa uwezo wa bodi hiyo ni kutoa mikopo kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa
na asilimia 24 na waliopatiwa hadi sasa ni wanafunzi 11,000 sawa na
asilimia 12.
Wakati
hayo yakielezwa leo October 20 2016 baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu
cha Dar es salaam wakiongozwa na viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa
chuo hicho ‘DARUSO’ wamefika Wizara ya elimu wakiwa na hoja kuu mbili,
uchache wa majina ya wanuafaika wa mikopo yaliyotoka mpaka hivi sasa na
hoja ya pili ni kuhusu vigezo ambavyo vimetumika kwenye fedha ya
kujikimu kwa wanafunzi.
Hata hivyo
baada ya kufika wizarani hapo wanafunzi hao wamesema hawakupata nafasi
ya kumuona waziri wa elimu lakini wamefikisha hoja zao kwa katibu mkuu
wa wizara na ametoa ahadi ya kushughulikia hoja hizo.
No comments:
Post a Comment