HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday 31 August 2016

VideoFUPI: Diamond Platnumz anunua Rolls Royce ya $400,000 na zaidi?



Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines siku ya February
1 2016 ni hii ya msanii wa Bongofleva na CEO wa record label ya Wasafi Classic
 Baby (WCB) Diamond Platnumz kuweka
 wazi kuwa kabla ya mwaka 2016 kumalizika atanunua gari aina ya Rolls Royce.
 Kupitia account yake ya instagram usiku wa August 30 Diamond Platnumz  
 alipost clip video ya Rolls Royce yenye kivuli cha sura yake, inawezekana 
Diamond akawa ametimiza ahadi yake ya kumiliki gari hilo kabla ya mwaka 2016
kumalizika, kama Diamond atakuwa kanunua gari hilo atakuwa ni mtanzania wa pili
 anayefahamika kumiliki Rolls Royce baada ya makamu mwenyekiti wa zamani wa
Yanga Davies Mosha.
Baadhi ya mastaa Afrika wanaomiliki gari aina ya Rolls Royce ni Koffi Olomide na
 staa wa soka wa zamani wa Arsenal Emmanuel Adebayor ambaye kwa sasa anaichezea
 Crystal Palace, bado haijajulikana Rolls Royce aliyopost  Diamond ni toleo la mwaka gani
 ila stori kutoka autoguide.com inaeleza kuwa Rolls Royce inauzwa zaidi ya dola laki 3
ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600 pia inategemeana na toleo.

IMG_20160122_182043



No comments:

Post a Comment