HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Monday, 11 July 2016

Usher Raymond atinga Tanzania July 10


Ugeni mwingine ambao Tanzania imekua ikitarajiwa kuwa nao toka juzi ya July 9 2016 ni ujio wa mwimbaji staa kutoka Marekani Usher Raymond ambaye anakuja Tanzania na moja kwa moja kwenda mbugani Serengeti.
Taarifa zilizosogezwa karibu yangu ni kwamba Usher anacho kibali cha kuwinda na uwindaji ataoufanya ni kwa kutumia Upinde na mkuki na ni kuanzia July 10 mpaka 19.
Usher anakua sio staa wa kwanza wa dunia kuja mbugani Serengeti nchini Tanzania, wengine wengi wameshawahi kuja akiwemo Mtangazaji Oprah Winfrey ambapo wengi wao huja lakini kwa kutotaka kutangaza au ijulikane, mpaka akiondoka ndio unaona kapost kwamba alikuwepo Tanzania.
Nilipojaribu kuutafuta uongozi kupata taarifa za zaidi nimeambiwa mara nyingi Mastaa wengi hupenda kujificha wanapokuja na hata hawataki ijulikane na wakati mwingine hawataki kupigwa hata picha lakini ikitokea chochote millardayo.com itakusogezea

No comments:

Post a Comment