Jeshi la
polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watatu
wakazi wa buguruni kwa kosa la kukutwa na nyaraka bandia za serikali
kama vyeti vya kidato cha nne, stika za SUMATRA, vyeti vya vyuo vya
uuguzi, vyeti vya kuzaliwa, leseni bandia za biashara, nyaraka za bima
pia walikutwa na mihuri mbalimbali ya ofisi za serikali na binafsi.
Watuhumiwa
wote bado wapo rumande na upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani, baada ya mahojiano na polisi watuhumiw hao wamekiri kuuza
vyeti watu wengi ambao wako kwenye ajira.
Akizungumza na waandishi wa habari kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema……….>>>’Wanataja
na wanaendelea kutaja watu ambao wamewauzia vyeti na wameshapata ajira
serikalini, kama ulinunua hiki cheti, nataka niseme ni balaa kwako kwa
sababu watatutajia kila mmoja mmoja na tutakufuata huko ulipo’.
>>>’Hatuishi
hizi nyaraka tulizozipata tutakwenda mbali zaidi kwa kuwanyofoa mmoja
mmoja aliyejipatia kazi kwa kutumia hivi vyeti bandia
No comments:
Post a Comment