Mix
Ni June 16, 2016 ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki walizifungia simu feki zenye IMEI bandia
Sasa millardayo.com imepata meneja wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy na kueleza idadi ya IMEI zilizokamata na mtambo wao ambao umehusika kuzifungia simu feki.
‘Tukizungumzia ambavyo vimezimwa
kinachofanyika kuzifunga zile IMEI bandia ambazo kwa jana tumefanikiwa
kuzifunga simu zenye IMEI zipatazo laki sita na elfu 3 kwa maana ya
kwamba unakuta simu moja ina IMEI mbili kwasababu simu yenye laini mbili
ina IMEI mbili sasa ziko simu zenye IMEI hadi nne‘- Innocent Mungy
‘Kwahiyo
ambacho tumeblock jana usiku ni IMEI laki sita ikiwa ina maana ni
ambazo zinatumika kwenye simu feki, modem ya internet na IPAD, sasa sisi
hatuwezi kutaja idadi ya simu ngapi tumezifungia ila tunachokijua ni
kwamba IMEI laki sita ndio zimefungiwa zilizopo kwenye simu‘– Innocent Mungy
‘Zoezi hili bado linaendelea
ambapo sasa hivi mtambo utakuwa unahakikisha simu zinazoingia bandia
zitakuwa zinafungiwa, IMEI ni namba tambulishi kama unakumbuka tulisema
kwamba kila simu inayotengezwa inapewa namba tambulishi, sasa simu ili
itengenezwe lazima ipite kwenye mchakato wa kuhakikisha kuna vitu
ambavyo havitakiwi viwepo kwenye simu- Innocent Mungy
KAMA ULIIKOSA HII YA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ALIVYOGEUZA GARI AKIELEKEA KAZINI ITAZAME HII VIDEO HAPA
No comments:
Post a Comment