HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 17 June 2016

Video: Ray C apewa msaada na Jeshi la polisi ya baada kuzidiwa


Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C usiku wa jana alikamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Kinondoni Manyanya almaarufu ‘Kinondoni kwa Mpemba’ jijini Dar es salaam baada ya kupiga makelele barabarani akidai anataka kutekwa.
Ray C akiwa kwenye gari la polisi
Ray C akiwa kwenye gari la polisi
Muimbaji huyo mahiri ambaye ameathirika na Matumizi ya madawa ya kulevya, alidaiwa kufika katika eneo hilo na kuomba msaada lakini baadae aliomba kisu ili ajichome kuhu akiongea vitu visivyoeleweka.
Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni msanii wa filamu, Esha Buheti kupitia instagram yake aliandika ujumbe huu:

Nashindwa hata niongee nini jamani, rayc Leo kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie rayc, I mean it jamani siku zote nlikua najua anaonewa ila nlichokishuhudia leoo nimeumiaa kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje? . Nilikuwa na Kabula Kinondoni kwa wapemba tumefata chips mara tukaskia mtu anasema me Rayc nataka kuvua nguoo, nikajua utani kushuka ni Ray C anasema nishikeni kuna watu wanataka kuniteka, alikua na nguvu sana watu kamshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaaanza kugaragara kwenye matope akipiga KELELE kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari YA polisi ikambeba ila kwa tabu sanaa alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpk rayc anaondoka na ile gari yapolisi sikujua anapelekwa wapi alikua kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?
Baada ya ujumbe huo, aliamua kupost video tena na kuandika:

Ray C hastahili haya jamani kweli Leo hii anafikia hatua hii? Najua hajitambui ila tumfikirie mwanamke mwenzetu ambae ni mamaake, anajiskiaje? Rayc nn kimekupata ? Hiii video inasambaa kila sehem kweli huyu ndo RAYC AMBAE NI NEMBO YA TAIFA? Plz tumsaidie manake tusimhukumu? MBONA sisi kila siku mungu tunamkosea na hesabu makosa yetu? We need to do something jamani @tzshaderoom @mangekimambi_ @divathebawse @babutale @ @mwanafa @linexsundaymjeda @paulmakonda naomba tumstiri huyu mtu plz plz @lisa_fickenscher ( tunafanyaje kumsaidia jamani tusichoke me natamani aende rehab mwaka mzima) Leo rayc umedhalilika najua haikua akili yako mama DAAAAH hata sijui amepelekwa wapi maskini 😒😒 atakua amelala wapi? Vipi kuhusu kesho Yake? Mamaake anajiskiaje? Inaumaa jamani tusikubali kumpoteza huyu dada nawaombaa πŸ™πŸ™πŸ™ tusaidiane @millardayo @rayc1982 my love kama hauko sawa jamani ongea na watz wapo tayari kujitolea kwa hali na mali my love,

No comments:

Post a Comment