Taarifa hii kutoka Benki ya Dunia ambayo imetoa ripoti
ya ustawi wa uchumi wa Afrika ambapo nchi za Afrika Mashariki za
Tanzania na Rwanda zinaonekana kuwa na uchumi wenye kustawi kwa wastani.
Ripoti
mpya ya Benki ya dunia itolewayo mara mbili kwa mwaka, Africa’s Pulse,
inaonesha kuwa mwelekeo wa ukuaji uchumi barani Afrika unatarajiwa
kudorora zaidi na kuwa asilimia moja nukta sita mwaka huu ikilinganishwa
na asilimia tatu mwaka jana.
Hata hivyo
imebainisha kuwa, mwelekeo wa ukuaji unatofautiana ambapo baadhi ya
nchi ustawi umedorora huku nyingine uchumi unakua. Kwa mfano Rwanda,
Tanzania na Ethiopia zimetajwa kuwa nchi zenye ustawi wa wastani ambao
ni zaidi ya asilimia sita kwa mwaka, huku Cote d’Ivoire na Senegal
zikiongoza kwa kasi ya ustawi barani Afrika.
Mchumi
Mkuu wa Benki ya dunia kuhusu Afrika Albert Zeufack amesema chanzo cha
kukwama ustawi wa uchumi ni kudorora kwa bei za bidhaa ikiwemo mafuta,
hali ngumu ya kifedha na sera za uchumi zisizo makini.
Benki ya
Dunia inasema mwelekeo ni kupanua wigo wa bidhaa zinazouzwa pamoja na
kuboresha sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo ili kuinua
vipato vyao na kupunguza umaskini.
No comments:
Post a Comment