HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Thursday 29 September 2016

Ndalichako aitaka bodi mpya ya TCU kukaza msuli

Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ameitaka bodi mpya ya tume ya vyuo vikuu TCU kushughulikia changamoto zilizopo katika tume hiyo baada ya ile iliyokuwepo kuvunjwa.

ndalichako
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo, Profesa Ndalichako, alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusiana na vyuo wanavyosoma hivyo ni wakati wa bodi hiyo kufuatilia kwa ukaribu malalamiko hayo na kuyafanyia kazi.
“Tunaelewa kuwa wanafunzi ni watu wa kulalamika kila wakati, lakini yapo malalamiko ambayo yana tija na ni lazima yatatuliwe,” alisema. “Kwa mfano nilipokea malalamiko kutoka chuo kikuu cha Ifakara mwezi Mei mwaka huu kuhusiana na walimu wa chuo hicho kuvuruga matokeo yao lakini chuo hicho hakijatoa maamuzi yoyote mpaka leo hivyo kuwaacha wanafunzi kubaki nyumbani na kutokujua nini hatma yao,” alieleza Profesa Ndalichako.
Aidha alisema TCU ina mamlaka ya kuvifuatilia vyuo vyote vikuu nchini, pamoja na kufuatilia utendaji kazi wa vyuo hivyo ikiwa unaendana na viwango vilivyowekwa.

No comments:

Post a Comment