Msanii wa vichekesho na muimbaji, Kingwendu amesema angependa kuwa na msimamizi wa shughuli zake katika sanaa ya muziki ili aweze kutoka badala ya kutegemea uchekeshaji peke yake
Akizungumza na Times Fm, Kingwendu alisema kuwa amekuwa akitoa nyimbo
mbalimbali lakini bahati mbaya hazipati nafasi ya kusikilizwa kwenye
vituo vya redio kwa ajili ya kumtangaza.
“Nimegundua kuwa sababu kubwa ambayo inanikwamisha kutoka kimuziki ni
kukosa meneja wa kusimamia kazi zangu, hivyo najaribu kuangalia
uwezekano wa kumpata,” alisema kingwendu.
Msanii huyo alisema kuwa ana uwezo wa kupambana na wasanii wa muziki
wa kizazi kipya wanaotamba kwa sasa na kuwabwaga iwapo atapata meneja wa
kusimamia kazi zake vizuri.
“Hao wanaotamba sasa ni kwa sababu wana watu wa kusimamia kazi zao na
mimi nitafanya hivyo ndipo mtaamini kile ninachokisema kwamba nina
uwezo mkubwa wa kuimba ila ninakosa usimamizi tu,” alisema
No comments:
Post a Comment