HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Wednesday 27 April 2016

VIDEO: Tatizo la vijana kukosa ajira halijaachwa kimya bungeni leo




Vikao vya Bunge vimeendelea tena leo April 27 2016, katika kipindi cha maswali na majibu
 moja ya Wizara zilizopata nafasi ya kujibu maswali ya wajumbe ni pamoja na Wizara 
ya Kazi, Vijana na Ajira, ambapo swali kutoka kwa Esther Michael Mbunge wa viti
 maalumu aliuliza>>
Serikali kupitia Taasisi za umma zimeweza kufanya tafiti nzuri kujua uhalisia wa
 suala la ajira kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu‘ –Esther Michael
Je, ni kwa namna gani Serikali inaweza kutumia majibu ya tafiti hizo kutatua 
changamoto za ajira katika nchi yetu?’-Esther Michael
Majibu yakatolewa na Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde 
 ‘Serikali kupitia Wizara imekuwa ikifanya au kutumia tafiti mbalimbali 
 kushughulikia changamoto za ajira, upangaji wa mipango na utatuzi wa changamoto
 za ajira kwa vijana wa vyuo vikuu na wengineo‘ 
Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwezeshaji kwa vijana na wahitimu wa
 vyuo vikuu ili kutatua changamoto za ajira katika nchi yetu‘ –Antony Mavunde




UMEWAHI KUMSIKIA PROF JAY AKIONGEA BUNGENI? HUYU HAPA SASA?

 

No comments:

Post a Comment