Monday, 25 April 2016
Raymond asimulia jinsi alivyomshawishi Diamond hadi kumchukua WCB (Video)
Raymond amesimulia jinsi ambavyo alimshawishi Diamond hadi kuamua kumchukua kwenye
label yake, WCB
Alisema kuwa alipigiwa simu na mshkaji wake, Maromboso aende studio kuungana
naye katika kusikiliza wimbo wa Diamond aliokuwa anataka mawazo ya watu wengi.
“Brother Diamond akifanya ngoma anapenda management yake, kuanzia madancer,
mameneja wote waweze kusikiliza wimbo wake. Katika hiyo crew ya watu waliokuwepo
Maromboso akapendekeza na mimi niwepo,” amesema
Anasema baada ya kumshauri vitu kadhaa Diamond aligundua ana kitu cha ziada na kumuuliza kisa cha kutotoka hadi muda huo. Amedai kuwa Diamond alimuomba nyimbo zake azisikie na akawa anamshauri vitu vya kurekebisha. Aliendelea kurekodi nyimbo kwenye studio mbalimbali na kuwa anamtumia hadi alipofungua studio ya WCB.
Anasema kuwa kwenye studio hiyo alirekodi nyimbo nyingi kali zilimchanganya Diamond na uongozi wake hadi wakashindwa watoi upi.
Ray ameongeza kuwa Bado ilitoka kwa mbinde kwakuwa kulikuwa na nyimbo zingine kali sana. Mtazame hapo juu kumsikia akielezea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment