Shirika la Afya Duniani lilikusanya taarifa za sababu za vifo mwaka 2012 na kuzifananisha na sababu kubwa za vifo mwaka 2000. Magonjwa ya moyo yamekuwa ni sababu kubwa ya vifo duniani kwani vimesababisha vifo vya watu milioni 7.4 mwaka 2012. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile shambulio la moyo, saratani na kisukari yamesababishwa 68 % ya vifo vyote duniani mwaka 2012, kutoka 60% mwaka 2000.
Ikilinganishwa na mwaka 2000, vifo vinavyotokana na HIV vimepungua kidogo, kipindupindu sio tena miongoni mwa sababu tano za juu zinazoongoza kwa vifo kwani imepungua kutoka vifo milioni 2.2 mwaka 2000 hadi milioni 1.5 mwaka 2012 . Vifo vinavyotokana na kifua vimepungua kutoka milioni 1.3 hadi milioni 1, na kifua kikuu hakipo tena kwenye top ten ya sababu za vifo.
Top 10 ya sababu zinazoongoza kwa vifo duniani
- Shambulio la moyo 13.2%
- Kiharusi 11.9%
- Pumu 5.6%
- Maambukizi ya njia ya hewa 5.5%
- Saratani ya mapafu na njia ya hewa 2.9%
- Virusi vya Ukimwi 2.7%
- Ugonjwa wa kisukari 2.7%
- Ugonjwa kuhara (Kipindupindu) 2.7%
- Ajali za barabarani 2.2%
- Shinikizo la damu na magonjwa ya moyo 2%
No comments:
Post a Comment