Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Rose Ndauka amesema aliumia kwa sababu alishatangaza kwa watu, kwamba anatarajia kufunga ndoa.
“Kiukweli iliniumiza sana, kwa sababu mpaka tumefikia hatua tufunge ndoa, na nilikuwa naamini kuwa siku chache zijazo Rose sio Rose tena bali ni Mrs fulani,” alisema Rose. Lakini mimi naamini ndoa inapangwa na Mungu, ilipofika mwenyezi Mungu hakuhitaji kile kitu kifanyike, basi nikamshukuru Mungu,”
Rose alisema kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mtu mwingine huku akidai kuwa hawezi kupata mtoto mwingine nje ya ndoa.
No comments:
Post a Comment