HUBATI.COM








THANK YOU FOR YOUR VISIT               

Translate

Search This Blog

Friday, 6 May 2016

Hasira za ugomvi wa mapenzi zilivyohamia kwenye gari

Picha za gari lililokuwa na ujumbe wa kukasirisha uliochorowa katika gari hilo zimesambazwa mara elfu katika mtandao wa Twitter.
160505150553_carklo2
Gari hilo jeupe aina ya Range Rover Revere lenye bei ya pauni 75,000 lilionekana limeegeshwa karibu na Harrods magharibi mwa London na kuchorwa ujumbe wa kukasirisha kwa kile kilichoonekana kuwa mpenzi aliyedanganywa.
Gari hilo liliandikwa ‘cheater’ { mwongo} katika pande zote mbili za gari huku maneno ”Natamani angekuwa na thamani” yakiandikwa katika madirisha ya gari hilo.
160505150536_carklo4
Klo ambaye alipiga picha za gari hilo alisema kuwa alimuona mwanamke mmoja akilichora gari hilo,alikuwa kama aliye na wazimu.
“Hakuna mtu aliyejaribu kumzuia. Baadaye aliondoka, ‘Its Over’ ni moja ya neno lililoandikwa kwenye gari hilo ikielezea kuisha kwa uhusiano wowote,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment